Ardhi mafia kunanuka rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ardhi mafia kunanuka rushwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mizizi, Feb 25, 2009.

 1. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Katika hali ya kusikitisha, sekta ya utalii baada ya kuleta tija na matumaini kwa ukombozi wa mtanzania wa hali ya chini, huku mafia hali ni tofauti kwa sekta ya utalii kutokuwa na maana halisi kwa kuwa wawekezaji wake kutumia njia za ujanja ujanja.

  Lakini hali inakuwa ya kusikitisha zaidi ni pale hata viongozi na idara za serikali zinaposhiriki kudhulumu wenyeji na kuwapa ardhi wanaojiita wawekezaji kwa njia za utata. Kwa mfano, Hapa mafia kuna mwekezaji mmoja ambaye alifika mwaka 1992 na kufanya makubaliano na baadhi ya wenye ardhi sehemu za kandokando ya bahari kwenye kijiji chetu cha kiegeani. Katika makubaliano hayo mwekezaji huyo mwenye asili ya Australia, anayejulikana kwa jina la Peter Byrne alifanya mikataba ya kukodi maeneo hayo kwa muda wa miaka 15 kuanzia tarehe 14/051993. Mambo mengine yaliyomo kwenye makubaliano hayo ni kwamba, wenye eneo hilo kuendelea kuvuna mazao yaliyokuwemo ndani ya eneo walilokodisha, yakiwemo nazi na korosho, kulipa kodi ya ukodishaji kwa kipindi chote kiasi cha shilingi laki sita kila shamba. Katika Mkataba huo Bwana Peter Byrne ambaye alikodi kama mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Sokwe Camp Ltd yenye anwani ya P.O.Box 3052 Arusha, Tanzania, alilipa kiasi cha fedha kupitia aliyekuwa afisa ardhi wilaya ya Mafia wakati huo ambaye alijulikana kwa jina la A.F. Mapunda.

  Lakini baada ya kuisha mkataba wa mwanzo wa miaka 15, hapo tarehe 14/05/2008 mwekezaji huyu akazuia wenye mashamba kuingia kwenye eneo alilokodishwa kuendelea kuvuna mazao yao kama makubaliano yalivyokua. Lakini hali ya utapeli ilionekana pale wenye maeneo walipomfuata na kumkumbusha juu ya kufanya mazungumzo juu ya kufanya mkataba mwengine ndipo alipowafukuza na kuwaeleza kwamba eneo lile ni la kwake na ameshauziwa na serikali na kuwaeleza kwamba yeye ana hati zote za umiliki wa maeneo hayo.

  Lakini baada ya kufuatilia Idara ya ardhi wilaya, wao wamekana kushiriki na kutojua hati hizo amezipata wapi.

  Lakini baada ya ufuatiliaji zaidi, tukapata nakala za umiliki wa ardhi wa kiwanja nje ya eneo la hoteli ambalo linaonyesha mmiliki wake ni Bwana peter Byrne. Lakini cha kushangaza zaidi, katika ramani iliyopo idara ya ardhi inaonyesha kwamba eneo ilipojengwa hoteli hiyo ni viwanja vinne tofauti, kimoja ni cha wenye eneo na vitatu ni maeneo ya kijiji, ambayo mwekezaji huyo alijenga kinyume na sheria bila hata kufanya makubaliano na serikali ya kijiji ama mamlaka ingine yoyote. Hata hivyo, jina la mmiliki wa kiwanja hicho namba 20 kilichokuwa na hati, mmiliki wake si kampuni ya Sokwe camp limited kama ilivyoingia mkataba na wenye maeneo, bali ni Kinasi Limited. Pia cha kutia shaka zaidi, katika hati yake hiyo yenye namba 44742 ya tarehe 29/08/1995 imesainiwa sehemu zote na ofisa mmoja tu, huyo huyo anaonekana ni stamp duty officer, assistant registrar of tittles na Registrar of titles. Hati hiyo ambayo inaonyesha kopi yake imepelekwa kwa kamishina wa ardhi na kuhifadhiwa katika faili namba 176936. lakini cha kushangaza wenye maeneo yao hawana taarifa kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa mchakato wote huu na hata kama serikali iliuza maeneo yao kwanini hawakulipwa fidia kama taratibu za kisheria zinavyotaka? Hapa inaonyesha kuna rushwa imetawala mchakato mzima na walioshiriki ni idara ya ardhi kuanzia ngazi ya wilaya mkoa hadi makao makuu.

  Kesi kama hizi Kisiwani mafia ni nyingi na pale wananchi wanapolalamika serikali inaonekana kusua sua kuchukua maamuzi ya dhati. Hii inaonyesha, wawekezaji kutumia jeuri ya pesa kuwanyamazisha viongozi na wenye rasilimali zao kuendelea kudhurumiwa na kukosa sehemu ya kupeleka malalamiko yao yakapatiwa ufumbuzi kwa ngazi ya wilaya.
   
Loading...