Ardhi anayogawa RC Makonda

Ardhi anayogawa RC Makonda

Sibonike

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Posts
17,297
Reaction score
18,053
Naomba ufafanuzi kwa wajuzi masuala ya ardhi hasa kuhusu sheria zake na umiliki.

Tumeshuhudia RC Makonda akigawa ardhi kwanza Kwa timu ya Yanga na baadaye kwa TFF.

Sidhani kama ni maeneo yake binafsi. Je? kuna ardhi chini ya mamlaka ya RC ambayo sheria inamruhusu kuigawa? Je? kuna sheria inamruhusu kugawa ardhi ya halmashauri au Jiji ndani ya mkoa anaongoza?
Isije baadaye ikaonekana zoezi zima lilikuwa kinyume cha sheria.
 
Huyu PM ni bonge la lodilofa. Anavyojitamba kugawa ardhi ya serikali utafikiri anagawa ardhi inayomilikiwa na mtu binafsi
 
Naomba ufafanuzi kwa wajuzi masuala ya ardhi hasa kuhusu sheria zake na umiliki.

Tumeshuhudia RC Makonda akigawa ardhi kwanza Kwa timu ya Yanga na baadaye kwa TFF.

Sidhani kama ni maeneo yake binafsi. Je? kuna ardhi chini ya mamlaka ya RC ambayo sheria inamruhusu kuigawa? Je? kuna sheria inamruhusu kugawa ardhi ya halmashauri au Jiji ndani ya mkoa anaongoza?
Isije baadaye ikaonekana zoezi zima lilikuwa kinyume cha sheria.
Hata ikiwa kinyume cha sheriab hivi nchi yetu ina sheria? Mtu akiwa ccm ndio sheria yenyewe.
 
Ukiona Rais Mstaafu anashangilia ujue kapatia. Kumbaka walikuwa wamekaa pamoja kwenye shughuli hiyo.
 
Alisema mtu yyte asifikiri ana cheo kikubwa kushinda yeye. Wawe na nidhamu maana Anawazidi vitu vingi Sana.
Baada ya Rais, anafuata yeye bila shaka. Mama Samia na Majaliwa si kitu kwake.
 
Ninavyofaham Mimi ardhi yote mmiriki ni Serkali ukiangalia hatimiliki inaukomo wa umiriki wake. Mwenye mamlaka ya ardhi ameanzia ngazi ya kijiji, wilaya, mkoa Na hadi taifa.

Kwenye ngazi ya kijiji mmiliki (sijajua kama ni mwenyekiti wa kijiji au nani)

Kwenye ngazi ya wilaya mmiliki ni mkuu wa wilaya. Anamamlaka ya kugawa ardhi ambayo bado haijapata mmiliki wa muda

Kwenye ngazi ya mkoa mmiliki ni mkuu wa mkoa

Kwenye ngazi ya taifa mmiliki ni raisi

Ndiyo maana unakuta baadhi ya wanaohitaji ardhi ukienda kijijini utaambiwa muone mwenyekiti wa kijiji nk

Isipokua kuna viwango vya umiliki ambao wanatakiwa kugawa kwa mtu, taasisi au kampuni. Kwa mwenyekiti haizidi hekari 5 na kwa mkuu wa wilaya nahisi 10 na mkuu wa mkoa 15 hii ni kwa pamoja. Yaani kama vile yanga kupewa hekari zilie hazizidi 15, TFF pia hazizidi 15 Haya ni majibu niliyopewa kipindi nafuatilia eneo husika kijijini
 
Asante kwa ufafanuzi huo.
 
Hata ikiwa kinyume cha sheriab hivi nchi yetu ina sheria? Mtu akiwa ccm ndio sheria yenyewe.
Kabisa--huu ni ukweli mchungu sana

Tena jana nimemsikia akiwaonya wale wanaopenda kuhoji hoji
 
Awagawie na simba, azam ili kuweka uwiano dar labda kama ni ardhi yake mwenyewe
 
Ardhi ni ya mkoa wa Dar es salaam, mkuu wa mkoa ndiye msimamizi. Hajauza ardhi ili jiji lipate pesa, ila anaamini kwa uwekezaji utakaofanyika,utaingiza kipato maradufu
 
Back
Top Bottom