Ningependa kwa kuanza kwa kumpongeza Muheshimiwa Makonda kwa jitihada zake na kutotaka kumkatisha tamaa. Ila kuna haja kidogo ya kushauriana ili kufanya jiji letu liwe safi na la mfano.
Ukiwasikiliza mameya wote pamoja na wakuu waliopita na wataalamu mbalimbali, tatizo kubwa la Dar es Salaam limegawanyika katika namna tatu kubwa – Mwamko wa wakazi, miundombinu na Vitendea Kazi. Kwa bahati mbaya tatizo la vitendea kazi (vifaa na miundo mbinu) linahusu manunuzi (budget). Na bila kutatua hilo hata ukifanikiwa hilo la mwamko bado utakwama mahali. Kama utafiti haujafanyika basi ufanywe kujua kila mtaa au kata inahitaji magari na vitendea kazi idadi gani kufanikisha hilo zoezi. Huo utafiti uweke bayana umbali, muda, gharama na kiasi cha fedha kinachohitajika. Hiyo itatatua kuliko kampeni za hapa na pale kwa kutumia wasanii na kulawapangia wafanyabiashara muda wa kufungua biashara. Hilo jambo litaleta mikanganyiko isiyoisha..
Hivyo basi we need to face reality by solving first the backbone problem.
- Yajengwe madampo kadhaa ya kisasa jijini. Ikiwezekana kila mwelekeo wa njia kuu za jiji, mfano Kibamba, Kigamboni, Tegeta, nk.
- Pili yanunuliwe au makampuni yapewe tenda ya kuzoa taka kwa kila wiki kupita mara 2 au 3 kila mtaa kuchukua taka.
- Tatu kila kaya itakiwe kisheria kuwa na special container la kutunzia taka zitakazosombwa na hayo magari. Sambamba na hilo kila kaya ilipie hizo gharama chini ya sheria (ordinance) maalumu za mitaa.
- Nne na muhimu sana, japokuwa suala la usafi ni la jiji na mkoa wenyeviti wa mitaa wawe wanawajibika moja kwa moja kwa hili. Na hakuna sababu in my view kuwapo na zawadi ya mtaa msafi. Kwa kufanya hivyo wanatimiza wajibu wao na si extracurricular activity. Kwani hata wanetu wakiwa wasafi hatuwapi zawadi bali wakiwa wachafu tunawapa adhabu!
Ukishaweka vema hiyo miundo mbinu na vitendea kazi, suala la kuhimiza watu wawe na mwamko litakuwa jepesi zaidi. Na wepesi wake unapokuja ni unawahimiza kama kukumbushana tu lakini sheria inakuwa tayari po wazi inayosema kila kitu juu ya nini kifanyike kama mtu anachafua jiji. Na kwa hili law enforcers duniani kote huwa ni jamii ya mtaa chini ya uongozi wa mtaa, jiji na hatimaye mkuu wa Mkoa.