Apple yaamrishwa kuifungua simu ya muuaji, yaigomea mahakama!

High Vampire

JF-Expert Member
Nov 17, 2012
2,915
2,131
Apple yaamrishwa kuifungua simu ya muuaji

Jaji mmoja katika jimbo la Carlifonia nchini Marekani ameiamrisha kampuni kubwa ya Teknolojia ya Apple kusaidia polisi katika kuchunguza simu ya mwanamume ambaye aliwapiga risasi watu 14 katika eneo la San Bernardino mwezi Disemba.

Syed Rizwan Farook na mkewe waliuawa na polisi baada ya kisa hicho.

Jaji alisema kuwa kampuni ya Apple ni lazima itoe msaada wa kiteknolojia baada kushindwa kuweka nywila ya simu hiyo kwa mara kumi. . Kampuni hiyo bado haijatoa tamka lolote na ina muda wa siku tano kupinga uamuzi huo.

Tangu kutolewa kwa programu mnamo mwezi Septemba 2014,data ya simu za Apple kama vile ujumbe na picha zimewekewa usalama wa kutosha.

Hii ina maanisha kwamba iwapo simu hiyo imefungwa ,ni nywila au neno la siri la simu hiyo linaloweza kuifungua na kupata data
1455710135379.jpg

Iwapo mtu atajaribu mara 10 bila mafanikio data iliopo ndani ya simu hiyo hujifuta .

Hakuna mtu ama hata kampuni ya Apple itaweza kupata ujumbe huo,hatua ambayo kampuni hiyo ilifanya kufuatia ufichuzi wa bwana Edward Snowden kwamba serikali ya Marekani imekuwa ikidukua simu za raia.

Apple wamekataa - Apple Resisting Magistrate Order to Share iPhone Information
 
FBI wanataka Apple watengeneze OS ingine ili watumie kuingilia hio simu ili kupata Data lakini sidhani kama Apple wako tayari kwa hili, kwa sababu hio inamaanisha Apple kurudi tena kwenye drawing board kutengeneza simu zingine mpya.

Kwa kufanya hivyo hio itakuwa ni gharama ingine.
 
na siku tu wakiruhusu hii kitu ya kudukua information za mteja ndio mwisho wa kufa apple na kulinganisha na ghalama zao wanavyouza
 
na siku tu wakiruhusu hii kitu ya kudukua information za mteja ndio mwisho wa kufa apple na kulinganisha na ghalama zao wanavyouza

Kabisa,

Kama unafuatilia haya mambo kuna wakati Blackberry nao waliambiwa mambo kama haya na nafikiri kwa wakati ule ilikuwa sawa kwao kufuata masharti ya kufuta hio encryption.

Encryption ni muhimu sana kwa sasa kwa sababu kwa kuzingatia umuhimu wa simu ya mkononi hasa smart phones kama iPhone.

Kwa sababu wakifanya hivyo kuruhusu kutengenezwa hio OS mpya basi kuna watu wamekaa pembeni wanasubiri loophole mahali na wakipata mpenyo basi simu za Apple zinakuwa si mali tena.

Tunakoelekea simu itakuwa na uwezo wa kuwasha hata gari na mambo mengine ya juu zaidi kiteknolojia, kwa maana kwa sasa hivio simu inatumika hata katika mifumo ya kibenki na mengine.

Hivyo suala la usalama wa simu kwa makampuni kama Apple inachukulia very serious.
 
unataka kulinganisha na tecno
apple hawana matangazo na budget yao ya matangazo ndogo mno kulinganisha na makampuni kama sumsung
Sijalinganisha kitu chichote.

Hapo ni promo tu kwamba hiyo simu ina security, sema tu jinsi ya kutangaza ndio hiyo fix yao na mahakama

Usishangae baada ya hiyo habari mauzo ya simu zao yakapanda.
 
Sijalinganisha kitu chichote.

Hapo ni promo tu kwamba hiyo simu ina security, sema tu jinsi ya kutangaza ndio hiyo fix yao na mahakama

Usishangae baada ya hiyo habari mauzo ya simu zao yakapanda.
tokea ujue neno promo kila kitu promo wateja wa apple wanajua simu zao za iphone huwa security na sidhani kama kama kuna mahali ushawahi kukutana na tangazo la kishamba kama hisia zako juu ya apple product kizuri kinajiuza acha mambo ya kukalili kila kitu kick we unaweza linganisha hii bidhaa na ipi mpaka waanze kutafuta kick hawa jamaa wamejipanga na soko awajaliteka kwa maneno wameliteka kwa vitendo hebu cheki kidogo apple event mwaka jana kwa ubora huo matangazo ya nini bidhaa inajiuza yenyewe
 
Kwanza sijakujibu wewe

Pili inaonekana hauko tayar kujadiliana kistaarabu, basi tuishie hapo kwa mimi na wewe...
 
Back
Top Bottom