Apple wazima kelele za wapinzani na ios 8.0.2

Apple wazima kelele za wapinzani na ios 8.0.2

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159
[h=1]APPLE WAZIMA KELELE ZA WAPINZANI NA IOS 8.0.2[/h]
  • user.png
    Mwandishi Wetu


Apple wametimiza ahadi ya kutokulala mpaka kieleweke kuhusu iOS. Siku ya leo wametoa iOS 8.0.2 ambayo itasuluhisha matatizo kadhaa baada ya jaribio la kurekebisha tatizo hilo kufeli vibaya mno walipotoa iOS 8.0.1 kwa kuongeza “bugs’, bugs ambao hupelekea simu kupoteza mtandao na pia kisoma alama za vidole kwenye kifungo cha mwanzo (home button) kutofanya kazi kabisa.


iOS 8.0.2 inaonekana kuwa “tweak” ndogo tu kwani faili hilo lina ukubwa wa 64.1 mb kwenye iPad Mini, 64.7 mb kwenye iPhone 5 na 72.2 mb kwenye iPhone 6 Plus. Hivyo huchukua muda mfupi kupakua na ku-install bali pia. Apple wametangaza kuwa simu na tablet ambazo zimewekewa iOS 8.0.1 zitatengenea mara tu zitakapowekea toleo hili la 8.0.2


Mafanikio ya kuboresha iOS yataleta faraja kubwa kwa Apple hasa baada ya wadau mbali mbali kuanza kupinga suala la kupinda kwa iPhone 6 Plus baada ya kukaliwa, wadau wa BBC Technology pamoja na kuikalia mara kadhaa pia wamefanya zoezi la kuiweka mfuko wa nyuma iPhone 6 Plus siku nzima. Simu hiyo imetumika katika shughuli za kawaida za kikazi na kimaisha na kutoa taarifa kwamba iPhone 6 Plus haikupinda wala kuathirika chochote.


Pia wadau wa Mac Romours nao wamefanya zoezi kama hilo bila ya iPhone kupinda. Pia Mac Romours pamoja na kukiri kwamba utakapoikalia kwa nguvu upo uwezekano wa kupinda kwa simu pia wameainisha kuwa fableti mbali mbali zinazopinda baada ya kukaliwa.


Kampuni mbali mbali za upinzani ikiwemo Nokia, LG na Samsung wamekuwa wakimimina mfululizo wa twitter na kuishikia bango kashfa ya kupinda kwa iPhone 6 Plus huku LG wakiongoza kutumia hashtag ya bendgate (#Bendgate).


Usiku wa leo tutaifanyia majaribio kadhaa app ya Health iliyokusudiwa kurekebisha na kuripoti hali yake, pamoja na kujaribu kuchunguza iwapo toleo hilo lina matatizo yoyote mengine mapya. Usiache kutembelea Gajetek kwa makala hiyo itayafuata hivi karibu itakayozungumzia suala hilo.


Chanzo: gajetek habari
 
Moja ya tatizo ambalo hata mimi nilipata kwenye ipad yangu ni baada tu ya ku install ios 8.0.1 ni kwamba niliona ina stuck sana
 
Asante kwa taarifa
muhimu,Iphone fun forever,kwa raha zangu na iphone5s & iPhone 6+ with updated iOS 8.0.2 😄😄
 
Na mimi nimesha update nakula life na ios 8.0.2 kweli mteja ni mfalme
 
Nami nime update ndiyo inaload sasa.
 
ok. nadhani iphone 6s+ itakua better zaidi na hiyo alminium mtaireplace na.polycarbonate 2gb ram na 13mp camera.

mwandishi wa makala inaelekea ni ifanboy eehh. kupinda #bendgate kwa 6+ ni kweli na video kibao youtube zimeonesha.
:focus: apple inc wameonesha kuwathmini wateja wo kw ku apologize na kulitatua tatizo mapema.

lakini kwnn ios tu? mwaka jana ios 7 nayo ilileta shida shida hizi hizi siku za mwnzo. mbona jelybean au kitkat hazisumbui sana?

hafu apple fans nao siku ya kwanza tu kila mtu kutaka ku upgrade os. duuuh hawanaga subira kabisa.
 
Lakini cha ajabu hii ios 8.0.1 na 8.0.2 vimeondoa personal hotspot kwenye ipad air yangu. Msaada tafadhali jinsi gani nitairudisha
 
Lakini cha ajabu hii ios 8.0.1 na 8.0.2 vimeondoa personal hotspot kwenye ipad air yangu. Msaada tafadhali jinsi gani nitairudisha
Jaribu ku-install tena, tumia iTunes badala ya ku-install OTA.
 
Moja ya tatizo ambalo hata mimi nilipata kwenye ipad yangu ni baada tu ya ku install ios 8.0.1 ni kwamba niliona ina stuck sana
iOS 8.0.1 ilikuwa na glitch na bugs, utakapo update 8.0.2 matatizo yataondoka
 
Back
Top Bottom