Wilhelm Johnny
JF-Expert Member
- Jan 13, 2016
- 1,368
- 1,325
Nimesoma BBC kwamba simu za apple na Samsung soko lao limeshuka ukilinganisha na macompany ya Uchina.
CHANZO: BBC
Mauzo ya simu za Samsung yashukaKampuni ya vifaa vya kielektroniki, Samsung imeathiriwa na kushuka kwa mauzo ya simu zake za aina ya Smartphone.
Mazingira mabaya ya kibiashara na viwango vya chini vya vifaa vya kiteknolojia vilisababisha kushuka kwa faida katika robo ya nne ya mwaka jana kwa asilimia 40 hadi dola bilioni 2.7.
Kampuni hiyo ya Korea Kusini imeonya kwamba itakuwa vigumu kudhibiti faida mwaka huu kama ilivyokuwa mwaka 2015.
Mapato ya mwaka 2015 yalishuka hadi dola bilioni 165 ikilinganishwa na miezi 12 iliopita.
Ushindani mkali kutoka kwa kampuni za Uchina zinazotengeza vifaa rahisi vya kiteknolojia kama vile Xaiomi na Huwawei katika soko hilo pamoja na kampuni ya Apple zimeathiri mauzo ya simu za Smartphone.
Simu ya Galaxy S6, ambayo ndio simu ya hadhi ya juu iliozinduliwa mnamo mwezi Aprili, ilishindwa kuwafurahisha wateja na kampuni hiyo imeshindwa kudhibiti soko lake.
Jake Saunders, mkurugenzi wa Asia-Pacific katika kampuni ya utafiti ya ABI Research ameiambia BBC: ''Inaonyesha kwamba wako chini ya shinikizo kwa sababu nusu ya mapato yao yanatoka katika simu za rununu''.
Xiaomi inapata wateja katika soko la India na Indonesia, ambalo ni kubwa kwa simu za smartphone na ndio eneo ambalo linakuwa kwa haraka.
CHANZO: BBC
Mauzo ya iPhone yapungua dunianiKampuni kubwa ya teknolojia ya Apple imeripoti kupungua kwa mauzo ya simu za iPhone katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho mwaka uliopita.
Kampuni hiyo iliuza simu milioni 75 mwaka uliopita ikiwa ni mauzo ya chini zaidi tangu mwaka 2007.
Hii ni kutokana na kuyumba kwa uchumi wa China.
Hata hivyo faida ya kampuni ya Apple iliongezeka katika kipindi hicho kwa zaidi ya dola bilioni 18.
Mhariri wa masuala ya Teknolojia katika mtandao wa CNET Ian Sherr, amesema huenda soko la simu za mkononi limefurika.
CHANZO: BBC