Ni wazo zuri kwamba tuombe Apple Retail Store Tanzania, lakini kwa ufahamu wangu mdogo sidhani kama hili litawezekana. Apple wanafungua Retail stores katika miji ambayo kuna wanunuzi wengi wa bidhaa zao, katika maduka yao zaidi ya 300 Duniani kwa sasa hakuna hata moja ambalo limefunguliwa kwa sababu tu waliomba, bali Apple wenyewe wameweza kuona opportunity na economic benefits (not necessarily profit) za kufungua duka sehemu husika.
Ukiangalia Financial statement za Apple, nyingi kati ya Retail stores hizi zinaendeshwa kwa hasara, Apple wanazitumia kama njia ya ku-promote bidhaa zao mbali na kuuza, pia kutoa customer service. Kwa mfano kuthibitisha hili Apple wanaendesha semina za bure kila wiki katika maduka yote haya kuwaelimisha wateja juu ya namna ya kutumia hardware (Mfano iPhone, Ipad) na software mfano iWeb.
Je ni wangapi kati ya Watanzania wakaazi wako tayari kununua iMac, iPad Apple TV na Macbook Pro? Nadhani ukiangalia uhalisi wa maisha ya Watanzania walio wengi utapata jibu kwamba Apple hawatafungua duka hili kwa sasa. Hao wenye iPhone tu, Apps zinauzwa Dollar 1 na wao wanachakachua badala ya kununua. Apple wanatrack watumiaji na wanunuzi wa vifaa vyao na wao wanajua kila penye soko. Huko UAE kuna duka moja tu, ikiwa Abu Dhabi hakuna Apple Store je Dar?