Apigwa risasi na kuuawa na majambazi Mbezi

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Jana usiku yametokea mauwaji ya mtu mmoja mwanaume kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi katika Bar ya Kadabla iliyopo katikati ya Mbezi kwa Msuguli na Kibanda cha Mkaa.Mauwaji hayo yametokea kati ya majira ya saa tano usiku hadi saa saba usiku

Mashuhuda wa tukio katika eneo hilo wanasema marehemu alifika katika Bar hiyo ambayo amezoea kufika mara kwa mara anapokuwa anatoka kwenye mihangaiko yake maeneo ya K'koo,usiku wa jana alifika akiwa peke yake na kuegesha gari kisha kuanza kupoza koo.

Baada ya muda kupita,alimpigia mkewe ambaye wanaishi nae maeneo ya Mbezi Mwisho eneo la Tanesco njia ya kwenda Malamba Mawili,wito huo kwa mkewe ilikuwa kwa ajili ya kukaa wote ili waagize "kitimoto" na kuburudika pamoja.Katika ya burudani ya moja moto na mbili baridi huku kitimoto ikiwa inakaangwa jikoni kwa Mangi,walikuja watu wasiopungua wawili na kuanza kugongagonga gari lake,ilibidi aamke ili kujua kulikoni watu hao kugonga gari lake?

Baada ya maulizo hayo,wale jamaa wakamwambia wao wanataka pesa,wanajuwa ana pesa ndani ya gari,hivyo wanazitaka.Yakatokea mabishano na baadae jamaa wakampiga risasi mbele ya mke wake na kuchukua maisha yake huku wakitokomea na kiasi cha pesa kilichokuwepo.Kulizuka taharuki na watu kuacha vinywaji vyao na chakula juu ya meza na kutawanyika,hata waliokuwa "tungi" waliweza kukimbia bila kuyumba.

Msiba uko nyumbani kwa marehemu maeneo ya Mbezi Mwisho(Tanesco Maghorofani) njia ya kwenda Malamba Mawili.Bwana alitoa na bwana ametwaa,Jina lake lihimidiwe.

Polisi iamke na kutazama matukio haya ya uhalifu maana watu wanauwa wazi wazi na silaha za moto zimeenea hovyo hovyo.
 
Sijui haya mauaji ya kikatili kila uchao tuilaumu serikali kwa kutokutulinda au tukubaliane na tatizo kubwa zaidi kwamba idadi ya watanzania makatili inaongezeka kwa kasi!
Wakati Marehemu Luck Dube alivyoimba 'Crazy world', few knew that time was near for Tanzanian also to be dying like flies everyday! RIP
 
Linapokuja suala linalohusiana na roho kuacha mwili mwanadamu anakuwa na ujasiri wa ajabu sana.....anaweza kufanya tukio ambalo wengi hawakulitazamia.....

Kuna nyumba moja kule mtaani palikuwa na mgonjwa ambaye ana miaka zaidi ya miwili anaumwa....siku nyumba iliposhika moto walishangaa mgonjwa naye anasaidia kuokoa vyombo tena kwa speed ya hatari sana.....ni tukio lililonifanya nikiheshimu sana kifo mpaka leo.....

Pole zangu ziwaendee wale waliofikwa au kuguswa na msiba huo kwa namna moja au nyingine.....na muumba awape moyo wa uvumilivu katika wakati huu mgumu.....

Sisi ni wa Mungu na kwake tutarejea.....
 
Sijui haya mauaji ya kikatili kila uchao tuilaumu serikali kwa kutokutulinda au tukubaliane na tatizo kubwa zaidi kwamba idadi ya watanzania makatili inaongezeka kwa kasi!
Wakati Marehemu Luck Dube alivyoimba 'Crazy world', few knew that time was near for Tanzanian also to be dying like flies everyday! RIP

We are living in CRAZY WORLD.....

People dies like flies everyday
You read about it in the news but you dont believe it...until that man in a long black coat come and knock your door....because you are his next victim........

CRAZY WORLD.......
 
Huyo jamaa alikua kubeba fedha za deal, otherwise asinge kua mpuuzi kutembea na pesa nyingi Bar.
 
Lile agizo la Makonda lipo wapi?au ndo wanazimalizia za mwisho mwisho?so sad,R.I.P Raia mwema
 
Jana usiku yametokea mauwaji ya mtu mmoja mwanaume kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi katika Bar ya Kadabla iliyopo katikati ya Mbezi kwa Msuguli na Kibanda cha Mkaa.Mauwaji hayo yametokea kati ya majira ya saa tano usiku hadi saa saba usiku

Mashuhuda wa tukio katika eneo hilo wanasema marehemu alifika katika Bar hiyo ambayo amezoea kufika mara kwa mara anapokuwa anatoka kwenye mihangaiko yake maeneo ya K'koo,usiku wa jana alifika akiwa peke yake na kuegesha gari kisha kuanza kupoza koo.

Baada ya muda kupita,alimpigia mkewe ambaye wanaishi nae maeneo ya Mbezi Mwisho eneo la Tanesco njia ya kwenda Malamba Mawili,wito huo kwa mkewe ilikuwa kwa ajili ya kukaa wote ili waagize "kitimoto" na kuburudika pamoja.Katika ya burudani ya moja moto na mbili baridi huku kitimoto ikiwa inakaangwa jikoni kwa Mangi,walikuja watu wasiopungua wawili na kuanza kugongagonga gari lake,ilibidi aamke ili kujua kulikoni watu hao kugonga gari lake?

Baada ya maulizo hayo,wale jamaa wakamwambia wao wanataka pesa,wanajuwa ana pesa ndani ya gari,hivyo wanazitaka.Yakatokea mabishano na baadae jamaa wakampiga risasi mbele ya mke wake na kuchukua maisha yake huku wakitokomea na kiasi cha pesa kilichokuwepo.Kulizuka taharuki na watu kuacha vinywaji vyao na chakula juu ya meza na kutawanyika,hata waliokuwa "tungi" waliweza kukimbia bila kuyumba.

Msiba uko nyumbani kwa marehemu maeneo ya Mbezi Mwisho(Tanesco Maghorofani) njia ya kwenda Malamba Mawili.Bwana alitoa na bwana ametwaa,Jina lake lihimidiwe.

Polisi iamke na kutazama matukio haya ya uhalifu maana watu wanauwa wazi wazi na silaha za moto zimeenea hovyo hovyo.
Siku nyingine unaporipoti taarifa za majonzi punguza vichekesho mkuu, eti hata waliokua tungi walifanikiwa kukimbia bila kuyumbayumba!!!!
 
We are living in CRAZY WORLD.....
People dies like flies everyday
You read about it in the but you dont believe until that man in a long black coat come and your door....cause you are his next victim....
CRAZY WORLD.......
Mkuu KikulachoChako umeiongezea nguvu post hii.
Sio ajabu huyu marehemu alikuwa amesoma habari za Dada yetu wa Kibada aliyelazimishwa kuacha mtoto wa miaka minne, but surely, little he did know that was the next victim!
Ninayeandika hapa na wewe unayesoma hiyo ndio hali halisi, kwa hali ilivyozidi kuwa mbaya kesho wanaweza kunipost mimi hapa au tukakuposti wewe. Kielelezo kwamba kama Watanzania tumekuwa tunajidanganya kwa miaka mingi na umoja bandia basi huu ndio muda wa kuungana na kuwa na umoja wa kweli ili kuweka mambo sawa.
 
We are living in CRAZY WORLD.....

People dies like flies everyday
You read about it in the but you dont believe until that man in a long black coat come and your door....cause you are his next victim....

CRAZY WORLD.......
daah so sad, rip man
 
Apo bar hapana hata walinzi wa iyo bar? Wakati yanatkea mabishano walikua wapi? Inaonesha ao majambazi walikua wanamfuatilia vizuri nyendo zake
 
We are living in CRAZY WORLD.....

CRAZY WORLD.......

"Crazy World"

So far so good we still living today
But we don't know what tomorrow brings
In this crazy world
People dying like flies every day
You read about it in the news
But you don't believe it
You'll only know about it
When the man in the long black coat
Knocks on your door
'Cause you're his next victim
As you are living in this

[Chorus:]
Living in, living in this crazy world [x4]

Leaders starting wars every time they want
Some for their rights,
Some for fun and their own glory letting people die for the wrong that they do
Oh it's painful come on now little boy
Say your prayers before you sleep
Little boy went down on his knees
And he said:
"Oh Lord Now I lay me down to sleep
I pray the Lord my soul to keep
And if I die before I wake
I pray the Lord my soul to take."

'Cause he's living in this crazy world
Oh Lord
 
Wenye baa wapewe namba ya POLISI DHARURA!!!
Bar zifunge camera nje ya bar!!!,au pawe na mlinzi kwa nje,maana Baa nyingi ulinzi unaanza baada ya baa kufungwa!!!
 
Hivi lile zoezi la ukaguzi na uhakiki wa umiliki wa silaha liliishia wapi? Au tulipoonyeshwa picha za mkubwa ndio ikawa tamati? Hali inazidi kutisha, usalama uko mashakani sana.
 
Jana usiku yametokea mauwaji ya mtu mmoja mwanaume kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi katika Bar ya Kadabla iliyopo katikati ya Mbezi kwa Msuguli na Kibanda cha Mkaa.Mauwaji hayo yametokea kati ya majira ya saa tano usiku hadi saa saba usiku

Mashuhuda wa tukio katika eneo hilo wanasema marehemu alifika katika Bar hiyo ambayo amezoea kufika mara kwa mara anapokuwa anatoka kwenye mihangaiko yake maeneo ya K'koo,usiku wa jana alifika akiwa peke yake na kuegesha gari kisha kuanza kupoza koo.

Baada ya muda kupita,alimpigia mkewe ambaye wanaishi nae maeneo ya Mbezi Mwisho eneo la Tanesco njia ya kwenda Malamba Mawili,wito huo kwa mkewe ilikuwa kwa ajili ya kukaa wote ili waagize "kitimoto" na kuburudika pamoja.Katika ya burudani ya moja moto na mbili baridi huku kitimoto ikiwa inakaangwa jikoni kwa Mangi,walikuja watu wasiopungua wawili na kuanza kugongagonga gari lake,ilibidi aamke ili kujua kulikoni watu hao kugonga gari lake?

Baada ya maulizo hayo,wale jamaa wakamwambia wao wanataka pesa,wanajuwa ana pesa ndani ya gari,hivyo wanazitaka.Yakatokea mabishano na baadae jamaa wakampiga risasi mbele ya mke wake na kuchukua maisha yake huku wakitokomea na kiasi cha pesa kilichokuwepo.Kulizuka taharuki na watu kuacha vinywaji vyao na chakula juu ya meza na kutawanyika,hata waliokuwa "tungi" waliweza kukimbia bila kuyumba.

Msiba uko nyumbani kwa marehemu maeneo ya Mbezi Mwisho(Tanesco Maghorofani) njia ya kwenda Malamba Mawili.Bwana alitoa na bwana ametwaa,Jina lake lihimidiwe.

Polisi iamke na kutazama matukio haya ya uhalifu maana watu wanauwa wazi wazi na silaha za moto zimeenea hovyo hovyo.

Duh, pole wafiwa...poleni sana....ila sentensi ya mwisho ina utata kidogo...ni kweli polisi jukumu lao mojawapo ni kulinda usalama wa wananchi, lakini polisi hawawezi kuwa kila mahali...wananchi wenyewe ni vema tuwe walinzi...majambazi yanafahamika tunaishi nayo katika jamii yetu, ila hatutaki kuyataja...halafu nyumba za wageni nazo zinatunza na kuficha majambazi...nyumba za wageni ziangaliwe upya, na hasa namna 'wageni' wanavyopokelewa...uwepo utaratibu wa kuonyesha vitambulisho au namna yoyote ya kumfahamu aliyechukua chumba ni nani na ni mtu wa aina gani....
 
Back
Top Bottom