Apartments threaten hotels in Dar, Nairobi










Mkuu si waarabu tu, na wazalendo wengi tu wapo katika hii biashara.
Hii nyumba ipo Mbezi Beach, Jogoo area..
Nyumba inaenda $600 p.m. fully furnished
 
hivi hizi apartment zinatoa huduma kama za mahotelini?
mfano kubadilishiwa mashuka, kusafishiwa chumba, bafu, choo nk kila siku?
aidha idadi ya hoteli zenye gym na bwawa la kuogelea zinaongezeka. kama hizo
apartments hazitoi hizo huduma bora nibanane hoteli.

binafsi nisingependa kufunga safari ya likizo mahali kisha mimi na madam
tunaendelea na mikikimikiki ya nyumbani mfanokuonsha vyombo,
kufua, kupika, kusafisha nyumba nk kama vile bado tuko home.
kwangu mimi hiyo siyo likizo ya kuilipia pesa nyingi. vinginevyo ni bora
nichukue "likizo" niende kijijini ambako nitajumuika na familia/ukoo.

ni mtazamo tu.
 

...hakuna huduma tajwa hapo juu, endelea kula raha za hotelini bro.

Apartments nyingi zenye hadhi ya Bronze, Silver au Gold "serviced apartments" unakuta kitchenette & na vyombo vyake, hoover, iron table na pasi yake, washing machine, na dishwashing machine kwenye apartment yako mwenyewe uzitumie.

 
Mkuu si waarabu tu, na wazalendo wengi tu wapo katika hii biashara.
Hii nyumba ipo Mbezi Beach, Jogoo area..
Nyumba inaenda $600 p.m. fully furnished

...mkuu, zinaonekana nzuri sana.

Vipi securitywise? unasema zipo Msasani...more info i.e Contacts au kama wana websites? Wengine tunapata wageni wa mara kwa mara wanaopendelea sehemu kama hizi.
 

kama mambo yenyewe ni hayo acha niendelee kula raha za hoteli lol
 
Ninaweza kupata link zingine za wamiliki wa apartments hapo Tanzania?
 
...mkuu, zinaonekana nzuri sana.

Vipi securitywise? unasema zipo Msasani...more info i.e Contacts au kama wana websites? Wengine tunapata wageni wa mara kwa mara wanaopendelea sehemu kama hizi.

Swali lako ni muhimu sana Mkuu, kama kuna ulinzi wa kutosha basi sehemu kama hizi ni poa sana ukilinganisha na Hotel.
 
Mkuu Lole,

Hebu tuwekee picha za ndani yaani tupe maelezo kamili ya hizo nyumba........sema pia kuhusu security na mambo kama hayo..........
 
Mkuu Lole,

Hebu tuwekee picha za ndani yaani tupe maelezo kamili ya hizo nyumba........sema pia kuhusu security na mambo kama hayo..........

Wakuu Ogah na Mbu hizi apartmetns ziko Mbezi Jogoo, floor ni timber na granite kitchen tops .Samahani siku weza kujibu in time maana nilikuwa kwa majukumu mikoani.Lakini ukitaka details pls ni PM
 
Wakuu wangu najuwa hii ni old thread ila nimeamua kuifufua naombeni wote mrudi tafadhali, naombeni wekeni apartments nzuri na bei rahisi kwa sasa hivi kwa hapaa dar na ulinzi upo wa kutosha au vipi??Najuwa now imepita mda mrefu sana, wengine huwa wa kusafiri kuja hata 2 months na kuondoka so bora zaid tukijua apartments za bei rahisi ambazo zipo furnished na ulinzi wa kutosha.
Ogah Lole Gwakisa BAK Mbu
 
Last edited by a moderator:

....Dahhh, nahisi kwa sasa zimejaa Dar, pesa yako tu...Anzia hapa,
PropertyFinder.co.tz - Tanzania houses for rent | Property and accommodation classifieds | Listings from LICENSED real estate agents (zamani TZadverts.com) - Find Property - APARTMENTS FOR RENT

hebu mwenye habari kuhusu zile Apartments za Mlimani City amsaidie Papizo...
ila asikudanganye mtu eti ubane matumizi ukafikie LAMADA APARTMENTS,..!
 
Last edited by a moderator:


Nashukuru sana ndugu yangu na nimepitia hiyo site naona zipo nyingi na za aina tofauti tofauti nzuri sana tu, itabidi sasa nikipata mda nizipitie zote niziangalie vizuri, hivi mkuu Mbu zile za Mlimani City na zenyewe kumbe za mda mfupi??

Nitafurahi n kushukuru kila mtu anayejua akaweka list tofauti ya apartments najuwa wengi watafaidika pia, asante sana mkuu wangu Mbu

Unajuwa sio mda mrefu kuna mtu ametoka kuniambia eti bora Lamada sasa mkuu naona umeitaja Lamada hapo hebu nipe habari papoje hiyo sehemu??
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nikiangalia ujumbe halafu nikichanganya na avatar nimecheka sana. Umetishaaaaaaa
 

Umetumwa?
 

Nina wasiwasi na hapo kwenye Blue, unazungumzia hoteli za nyota ngapi? Kumbuka kuna TAG inaitwa DND yaani DO NOT DISTURB hiyo tag ukiweka mlangoni kwa hoteli ya hadhi ya nyota tano huwezi kusumbuliwa mpaka pale yatakapopita masaa nane kuanzia asubuhi ndipo atakapopigiwa simu kuulizwa kama anahitaji huduma ya kusafishiwa chumba au la na si kugongewa tu kiholela.
Nadhani apartment zitakuwa ni tishio kwa hoteli za hadhi ya nyota 2 na 3 lakini si kwa hadhi ya nyota 4 na 5.
 

Umenena mkuu, wachina hawa waliochoka ni wachafu na wakitoka sehem imechakaa na kunuka kama jalala!
 

.....hivi kuna hoteli ya nyota tano Dar-es Salaam au Zanzibar?
najua mawazoni mnaweza kuja na majina ya Hyatt-Kilimanjaro, au Melia Zanzibar....
 

....Jamaa/management ya Lamada hawapo serious kabisa na Accomodation aisee,...
wao wanachojali ni kukodisha ukumbi na viwanja vile kwa mashughuli!

ndio kusema shida utayokumbana nayo ni kelele za muziki (kuna wakati unakuta functions hata nne around, utadhani mpo Fete au saba saba vile!), shida ya parking, nk....

Mbaya kuliko yote, Mende, uchakavu wa milango, makabati, masinki na vyoo ....pia ni tatizo lililofumbiwa macho na utawala.
Wasanii wa Bongo Movie bado wanaweka kambi pale, na kuna wakati ma miss Tanzania na hata team ya Simba walikuwa wanaweka kambi pale...you can Imagine 'nje ya boksi'...

Niliwahi kukodi apartment pale 2009, ....nikaja gundua kuna baadhi ya vitu vyangu vimebiwa. Malalamiko yangu yaligonga mwamba kwani Uongozi walinionyesha bango "Utawala hauhusiki na Upotevu wa Mali Vyumbani"....ndio kusema unapotoka, chukua begi lako la nguo na kila kitu chako, maana vitu vya thamani sio lazima iwe (mfano) Camera, Perfumes, na Laptop pekee...
 

Habri mkuu, kwanza kabisaaa nashukuru sana kwa kuweza kufunguka zaidi maana nilikuwa bado sijajua hasaa tatizo la hapo sasa hizo si itakuwa karaha tu mtu unaenda mhali inabidi upumzike aisee na kuwa free, na sio kelele tena, na upande wa mali vyumbani ina maana na wenyewe wanakuwa na funguo wako wa chummbani??Kama yes why wahusika wanasema kwamba wenyewe hawahusiki na upotevu wa mali zako chumbani??Kama ni hivyo basi wasiingie chumbani kama vipi simple and clear,

Hapo moja kwa moja nimeona hapafai nadhani usalama wa vitu ni muhimu sana tena sanaaa kulikoo kitu kingine maana mtu unaweza kuondoka then ukawaza kuna mizigo umeacha unaweza kuibiwaa na usafi vile vile wa muhimu sana

Nashukuru mkuu wangu kwa kunifungua aisee nitaangalia sehemu zingine tu hapo hapafai kumbe,wenyewe wanaangalia tu kutengeneza hela ina maana na sisi tunaolipia upande wa apartments tunakuuwa tunakaa bure au??

Mkuu kwa maelezo yako tu nashukuru sana umenifungua kuliko ningeenda kichwa kichwa asante saa na siendi tena hapo
 
Reactions: Mbu
Hata ukiweka DO NOT DISTURB tag haisaidii sana manake hizo movemnts na commotions zinazoendelea along the hall way ni kero tupu na utaamka tu.
Nimelala sana 4 and 5 star hotels nyingi kila kona ya dunia hii na bado ni kero tu unless upate suite. South America katika nchi kama za Costa Rica, Panama au Colombia angalau cleaners wanaanza kuja late around noon. Ila US ni worse, sababu 7 am utawasikia kwenye hall way
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…