Hii kitalamu wanaita gynaecomastia ni mojawapo ya effect ya dawa nyingi tu sio ARVs pekee. Ni kweli haipendezi kuona mwanaume ktk hali kama hiyo, lkini sioni sababu ya kuilaumu TFDA. Hii ni side effect inayotokea kwa nadra sana, na ndio maaana walipolinganisha faida na hasara ya dawa hii wakaridhia itumike.
Lakini hata hivyo, hebu tuwe wakweli jamani. Kipi bora kwako, kumpoteza mpendwa wako au kuendelea kuishi naye akiwa ktk hali hii ambayo sababu yake inajulikana.