Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,072
- 79,444
ANZIA CHINI LAKINI KABIA JUU!
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Humble beginnings! Anza kidogokidogo! Hapohapo ulipo na ulichonacho. Tumia ulivyonavyo kupata vile unavyovitaka ambavyo hauna.
Moja ya ishara za awali kuwa Jambo unalofikiri unaenda kushindwa ni kutaka uanze ukiwa juu. Utafeli pakubwa.
Sijui niongee kisaikolojia au kifalsafa. Au niongee lugha ya kawaida ya mtaani ili uweze kunielewa.
Unapopanga mipango usionyeshe dalili wala ishara. Chini kwa chini. Kisha anzia hukohuko chini. Kisha boom! Unalipuka baada ya kupata nguvu.
Kijiografia wind blows from high pressure to low pressure. Jambo Hilo kifalsafa linaweza kuwa na hekima nyingi. Lakini kwa kijana mdogo kama wewe Jambo hili linakuambia kuwa siku zote kama unataka kufanya movements yaani mijongeo, kupiga hatua hasa ukiwa katika hatua za chini kabisa itakupasa uuige upepo au utazame mambo ya kijiografia.
Anzia chini. Tembea chini! Mahali ulipo kwenda chini.
From High to low! Kisha baadaye ukishakua na nguvu unabadili muelekeo. From Low to High.
Kijiografia pia, River flows to lowland from highland. Yaani mto hutiririka kutoka kwenye miinuko au milima au uwanda wa juu kwenda mabondeni au kwenye tambarare.
Falsafa hii ya maji na upepo zinafanana kwa kiwango Fulani.
Kwenye biyolojia hasa kwenye mambo ya reproduction, kanuni ni ileile. Haizai au Kuota bila kuoza. Haiponi bila kuharibika na kuoza Kwanza.
Code na pattern hizo zipo pia kwenye mfumo wako wa maisha.
Huwezi kuanzia juu kwani lazima utaanguka tuu. Hapo ulipo lazima uanzie Kwanza chini ndipo uende juu ukishapata nguvu.
Usione aibu kuanzia chini. Kwa sababu huko ndipo ilipohatua zako za kwenda juu.
Mfano, unataka kuwa mfanyabiashara Mkubwa wa nguo. Lakini huna mtaji mkubwa. Huwezi niambia huna mtaji kabisa.
Anza biashara ya nguo za elfu 20, tembeza. Utapata wapi elfu 20? Fanya vibarua, nenda kuwa saidia fundi, Fanya udalali, Fanya uwinga.
Masuala ya kusema unaona aibu kuwa winga au dalali au kusaidia fundi au kufanya kazi anayoweza kufanya mtu yeyote ni dalili kuwa hata KAZI unayoitamani hutoiweza.
Mambo ya kusema unaelimu au mwonekano mzuri na kufanya baadhi ya kazi ni kujidhalilisha achana nayo.
Hakunaga kujidhalilisha kwenye KAZI halali. Hakuna anayekutazama na kukujali. Hasa ukiwa na mawazo ya kijinga kama hayo.
Anzia chini lakini kamwe usiache kukabia juu. Sio unaanzia chini lakini unafanya shughuli zako ilimradi. Kabia juu. Kuwa na focus, mipango, mikakati na malengo.
Sikiliza, pressure inapozidi ndipo upepo unavyozidi kuwa na nguvu kuvuma. Halikadhali, pressure kwenye maji mtoni inapozidi ndivyo maji yanavyozidi kuflow kwa nguvu na Kasi.
Kwenye maisha yako. Hakikisha kadiri pressure za maisha, changamoto za maisha zinavyoongezeka kwako hakikisha zinakupa nguvu ya kuzidi kuflow kama maji na kublow kama upepo. Move! Jongea!
Sio unachekwa kidogo unaacha!
Sio unataniwa kidogo unaacha!
Sio unaambiwa huwezi au hautafika popote nawe unaingia hofu na kukataa tamaa unaacha!
Tumia hizo changamoto kama pressure ya kukusukuma(motivate) kusonga mbele!
Kuna wakati Taikon Master nilipokuwa naanza kuandikaandika mtandaoni kuna watu walikuwa wakisema maneno kama hayo! Oooh! Hujui chochote, unaandika utumbo! Unaandika mavimavi!
Lakini Ile ilikuwa kama wanachomeka Gia na kuniongezea mwendo.
Unafikiri kama ningewasikiliza Miaka hiyo Leo ningekuwa hapa? Ungenijua wewe?
Ningepewa nafasi mbalimbali za kuandika makala au hutoba za baadhi ya viongozi wa taifa hili?
Au unafikiri makumi kwa mamia ya Watanzania wanaonipigia simu kuomba ushauri, wengine kunipa mialiko binafsi na kwenye matukio ya shughuli zap, wangenialika kama ningekata tamaa na kuishia njiani?
Ni kweli wakati unaanza hautakuwa na uzoefu wa kutoa jambo zuri lenye kuwavutia watu wengi. Lakini ni ukweli pia hata utakapokuwa bingwa bado kuna watu wachache hawatakukubali.
Watu hao wote ni wako. Kila kundi litumie kukunufaisha na kukufanya kuwa Bora zaidi.
Wakati unaanzia chini usiangalie madhaifu yako kama kikwazo. Yaangalie kama kichocheo cha wewe kufikia malengo yako.
Watu wanakuona huwezi, jifuhze ongeza maarifa waone kuwa unakua na unaanza kuweza. Sio ukate tamaa.
Watu hawakuamini, ni jukumu lako kuwaaminisha kuwa unaweza kwa kazi zako. Teka Imani yao. Usitie tie huruma kuwaomba wakuamini. Show them you can.
Usianzie juu wakati unajua upo chini. Huko ni ku-fake.
Hujawahi kufanya biashara yoyote. Unataka kufungua biashara ya duka la nafaka. Anza kidogokidogo anzia chini hata kama kipato chako ni kikubwa.
Unamtaji wa milioni kumi. Anza na milioni Moja au mbili.
Kuanzia chini kutakuweka katika faida zifuatazo;
1. Kujifunza na kupata uzoefu.
Ukianzia chini utajifunza kwa namna nzuri kisaikolojia. Itakujenga Sana. Lakini ukianzia juu utajifunza in hardway ambapo haitakuwa funzo nzuri kisaikolojia kwa itakuathiri pakubwa kwani utakuwa umepata hasara kubwa.
Ndio maana mtoto huanza kwa kukaa, kutambaa kisha kusimama, kutembea kisha kukimbia.
Mtoto akikaa hata akianguka haumii Sana na inamfunza kuliko akitoka moja kwa moja mpaka kusimama.
Unaweka milioni 10 kwenye biashara mpya usiyoijua. Ukipata hasara haitakupa funzo lenye maana tofauti na Yule mwenye milioni 10 aliyeanzisha biashara hiyohiyo kwa mtaji wa milioni Moja au Mbili huku hela zilizobaki akizitumia kama silaha ya akiba kulinda biashara.
2. Kuepuka ushindani mkubwa na maadui wakubwa bila ulazima.
Jitahidi unapofanya movements zako kukwepa kupambana na watu wenye nguvu kukushinda.
Maji hufuata mkondo kwa kuepuka vikwazo na vizuizi vikubwa.
Maji madogo hayapandi mlima. Ukiwa mdogo epuka kupambana na watu waliokuzidi. Jitahidi ujifunze kutoka kwao ikiwezekana kuwa nao karibu.
Unaingia kwenye game unakuta Wakongwe. Hujui hili wala lile. Hujui biashara hiyo ikoje na inafanyikaje. Unajua juujuu tuu.
Umekopa pesa zako huko unaimwaga yote kama mjinga.
Njia sahihi ni kuingia kwa low Key, anzia chini Kwa lengo la kutotibua maji na kushtua wakongwe. Pia kukusanya taarifa za msingi za hiyo biashara.
Elewa, taarifa halisi za biashara husika huwezi kuzipata kwa kuuliza watu isipokuwa utazipata kwa kufanya biashara husika. Wahenga wanasema kitanda usichokilalia huwezijua kunguni wake
Na siri ya kaburi aijueye ni maiti.
Huwezi ijua biashara kwa kusoma kwenye vitabu au kusikiliza maprofesa au matajiri. Biashara utaijua wakati umeingia kuifanya.
Hayo ya vitabu na maneno ya watu ni asilimia 20% tuu ya kile kilichomo kwenye biashara husika.
Ndio maana unatakiwa uanzie chini ili kusoma upepo unaelekea wapi na lini hubadili uelekeo.
Taikon Master sina la ziada.
Acha niinjike makande yangu hapa. Kwa wapenzi wa makande karibuni.
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam