BUSARA ZANGU
JF-Expert Member
- May 5, 2013
- 778
- 1,269
Mshahara haujawahi kutoshaHizo za kutunza mkuu si mpaka ziwepo? Au unazani tunavipato sawa?
Ila ngoja waje wenye ajira na mishahara minono
Mkuu za kutunza huwa zipo tu. Lakini pia za kutunza huwa hazipo tu. Inategemeana na utayari wako.Hizo za kutunza mkuu si mpaka ziwepo? Au unazani tunavipato sawa?
Ila ngoja waje wenye ajira na mishahara minono
Binadamu wengi (90% ambao ndio masikini na middle class) huwa wanaishi/wanatumia kwa kadiri anavyoingiza pesa, ndio maana hawajawahi kuona kama kuweka akiba inawezekana. Kwao kila siku pesa haitoshi.Mshahara haujawahi kutosha
Kwa mfano utasikia wanasema jamaa ana hela lakini nguo zake ni zile zile, au jamaa ana hela lakini mchoyo.Mada nzuri sana. Asilimia 95 au zaidi ya watu wanaona pesa hazitoshi. Akiwa na mshahara laki tano hautoshi. Akipandishiwa ukafika milioni hautoshi pia. Akifikisha milioni mbili bado ataona hautoshi. Kisa? Kila kipato kikiongezeka matumizi yanaongezeka. Mtu pekee atakayeweza kuweka akiba kama mtoa mada anavyosema ni mtu mwenye NIDHAMU YA PESA ya hali ya juu. Hao ni wachache sana. Nidhamu hiyo unaikuta kwa matajiri tu. Ndio maana watu wengi wa kawaida wanawaona matajiri kama watu bahili. Kumbe sio ubahili bali ni nidhamu ya pesa
Kwa mfano utasikia wanasema jamaa ana hela lakini nguo zake ni zile zile, au jamaa ana hela lakini mchoyo.
Wanasahau Warren Buffet tajiri wa pili duniani, anaishi kwenye nyumba ya vyumba vitano ambayo alikuwa anaishi humo tangu mwaka 1958
100 mkuuWakuu Habari za Asubuhi
Kuna mambo mengi ambayo huwa yanakwama kwasababu ya kushindwa kuanza leo, watu wengi wamekuwa pale pale, miaka nenda rudi sababu ya kuahirisha kufanya mambo ambayo pengine yangewasogeza mbele kama Wangeanza kufanya jambo kwa wakati.
Watu wanaahirisha kuoa, watu wanaahirisha kusoma, watu wanaahirisha kujenga, watu wanaahirisha mambo mengi ambapo baadae wanakuja kujilaumu kwanini hawakufanya. Huu ni ugonjwa mkubwa.
Umewahi kuwaza ungeanza kutunza Tsh 100,000/= au 200,000/= au 300,000/= kila mwezi kwa miaka 5 iliyopita leo ungekuwa wapi? Vipi ukianza leo, baada ya miaka 5 ijayo utakuwa wapi kiuchumi. Achana na kiasi cha fedha, embu chukulia ungeanza leo kutunza/ku save angalau 15%/20% ya pato lako mwaka 2023 utakuwa na fedha kiasi gani? Anza Leo.
Anza Leo, panda miti leo kwenye shamba lako, ili miaka kadhaa upige hela. Najua ukiwaza mpaka mwaka 2025 ndio uvune miti yako utaona mbali sana. Lakini je, mwaka 2010 ungeambiwa panda miti yako ili uje uvune 2017,si ungeona ni mbali sana. Lakini huu ndio mwaka 2017. Kwa aliyekuwa na spirit kama hii mwaka 2010,leo anakula matunda.
Anza Leo kulima, Anza Leo kufuga, Anza Leo biashara, usiahirishe. Watu wengi wapo pale pale sababu ya kuahirisha.
Tarehe 30/11/2018 utajiuliza kwanini hukufanya leo, utajilaumu kwanini hukuanza leo.
Sawa mkuu. Orodha imekuwa ikibadilika mara kwa mara. Nina imani hiyo haijapoteza msingi wa hoja yangu.Warren Buffet ni tajiri wa nne duniani na siyo wa pili. Nafasi ya pili anaishikilia Gates, ya tatu Ortega na ya kwanza yupo Bezos wa Amazon.
Mkuu ni kweli hizo changamoto huwa zinajitokeza, cha msingi ni kuwa na malengo.Somo Zuri Shida Ipo Hv Unaweka Akiba Then Kibarua Kinagoma Kwa Cku Kadhaa Unachokifanya Unachukua Ile Akiba Uloweka Unaitikita ,then Una Anza Upya