Anyimwa Unyumba Amuua Mtoto Wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anyimwa Unyumba Amuua Mtoto Wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 13, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [TABLE]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Meshack Kazonda mwenye umri wa miaka 35, ameuliwa na wananchi wenye hasira baada kumuua mtoto wa kaka yake ili aliyekuwa mke wa kaka yake aweze kukubali kumpa unyumba na hivyo kuzaa naye mtoto.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Meshack ambaye ni mkazi kijiji cha Mititi wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa alifariki dunia baada ya kushushiwa kipigo cha nguvu na wananchi wenye hasira baada ya kumnyonga mtoto wa marehemu kaka yake mwenye umri wa miaka minne, Ezekiel Chaila na kisha kuitupa maiti yake uwani wa nyumba aliyokuwa akiishi na aliyekuwa mke wa marehemu kaka yake.

  Kamanda wa polisi wa Rukwa, Isuto Mantage aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea jumatatu wiki hii kwenye majira ya saa tatu usiku kwenye kijiji hicho cha Mititi.

  Kwa mujibu wa kamanda, Mantage, Meshack alimrithi mke kaka yake ambaye alifariki ghafla miaka miwili iliyopita. Lakini baada ya kumuoa mwanamke huyo aliyekuwa mke wa kaka yake, alikataa kumpa unyumba Meshack kwakuwa alikuwa hataki kuzaa naye.

  Taarifa zaidi zilisema kwamba Meshack alikuwa hampendi mtoto huyo pekee wa marehemu kaka yake na alimuona kama kizuizi cha mke wake kumpa unyumba na hivyo kuamua kumuua mtoto huyo ili mkewe aweze kukubali kuzaa naye.

  Siku ya tukio hilo, mkewe alienda kununua mafuta ya taa dukani na kumuacha Meshack akiwa na mtoto huyo. Aliporudi hakumuona mtoto huyo na baada ya kumbana sana Meshack ugomvi ulizuka kati yake na Meshack. Baada ya Meshack kuzidiwa ubavu na mkewe alitoboa siri kuwa amemuua mtoto Ezekiel na alienda kumuonyesha mkewe sehemu aliyoitupa maiti yake.

  Kwa uchungu wa kuiona maiti ya mtoto wake, mkewe alipiga kelele zilizowavuta majirani ambao waliwasili wakiwa na mapanga na mawe na silaha zinginezo wakidhani kuna mwizi.

  Baada ya kugundua kilichopelekea mke wa Meshack kupiga kelele, wananchi wenye hasira walianza kumshambulia Meshack na kumuua hapo hapo.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  oooogh, .................. what???................... ah, ah, ah..................... i am speechless,......................... hivi huyo majaa naye alikuwa binadamu kamili??................
   
 3. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Aisee huyu jamaa alistahili kabisa hiyo hukumu maana malipo ni hapa hapa duniani kwa mungu hakuna mahakama.
   
 4. I

  Ikunda JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2011
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 722
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ohhh My God! tunaelekea wapi jamani??? masikini mtoto yule hakuwa na hatia yeyote Mwenyezi Mungu ailaze roho yake pema, 4yrs tu kauwawa kifo cha mateso,

  Eeee mwenyezi Mungu wanusuru/waepushe/ walinde watoto wote ktk ulimwengu huu. AMEN
   
 5. mchakavumlasana

  mchakavumlasana JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  hivi bado watu wanarithi mke?

  ila amelipwa hapa hapa kw dunia
   
 6. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  omg! mtoto hana hatia jamani malaika wa watu, kweli kuna viumbe wakatili sana duniani...yani angekatwa katwa vipande huyo mbaba baaada ya kuulizwa!..
  Halafu hizi mila za kurithiana bado zinaendelezwa?!! mweeh!
   
Loading...