Utaratibu wa kuwa na anwani za makazi ni jambo jema sana; Napongeza sana Serikali yangu
hata hivyo ninamapendekezo yafuatayo;
1. napendekeza kuwe na nyongeza ya kuelekezwa namna ya kuandika anwani baada ya kupata namba kwenye Nyumba;
Mf: utakuta nyumba imeandikwa #46 sinahakika nikisema Naishi Bugurini - Dar; nyumba #46 imetosha?
Namaanisha kila mtu ataandika kivyake na pengine kuchanganya; mwingine; Buguruni dar, karibu na Msikiti mkuu, nyumba namba #46 nk Nimeandika kwa kuwa kwenye maeneo kuna vitu maarufu pengine kuliko mitaa yenyewe; mf: Shule za zamani, Viwanda, Hospitali, Misikiti/makanisa nk. mfano; nakaa morogoro mjini karibu na geti la kiwanda cha Tumbaku # 46 NK
2. Nimeona Namba zina andikwa kwa kalam (nafikiri Marker pen) wananchi wasipokuwa makini muda sio mrefu nyingi zitafutika hasa Vijijini; sijui kutakuwa na utaratibu gani wa kuhakikisha zinadumu tusirudi huko baada ya miaka 5)
Ni mawazo yangu!