Antony Lusekelo( Mzee wa Upako) alalamika kunyang'anywa kipindi chake Channel Ten

kwa sasa anaonekana mzee slow mo slow mo na kipindi chake cha kupiga simu


=======
Mzee wa upako adai kwa miaka kumi na tano aliyokuwa na kipindi cha Tutashinda Channel Ten amedai amepata mafanikio makubwa kama watu kuponywa kiroho, magonjwa na mafanikio mengine mengi.

Lakini pia amedai amepata changamoto niyingi ambazo ziliweza kugharimu maisha yake, watoto wake kunyanyaswa kisaikolojia kwa kuambiwa baba yao ni Freemason.

Amedai kuwa tarehe 12 alipigiwa simu kuwa kipindi chake cha siku ya Jumamosi amepewa mtu mwingine bila taarifa, amelalamika kuwa wamemtupa kama mbwa tena mbwa koko bila taarifa hata ya masaa mawili achana na wiki moja.

Amedai alikuwa kaandaa kipindi kama kawaia lakini hakupewa taarifa kuwa hana kipindi tena. Amesema wangekuwa waungwana wangempa taarifa ya kumnyang'anya kipindi hata kabla ya saa moja.

Amedai hajawahi kuchelewa kulipa hela yao amekuwa mwaminifu kwenye malipo kwa muda wa miaka 15 hajawahi kuchelewesha malipo hata siku moja.


Sent from my TECNO W5 Lite using JamiiForums mobile app
 
Kipindi kimechukuliwa na mtangazaji Polepole ,mbunge wa viti maalumu.
 
Back
Top Bottom