Antony Joshua Vs Andy Ruiz 2, tukutane hapa kwa updates

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,792
15,693
Yamebaki masaa machache tushuhudie lile pambano litakalosimamisha dunia kwa dakika kadhaa lililopewa jina CLASH ON THE DUNES ambapo litafanyika Saudi Arabia.

Pambano hili limekuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa ndondi duniani, hii ni baada ya AJ aliyekuwa bingwa na kipenzi cha watu kupigwa pambano la kwanza lililofanyika June 1 kitu ambacho wengi hawakuwaza, na pambano hilo kuwekwa katika kumbukumbu ya one of the biggest boxing upsets of all time. Je AJ ataweza kurejesha mikanda yake aliyopoteza? Tusubiri Jmosi.

Screenshot_20191202-184219_1575350800593.jpeg
 
Na iwe hivyo aseee itakuwa mbaya sana akipigwa yaani itakuwa ndio basi nani atataka kupigana na AJ tena?
Mapambano atayapata, unajua jina lake linauza kuliko bondia yoyote (ukiondoa Canelo), sema thamani yake na legacy itakuwa imeshuka sana. Kila bondia Heavyweight anatamani apigane na AJ ndipo kwenye hela kwa sasa
 
Mimi nataka apigwe ili sisi wenye vitambi tuendelee kuwa na heshima huku mtaani,maana tumedharaulika sana.....
Hii ndo comment yako halafu unaniambia unajua ngumi kwahiyo mimi niliandika utumbo?

Anyway, Ruiz ana ngumi nzito kumzidi AJ, AJ ana weak chin na pumzi hana.

Pambano la AJ na Klitschiko lilithibitisha juu ya chin na pumzi ya AJ. Kama atafanyia kazi pumzi kisha akaachana na 'Attack the trunk and the tree will fall' atashinda.

Hii ni unaambiwa 'Don't get crazy and we are home' so AJ kazi ni kwake.

Ruiz mwili wake unamsaidia kuabsorb body shots, ana ngumi nzito na anaweza kuvumilia offensive shots. Kibiashara hana cha kupoteza, kihadhi hana cha kupoteza pia as huyu mtu alichukuliwa ni journeyman na stepping stone kwa AJ (Nafikiri ni sababu pia akataka pesa ndefu kurudiana as he knew after this he is done)

Ruiz akiingia akawa karelax, toying, showboating na kumvuta AJ mpaka raundi ya tano naona akishinda. Unless awe kalipwa more than what we see on paper.

Sitarajii action packed fight as kila mtu atakua busy kumvizia mwenzie ateleze.
 
Halafu Ruiz hana njaa tena, kwenye mahojiano yake nimeona amesema ameshatimiza ndoto ya kuwa bingwa. Ni kweli ulichosema yeye hana cha kupoteza kivile, ndio maana alijitahidi kumng'ang'ania Eddie Hearn amlipe vizuri kama anataka aende kupigana Saudi Arabia(alifanya kamgomo). Kwa taarifa za chini nimesikia analipwa $15 Mil, dau ambalo alikuwa anaota tu kulipata maana pambano la Kwanza alilipwa kwenye $7 Mil. Ila kwa upande wa AJ anavuta $ 85 Mil pamoja na kutokuwa bingwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom