tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 23,519
- 21,549
Mh Anne Kilango Maleccela anasubiri kupangiwa kazi nyingine na Rais Dr Magufuli na huenda akapangiwa kazi nzuri zaidi ya kazi yake ya awali ya Ukuu wa Mkoa.
Kuna baadhi ya taarifa zinasema kwamba huenda akateuliwa kuwa balozi katika mojawapo ya nchi za ng’ambo.
Ofisa mmoja wa Ikulu ambaye hakupenda kutajwa jina lake alinukuliwa akisema kuwa “Rais Magufuli anajiandaa kumpangia Kilango kazi nyingine na kuna uwezekano mkubwa akateuliwa kuwa balozi katika nchi za Ulaya, Marekani au Asia”, alisema.
CHANZO 1: Gazeti la ZANZIBAR YETU
CHANZO 2: MWANANCHI
NANUKUU: "Rais Magufuli alisema baada ya kutengua uteuzi wake, Kilango ATAPANGIWA KAZI NYINGINE huku akiwataka wakuu wa mikoa yote kuwafichua watumishi hewa wote ili waondolewe mara moja" MWISHO WA KUNUKUU. Hebu jisomee wenyewe HAPA: Kilango akutana na hasira za JPM siku 30
MAONI YANGU
Rais Maguguli anajua sana kucheza na akili za watanzania. Staili yake ya utumbuaji majipu imenjengea umaarufu kwa wananchi kiasi kwamba kila jambo analofanya, liwe zuri au baya, wananchi hushabikia tu kama jongoo pasipo kuelewa mantiki na manufaa yake kwa umma wa watanzania.
Wakati watanzania wanamshabikia Magufuli kwa kutumbua JIPU kumbe ndio kwanza anafikiria kulipangia JIPU kazi nzuri na ya heshima zaidi ya Ukuu wa Mkoa. Nchi hii haiishi vituko.