Anna Mghwira avuliwa uenyekiti ACT-Wazalendo, Yeremia Maganja akaimu uwenyekiti

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,709
13,461
Heshima kwenu wakuu,

Kutoka Makao Makuu ya ACT Wazalendo

Leo kuna mkutano wa Chama cha Siasa ACT Wazalendo na Waandishi wa habari.

Leo nmefanikiwa kufika eneo la tukio, hivyo ntawaletea Updates ya kile kitakachojiri. Mkutano unaanza saa nane kamili.

Karibuni.



Screenshot from 2017-06-07 15-53-58.png


=======

UPDATES;

=>⁠⁠⁠Tumewaiteni kuhusu haya mambo yanayoendelea

=>Mama Anna aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa

Kamati kuu ya uongozi imekaa Imezingatia haya

=>Hatuna kipangamizi Rais kumteua yeyote

=> ACT Wazalendo ni chama cha siasa cha kutumikia wananchi

=> Rais kavunja mwiko kwa kuanza kuteua wapinzani

=>Huu ni uthibitisho kwamba ACT ina viongozi bora hivyo inaweza kuongoza nchi.

=>Bado tunao wazalendo wa kutosha, hivyo raia asisite kuchagua wengine
=>CCM wajifunze kupitia kwetu kuchagua viongozi bora

=>Kamati ya uongozi inamshauri Rais kuweka mfumo bora wa kuazima watu kutoka vyama vingine kwa kuweka mashauliano ili kuepuka migongano ndani ya vyama.Japo anao uwezo, hii ni kuimarisha umoja wa kitaifa

=> Kuteua bila mashauriano kunaleta wasiwasi miongoni mwao

=>ACT inampongeza Anna Mghwira kwa kuteuliwa

=> ACT imeona kutakuwa na mgongano kati ya nafasi yake na chama

=> Katiba ya ACT Wazalendo, Mama Anna Mgwhira amekoma kuwa mwenyekiti.

=> Kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa hawezi fanya kazi kwa ufanisi kwa ACT- wazalendo.

=>ACT inamshukuru kwa kufanya kazi kwa uzalendo na ACT Wazalendo imemteua ndugu Yeremia Maganja kuwa Makamu Mwenyekiti mpya

Maswali

1.
Je, hamjashauriana katika uteuzi huu?


=> Kama tulivyoeleza mwanzo, Rais alimteua mama wakati yupo nje ya nchi na sisi tulipata taarifa na tukamtafuta kwa mashauriano. Tumetoa tamko baada ya kushauriana na Mama Mghwira

2. Mama bado ni Mwanachama halali wa ACT Wazalendo, Kupewa ilani ya CCM mnaichukuliaje?

=> Rais na vitengo vyake vyote vimejilidhisha kwamba ACT ina viongozi waadilifu, huu ni ujumbe kwa watanzania kwamba ACT-Wazalendo ipo tayari kupewa nchi. Na watanzania wenyewe wameona

=>Ni mujimu haya mambo yakaeleweka, tunapofanya uchaguzi, wananchi wanasoma na kuchagua ilani ambayo wanaona inafaa. Kwa hivi sasa chama kinachoongoza ni CCM na ilani inayotekelezwa ni ya CCM. Mwaka 2015 Mama Anna pia alimpa ilani ya ACT Wazalendo na tunaamini kuna mambo mazuri ya Ilani ya ACT

=>ACT tungeshinda tungeunda serikali ya umoja wa kitaifa, hivyo hiki kinachofanywa ni moja ya Malengo tuliyokuwa nayo.ACT tungechagua watu kutoka vyama vyote.
18882175_1776875265958037_8632259359512225577_n.jpg

Ndugu Yeremiah Kulwa Maganja Kaimu Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo

=======

MAAMUZI YA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI JUU YA UENYEKITI WA CHAMA CHA ACT Wazalendo

Tarehe 3 Juni, 2017 Mwenyekiti wa chama chetu cha ACT Wazalendo, Mama Anna Elisha Mghwira aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kufuatia uteuzi huu, Kamati ya Uongozi wa Chama ilikutana leo tarehe 7, Juni 2017 kutafakari juu ya matokeo ya uteuzi huu katika utekelezaji wa majukumu yake ya Uenyekiti na mustakabali wa siasa za Chama chetu na mfumo wa Demokrasia ya Vyama Vingi nchini kwetu. Katika tafakari yake, Kamati ya Uongozi imezingatia yafuatayo:

Kama Chama hatuna kipingamizi kwa Mama Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa, wala kumzuia ndugu Rais kumteua mtanzania yoyote na haswa mwana ACT Wazalendo kutumikia Taifa letu. ACT Wazalendo ni chama cha siasa na azma yake ni kutumikia Taifa.

Kamati ya Uongozi inampongeza Rais kwa kuvunja miiko ya siasa za Tanzania kwa kuanza kuteua wapinzani katika utumishi wa umma. Uteuzi wa mara ya pili wa ndugu Rais kwa wanachama na viongozi wa ACT Wazalendo ni kielelezo kuwa chama chetu kinao watu makini na wanaofaa kuongoza. Ni uthibitisho kuwa ACT inapaswa kupewa nafasi ya kuongoza nchi katika uchaguzi ujao. Tunapenda kumhakikishia ndugu Rais kuwa tunao watu waadilifu na wazalendo wengine wengi ndani ya ACT kama jina la chama chetu linavyojipambanua yaani ACT- Wazalendo. Asichoke na asisite kuja kuvuna na wengine maana tumeonyesha uwezo wa kutengeneza wengi wa aina hiyo. Muhimu zaidi, Chama chake cha CCM kijifunze kutoka kwetu namna ya kuchagua na kuvutia viongozi waadilifu na wazalendo katika chama chao.

Kamati ya Uongozi inashauri Rais au mamlaka yoyote ile ya uteuzi kuweka mfumo bora wa kuazima watu kutoka vyama vingine kumsaidia kazi za Maendeleo ya Nchi Kwa kufanya Mashauriano na Vyama husika ili kuepuka migongano isiyo ya lazima ndani ya vyama na katika jamii. Pamoja na kwamba Rais kama Mkuu wa Nchi anayo mamlaka ya kuteua yeyote amtakaye, lakini ni Afya na hekima teuzi hizo kufanywa kwa kushauriana na Viongozi wa Vyama husika ambavyo anachukua wanachama wake. Hii haitakuwa kuingilia mamlaka yake ya Kikatiba bali kuimarisha Umoja wa Kitaifa na hata Mfumo wa Vyama Vyama vingi nchini. Kuteua bila ya mashauriano kunaleta wasiwasi wa dhamira mbaya na kuathiri taswira ya vyama vya upinzani ambavyo Rais anachukua wanachama wake.

Kwa hiyo basi;

a. Kamati ya Uongozi imempongeza Mama Anna Elisha Mghwira Kwa kutambuliwa na hatimaye kuteuliwa na Rais kushika nafasi muhimu ya Mkuu wa Mkoa.

b. Kufuatia uteuzi wake kuwa Mkuu wa Mkoa, Kamati ya Uongozi imezingatia kuwa kutakuwa na mgongano wa moja kwa moja wa kiutendaji na kitaswira kati ya majukumu ya Uenyekiti wa chama na majukumu yake mapya, jambo linaloweza kuathiri Ufanisi wa moja wa nafasi hizi mbili.

c. Kwa mujibu wa Ibara ya 17(1)(iii) ya Katiba ya ACT Wazalendo na kutokana na mashauriano kati ya Mama Anna Mghwira na viongozi wenzake wakuu wa Chama, Mama Anna Mghwira amekoma kuwa Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo. Ibara ya 17(1)(iii) ya Katiba ya ACT inamfanya Kiongozi wa Chama kukoma kushika nafasi yake iwapo atashindwa kutekeleza majukumu yake. Ni dhahiri kuwa kwa kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa, Mama Anna Mghwira hawezi tena kutekeleza kwa ufanisi wajibu huu.

d. ACT Wazalendo, inamshukuru Mama Mghwira kwa muda, mchango, nguvu, busara na hekima zake alizozitumia katika muda wote wa Uenyekiti wake, na tunamtakia kila la kheri katika kutumikia nafasi yake mpya.

e. Mwisho, Kamati ya Uongozi (Kwa mujibu wa Ibara za 29(24) ya Katiba ya ACT Wazalendo imemteua Ndugu Yeremia Kulwa Maganja kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Chama Taifa hadi uchaguzi Mkuu utapoitishwa Mwezi Machi 2018.

Ahsanteni Sana.

Samson Maingu Mwigamba

Kaimu Kiongozi wa Chama

Juni 7, 2017

Dar es salaam
 
Tumekaa kwenye viti tunasubiri. .....

Zitto embu tegua kitendawili hiki
 
Saa nane na dk kumi bdo haujaleta updates. Vp au mmetekwa hapo au ndio mmesambaratishwa na wale vijana wa mkuu? Tupe updates
 
[HASHTAG]#Differential[/HASHTAG] Equations

ngoja tuwasubiri watakuja na povu gani
 
Dah waseme tuu hiki ni kikao kimeitshwa na mwenyekiti wa tawi mojawapo la chama bana na sio mwenyekiti au kiongozi mkuu wa chama
 
Mbona nasikia Zitto hayupo, yupo njiani anaelekea ujerumani kuhudhuria mkutano wa vyama rafiki?
 
Back
Top Bottom