Kutoka kwa Kaka Ebby Siwa.
Kuna wakati ili Muziki wetu upanuke zaidi tunahitaji jasiri wa kusimamia lakini si kwa kutoa majibu mepesi kwa sanaa yenye kuhitaji majawabu huru.
Kwa zama hizi, tena kwa utitiri huu wa vyombo vya habari na kuzagaa kwa mitandao Wasanii watalalamika wanaibiwa ama kubaniwa Kazi zao huu ni uzwazwa wa hali ya juu.
Tuangalie tunapokwenda kabla ya kutoa majibu mepesi lazima tufikirishe akili kwanza!
Nani asiyemfamu anguko la Wasanii wengi huko nyumbani Tanzania ni malimbukeni wenye kutafuta sifa badala ya kuweka mipango ya maisha ya mbeleni.
Naongea huku nikitanguliza maslahi mapana ya vijana wote wa Tanzania waliojiajiri kupitia Sanaa, nawaheshimu na kuwapenda sana lakini kuna mahali tunakosea mno.
Kwanini Kila siku lawama zinadondoka kwa mtu mmoja yeye ni nani? Kila msanii anayefeli baada ya muda wao kupita anatupa lawama. Ipo mifano ya wasanii walipoona shimo walidumbukia wenyewe bila kusukumizwa?
Joslin alipoanza kuchoka aligeukia madhabahu yeye aliuona mwisho wake?
Juma Nature mtoto wa Temeke aliapata nafasi ya kusimama jukwaa moja na Lil Kim lakini leo hii yupo Temeke walimwengu wanajua anafanya nini hata Pfunk hajui kwanini au sababu majani naye kachoka?
Z Anto pesa zilimlevya akamaliza Kazi alipopata Mark 2 Grande kama ni msanii mwenye kipaji Tale angempeleka Wasafi. Tunagundua jibu ni hapa ni ulimbukeni na kutokujijali.
Wakati nipo kwenye Treni naenda Beiersdorf (Hamburg Germany) nikakutana na Habari ya kushangaza Instagram ukurasa wa Rehema Chalamila (Ray C) analalamika nimesoma kwa undani nikasema bado Watanzania kuna upumbavu tuna ishi nao.
Kubadilika kwa Venue show ya Lady Jay Dee iliyopata walaji wachache tuseme basi wameangukia pua. Lawama zikaelekezwa kwingine hii si Sawa.
Tuanzie na hili la kwanza Show iliyokuwa ifanyike Golden Tulip, Ray C anasahau kuwa muda wa mwisho kisheria ni saa 5:30 labda Rafiki yako Jide alikudanganya shughuli kuwa amebaniwa Sababu alishtukizwa hapana Show zote za nje husitishwa saa 5:30 usiku kupisha utaratibu wa wateja.
Toka mwanzo waandaji walikuwa na wasiwasi kuhusu mahudhurio kumbukumbu ni Show aliyoifanya Hyatt pale mwanzoni mwa February tujiulize ni wangapi wanakumbukumbu na idadi ya mahudhurio ya watu ni muendelezo wa yaliyotokea February.
Show ilihamishwa Police Mess Sababu waliona ni auheni kidogo hapa ndipo walipokosea Team ya Jide kwa kipindi hiki watanzania wasiowapenda polisi eneo kama lile siyo rafiki watu kwenda. Hakuna mchawi wala figusu hapa walijiloga wenyewe.
Sawa kwenye andiko Ray C umelalamika unabaniwa hapa nyumbani Tanzania.
Mwanangu Shellow ana miaka mitano sasa picha yako anayoifahamu kuhusu wewe ni mtumiaji wa dawa za kulevya siyo msanii napata tabu kumuelewesha kwamba Wewe ulikuwa namba moja wa kukata nyonga.
Hii ni hatari sana lakini imenifikirisha mengi sana kama nyumbani unabaniwa Kila nikipiga story na kina shafii Werru, Willy Tuva Mzazi wananiambia Upo Nairobi unazunguka tu embu niambie huko umetengeneza hits ngapi huu mwezi wa saba sasa.
Wasanii wengi hamjui Kesho yenu na Muziki hauwezi ukadumu na kukaa milele. Wengi ni wabinafsi msiopenda wengine wasonge mbele sababu hamtaki kukubali muda wenu umepita.
Haya ni majina makubwa sana kwenye mpira wa miguu ni nani aliwashusha Edibily Lunyamila, Said Maulid Kalikula (CMG) Stephen Mapunda, Joseph Kaniki wasivuke mipaka jibu ni hakuna wamebakia na majina lakini leo hawewezi kugombania namba na kichuya au Ibrahim Ajib. Wamekubali muda wao umepita tayari.
Kwanini tutafute majibu mepesi kwa ajili ya Sanaa yetu? Lipo Tatizo mahali kwanza Wasanii wamekosa ushirikiano na mashabiki wao kabisa hawapo pamoja na watanzania hichi ni kipindi Wananchi wanahitaji faraja kutoka kwa Wasanii wao wanaowapenda.
Embu nyinyi Wasanii niambie ni nani amekuwa faraja kwa Watanzania zaidi ya Kila siku kuimba nyimbo za kitandani?
Ushauri wangu sanaaa ni dubwasha pana mkipata hela ajirini menejimenti zenye uweledi msikimbilie Pombe na Anasa mkishuka mnatusumbua, Hata mkiumwa Kila siku mnatembeza bakuli.
Narudia tena, Wasanii mkiweza kukubali matokeo halali kuwa nyinyi ni wajinga na kukaa chini pamoja na kuamini mziki una zama zake mtaepukana na lawama za kijinga.
Tazama Marekani wapo wasanii wakali kama Ja Rule, 50 Cent, Nas Escoba, Mariah Carey, hawana nafasi ya kumtupia mtu lawama mbele ya wasanii kama Migos, Drake na Cardi B hawa ndiyo wanaotamba kwasasa muda unabadilika tukubali wakati ni Ukuta ukipita umepita.
Siwezi kukaa kimya napasua jipu pwaaa!
Ebby Mkandara Siwa.
Northern Hemisphere.
London.
Niandikie
ebbysiwa@gmail.com