Anguko la CCM ni Julai 12

Anguko la CCM ni Julai 12

Mfukutuzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2015
Posts
239
Reaction score
175
Ni suala lisilo na ubishi kuwa CCM, bila hata kuwataja wapinzani, itajiua yenyewe pale tu litakapotangazwa jina la mgombea wa Urais Julai 12, na hii inatokana na sababu kuu tatu;

1. Makundi: Hakuna asiyejua kuwa CCM sasa kimekuwa ni chama cha makundi makubwa, makundi hatari yenye ajenda binafsi kupitia mgombea. Nakuhakikishia hakuna kundi litakubaliana kirahisi na mgombea kutoka kundi tofauti, tofauti na makundi ya nyuma ya kuzuka na kupotea, makundi ya sasa ni makundi hatari na yamedhamiria, mfano, lipo kundi linaitwa kundi la Safari ya Matumaini, kundi hili ukiliangalia limebeba watu wenye nafasi kubwa ktk chama na wadhamini wakubwa wa chama, hawa ni watu waliojihakikishia hivyo hawako tayari kumwona mgombea wao anapoteza kwa sababu kupoteza kwake ni kupotea kwa nafasi zao, kama tunavyojua CCM sasa ni chama cha visasi.

Hivyo makundi haya kwa kuwa haliachwa yakachanua yakastawi, hakuna shaka chama kinahaha kuyatuliza lakini haiwezekani kwa sababu kila mmoja anaongea lake, hii ni sindano namba moja ya sumu itakayowaua taratibu toka Julai hadi Oktoba inafika

2. Utanganyika na Uzanzibar: Ili kuwaengua wagombea wenye nguvu watalazimika kutumia sera kama ile iliyomng'oa SITTA kwenye uSpika kwa kusema wanahitaji Mwanamke, katika hili tunajua kabisa watasema ni zamu ya "Mzanzibar", na dalili imeshajionyesha kwamba mfumo umejielekeza kwa mwanachama mchanga Jaji AGUSTINO RAMADHANI ambaye bila kujali kadi yake ya uanachama ni ya mwaka gani, bila kujali anakijua chama kwa kiasi gani mpaka awe Mwenyekiti wa chama watalazimika kumweka kwa sababu wengine wana mizigo ya kashfa hivyo muda hautatosha kwa chama kuanza kuwasafisha, vile vile ni faida kwao kwa Zanzibar na Bara kwa sababu za mchanganyiko wa Dini, yaani Ukristo-Uislamu. Sasa kwa jinsi tu hali ilivyo, wale wa Tanganyika hawataki kuongozwa na wachache, huu nao ni mtifuano mwingine ndani ya chama

3. Uroho wa madaraka: Katika historia ya Afrika na Dunia, CCM imevunja rekodi kwa kutoa wagombea wengi nafasi nyeti kama hii ya uRais, wanajitetea eti ni kukua kwa Demokrasia wakati sababu ni tatu tu; Moja ni kutengeneza jina ili kuonekana na kiongozi ajaye, pili ni jinsi Nchi ilivyoendeshwa kwa miaka hii kumi na mtangulizi wao, hivyo kila mmoja anajiuliza "kama hata huyu kaweza mimi nitashindwaje?", hili ni tusi kubwa. Sababu ya tatu kubwa, ni Uroho wa Madaraka, kama tunavyojua kwa sasa Uongozi sio utumishi tena bali ni Biashara, basi kila mmoja ana hamu ya kufika Ikulu, kila mmoja anatamani kuwa Rais kwa sababu kama Mbunge tu mbali na Mshahara mnono analipwa kiinua mgongo cha Mil.238 vipi kwa Rais?

Ni hili linamfanya kila mmoja atumie mbinu yoyote ile iwe safi au chafu ila tu afike Ikulu, hakuna anayekubali kumpisha mwenzake, hili nalo janga jingine

Ningeweka sababu nyingi za anguko hili ila hizi tatu (ambazo wengi wanaziruka) zinatosha kwa wewe kupata picha ya jinsi Dola hii itakavyoanguka kabla hata ya kufika uchaguzi Oktoba

Mr. ZigZag (#TeamTanzania)
 
Tumekusoma mkuu, wewe ni wachache kati ya wale wanajitambua. Ila hapo namba tatu nadhani si kweli!.

[h=2]The republicans[/h]Running

bush-square-150.jpg
Bush
Running

cruz-square-150.jpg
Cruz
Running

paul-square-150.jpg
Paul
Running

rubio-square-150.jpg
Rubio
Running

carson-square-150.jpg
Carson
Running

fiorina-square-150.jpg
Fiorina
Running

huckabee-square-150.jpg
Huckabee
Running

santorum-square-150.jpg
Santorum
Running

pataki-square-150.jpg
Pataki
Running

graham-square-150.jpg
Graham
Running

perry-square-150.jpg
Perry
Running

trump-square-150.jpg
Trump
Running

jindal-square-150.jpg
Jindal
Running

christie-square-150.jpg
Christie
Running
 
Nataka CCM igawanyike vipande vitatu nadhani ndio mwanzo na nchi kuendelea sasa..
 
Tumekusoma mkuu, wewe ni wachache kati ya wale wanajitambua. Ila hapo namba tatu nadhani si kweli!.

[h=2]The republicans[/h]Running

bush-square-150.jpg
Bush
Running

cruz-square-150.jpg
Cruz
Running

paul-square-150.jpg
Paul
Running

rubio-square-150.jpg
Rubio
Running

carson-square-150.jpg
Carson
Running

fiorina-square-150.jpg
Fiorina
Running

huckabee-square-150.jpg
Huckabee
Running

santorum-square-150.jpg
Santorum
Running

pataki-square-150.jpg
Pataki
Running

graham-square-150.jpg
Graham
Running

perry-square-150.jpg
Perry
Running

trump-square-150.jpg
Trump
Running

jindal-square-150.jpg
Jindal
Running

christie-square-150.jpg
Christie
Running

Kwan ukiwahesabu hao wanafika wangapi mkuu?
 
Hakuna namna ya kuiokoa CCM mwaka huu
ni anguko
ndio ni anguko kuu
 
CCM itakufa ila sio sasa, kitakachofanyika wale wagombea wote wenye makundi wanakatwa majina yao kwenye 5 bora na ni lazima wakubaliane na matakwa ya chama kwasababu wana maslahi yao hivyo kama CCM itakufa na maslahi yao yatakufa vilevile na hakuna aliyeko tayari kulishuhudia hilo likitokea.
 
Walaaniwe wote wanaoiombea CCM mabaya. Kila mwenye nia njema na nchi hii aseme AMIN.
 
Ni suala lisilo na ubishi kuwa CCM, bila hata kuwataja wapinzani, itajiua yenyewe pale tu litakapotangazwa jina la mgombea wa Urais Julai 12, na hii inatokana na sababu kuu tatu;

1. Makundi: Hakuna asiyejua kuwa CCM sasa kimekuwa ni chama cha makundi makubwa, makundi hatari yenye ajenda binafsi kupitia mgombea. Nakuhakikishia hakuna kundi litakubaliana kirahisi na mgombea kutoka kundi tofauti, tofauti na makundi ya nyuma ya kuzuka na kupotea, makundi ya sasa ni makundi hatari na yamedhamiria, mfano, lipo kundi linaitwa kundi la Safari ya Matumaini, kundi hili ukiliangalia limebeba watu wenye nafasi kubwa ktk chama na wadhamini wakubwa wa chama, hawa ni watu waliojihakikishia hivyo hawako tayari kumwona mgombea wao anapoteza kwa sababu kupoteza kwake ni kupotea kwa nafasi zao, kama tunavyojua CCM sasa ni chama cha visasi.

Hivyo makundi haya kwa kuwa haliachwa yakachanua yakastawi, hakuna shaka chama kinahaha kuyatuliza lakini haiwezekani kwa sababu kila mmoja anaongea lake, hii ni sindano namba moja ya sumu itakayowaua taratibu toka Julai hadi Oktoba inafika

2. Utanganyika na Uzanzibar: Ili kuwaengua wagombea wenye nguvu watalazimika kutumia sera kama ile iliyomng'oa SITTA kwenye uSpika kwa kusema wanahitaji Mwanamke, katika hili tunajua kabisa watasema ni zamu ya "Mzanzibar", na dalili imeshajionyesha kwamba mfumo umejielekeza kwa mwanachama mchanga Jaji AGUSTINO RAMADHANI ambaye bila kujali kadi yake ya uanachama ni ya mwaka gani, bila kujali anakijua chama kwa kiasi gani mpaka awe Mwenyekiti wa chama watalazimika kumweka kwa sababu wengine wana mizigo ya kashfa hivyo muda hautatosha kwa chama kuanza kuwasafisha, vile vile ni faida kwao kwa Zanzibar na Bara kwa sababu za mchanganyiko wa Dini, yaani Ukristo-Uislamu. Sasa kwa jinsi tu hali ilivyo, wale wa Tanganyika hawataki kuongozwa na wachache, huu nao ni mtifuano mwingine ndani ya chama

3. Uroho wa madaraka: Katika historia ya Afrika na Dunia, CCM imevunja rekodi kwa kutoa wagombea wengi nafasi nyeti kama hii ya uRais, wanajitetea eti ni kukua kwa Demokrasia wakati sababu ni tatu tu; Moja ni kutengeneza jina ili kuonekana na kiongozi ajaye, pili ni jinsi Nchi ilivyoendeshwa kwa miaka hii kumi na mtangulizi wao, hivyo kila mmoja anajiuliza "kama hata huyu kaweza mimi nitashindwaje?", hili ni tusi kubwa. Sababu ya tatu kubwa, ni Uroho wa Madaraka, kama tunavyojua kwa sasa Uongozi sio utumishi tena bali ni Biashara, basi kila mmoja ana hamu ya kufika Ikulu, kila mmoja anatamani kuwa Rais kwa sababu kama Mbunge tu mbali na Mshahara mnono analipwa kiinua mgongo cha Mil.238 vipi kwa Rais?

Ni hili linamfanya kila mmoja atumie mbinu yoyote ile iwe safi au chafu ila tu afike Ikulu, hakuna anayekubali kumpisha mwenzake, hili nalo janga jingine

Ningeweka sababu nyingi za anguko hili ila hizi tatu (ambazo wengi wanaziruka) zinatosha kwa wewe kupata picha ya jinsi Dola hii itakavyoanguka kabla hata ya kufika uchaguzi Oktoba

Mr. ZigZag (#TeamTanzania)

umetulia mkuu
 
Walaaniwe wote wanaoiombea CCM mabaya. Kila mwenye nia njema na nchi hii aseme AMIN.

Sidhani km kuna anayepoteza muda kuitaja CCM kwenye maombi yake, zaidi ni CCM inajiua na sumu iliyotengeneza yenyewe
 
Mpasuko unaanza leo, mara baada tu ya kuwaengua 33
 
Back
Top Bottom