Anguko kuu la CCM, dalili kuu ya kwanza!

Anguko kuu la CCM, dalili kuu ya kwanza!

Anyway,Mwenyekiti aliwatahadharisha wana ccm kuwa wajiandae kisaikolojia.
Naami wamelifanyia kazi agizo la Mwenyekiti,mda ndio huo umefika.
 
Wafutwe ndiyo wacha Ukawa wawadelete ccm maana hamna namna sasa tumechoka ndiyo ccm wafutwe tu.
 
CCM imedhoofika, imepasuka na kutikisika. CCM imetiwa unajisi na watu wanaoiongoza, kwa maana wameiacha misingi ya utawala bora na uwajibikaji, ndio maana laana imeila CCM. CCM inayumbayumba kama mlevi, inawayawaya kama machela, na mzigo wa dhambi zake umeilemea, nayo itaanguka na anguko lake litakuwa kuu.
 
Mkuu G Sam, kuchelewa ndio mpango mzima ili wakimpiga mtu chini, there will be no time to jump ships!.

Pasco
[/QU
i have always thought of the same strategy to be applied.Their only last but safe move
 
Mola anijalie uzima na afya tele nije kucomment tena oktoba baada ya uchaguzi mkuu
 
Ninaendelea kuamini maneno ya Mbowe kuwa come Octber 2015 hakuna uchaguzi wa viongozi...yaani UCHAGUZI HAUTAFANYIKA NA WATAENDELEA KUBAKI MADARAKANI KWA NGUVU.
 
CCM imeshajifia mkuu Sasa hivi limebaki jina tu. UKAWA wameshambulia kila sehemu ya Tanzania. Muda sio mrefu CCM itabakia kwenye vitabu vya historia mashuleni. Maana hawa viongozi wa Sasa hivi hawa wazee wa madili siku CCM ikipoteza uchaguzi tu na wao wanahama chama. Usije ukashangaa Ukiona wengine wamekimbilia chadema,wengine CUF ili waendelee kula. Maana hawa akili zao zinawatosha wenyewe. Hawa ndio mafisi bwana kwa tamaa huwawezi asilani. Bila ya kujali kwamba mahakama za ukweli muda huo zitakuwa zinawasubiri sio Sasa hivi mtu anasimama mbele ya baraza la maadili na kuthubutu kusema million 10 ni hela ya mboga tu. Wakati zaidi ya 70% ya watanzania wanaishi chini ya poverty line kwa maana ya wanaishi kwa dola moja kwa siku. Dah! IInaumiza kweli! Tanzania bhana! Sijapata kuona nchi ambayo viongozi hawana imani na watu wao kama Tanzania. Yaani huyo Mugabe ambaye anambiwa dictator,gaidi basi anasingiziwa yaani Tanzania kupiga hela imekuwa ni ushujaa zama hizi Dah! Hata kama baba wa taifa mwalimu nyerere anafufuka Leo akiona maisha wanayoishi viongozi wa Leo kwa jinsi yalivyokuwa ya anasa na pia akiangalia upande wa wananchi jinsi wanavyohangaika kutafuta mlo mmoja tu kwa siku. Halafu pembeni anakutana na lundo la watoto wa mitaani mara mbwa mwitu mara panya roads basi anazimia hapo hapo na kufariki tena. Tanzania! Tanzania nchi yangu nakupenda sana.
 
Magamba yanaruka na kukanyagana mwaka huu Chama Cha Mafisi wanalo kila sehemu everything is tight.
 
Kwa hakika mkuu! Itazame nchi ya Marekani, Uchaguzi wao ni wa 2017, Vyama vikuu vyote vimeshaweka wagombea wao wazi. Na mimi nataka kuamini Inawezekana CCM wanategea kujua kua upinzani watammeka nani awe mgombea.Kama ni hivyo basi wamekwisha.

Wakuu mi nawashangaa mnaizungumzia ccm kama vile bado ipo hai wakati ccm sasa hivi ni maiti tayari.
 
Hapa CCM wanatafuta namna ya kuchomoka. Wanatamani kura ya maoni ya katiba izibe uchaguzi mkuu, lakini sasa kura ya maoni haipo ki-katiba wakati katiba inaelekeza wazi kuwa uchaguzi mkuu ni October. Wanatamani kura ya maoni ivuruge utaratibuwa uchaguzi hasa kutumia kipindi cha mpito endapo kura ya maoni itakuwepo na katiba kupitishwa. Ni yamoto kumeza na tamu kutema!

Mmakonde alisema NJOMBA HUCHITEME WAALA HUCHI MEJE CHACHOOTE NJOOMBA.ndio hali ya ccm sasa yamewakaa kooni.
 
Mkakati umeshaandaliwa wa kutompitisha Membe na Lowasa kugombea uraisi anguko liko pale pale.

Duwa zetu wasimpitishe lowasa tuone mahinterahamwe yanavyo sambaratika
 
Anyway,Mwenyekiti aliwatahadharisha wana ccm kuwa wajiandae kisaikolojia.
Naami wamelifanyia kazi agizo la Mwenyekiti,mda ndio huo umefika.

Mkuu ccm luwala hawakubali hilo wenyewe bado wanajidanganya kuwa ccm yao bado ina nguvu kama miaka 10 iliyopita
 
Back
Top Bottom