Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,506
Rafa Benitez wakati anafundisha Liverpool mbona alikuwa anapendwa ingawa alikuwa ni Mspanish,hizo media hazikuwepo?
Mkuu, hivi unazifahamu media za Waingereza kwa undani zilivyo au na wewe ni mmoja kati ya wale ambao wameisha uvaa mkenge wa hizi media.
Hivi huwa unafuatilia Press conference za ijumaa au talk sport radio kabla ya mechi za jumamosi kuelewa kwa undani kilichoko nyuma ya media nyingi za hapa kwa kila Manager.
Nimekwambia sumu aliyoinywa Benitez ni kuzi accuse media kama zinakuwa bias (kitu ambacho ni kweli) huku akitoa mfano wa Sir Alex Furguson.
Unakumbuka uhasama wa Benitez na Mourinho (Liverpool Vs Chelsea ) hasa baada ya Liverpool kuwatoa Chelsea kwenye Champs League baada ya goli la utata la Luis Garcia ambalo Mourinho alisema sio halali.
Ugomvi wa SAF na Benitez haujaanza leo ulikuwepo tangu kipindi Benitez akiwa Liverpool tena bora hata sasa hivi haujaonekana,unataka kutuambia Liverpool walimfukuza sababu ya ugomvi wake na SAF?
Media za Uingereza huwa zinatafuta kwanza mahari pa kuanzia ndiyo maana kwa mtu asiyezifahamu anaweza usijue picha nzima ikoje. This people are cunning na kwa kufanya hivi, huwa wanawaokota wapenzi au washabiki wengi sana.
Kama wachezaji wanaohama timu moja kwenda nyingine wanazomewa(ACole,Nasri,Parker,Tores),unategemea kwa makocha ndio itakuwa kinyume? David Moyes akihamia Liverpool mashabiki wa Everton hawatamzomea?
Kweli wewe huelewi. Ngoja nikupe mfano hai wa media za waingereza zinavyosaidia Manager ambaye ni Mwingereza. Kama una kumbukumbu, mwaka 2004 Harry Redknapp alihama kutoka Portsmouth kwenda Southampton timu ambayo ni wapinzani wakubwa. Washabiki na wapenzi wa Portsmouth waliamua kumzomea kila mechi na wengine wakatengeneza placard lakini kwa vile media zinampenda, Media nyingi za Kiingereza zilianza kuwalaaumu hao mashabiki na wapenzi kwa kitendo chao cha kumuita Harry majina kama Judas, Scummer and Rot in hell. watu walikuwa discouraged na media kufanya hivyo, matokeo yake kelele hizo zikawa hazina nguvu yoyote ile. Hizi ndizo media za Waingereza.
Huwezi kusikia media zinawasimanga watu wanaomzomea Benitez, badala yake zinachagiza vitendo vyao. Hii ndiyo tofauti ya media za hapa UK.