Wong Fei
JF-Expert Member
- Apr 13, 2016
- 4,818
- 6,464
Mama hongera na pole kwa majukumu ya kila siku ya kujenga taifa. Zoezi lako la uhakiki ni zuri na lina manufaa ya kulijenga Taifa kwa ujumla na kuimairisha hali ya uaminifu kwa watanzania (hakuna kufoji vyeti. Jasho lako ndiyo ukombozi wako).
Pindi zoezi lako la uhakiki limeanza lilishangiliwa na kuungwa mkono na watanzania wote lakini sasa zoezi la uhakika wa wafanyakazi hewa limegeuka mzigo, msiba na mwiba kwa watanzania na kuwafanya Vijana kutojua hatima yao katika nchi ya ma babu na ma bibi zao waliopigania uhuru ili Taifa la Tanzania lipate kuwa huru kutoka kwa wakoloni.
Zoezi lako limekwamisha ajira mpya, uhamisho wa wafanyakazi, kupandishwa madaraja na nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi na hauna habari kabisa na zoezi lako na umeshasahau kabisa kuwa unaongoza watanzania na siyo mawe. HAKUNA SERIKALI YOYOTE DUNIANI NA PIA HAKUNA SERIKALI YOYOTE DUNIANI ISIYOAJIRI WATU WAKE. HIZO AJIRA ZA WALIMU, MANESI NA WENGINE NDIYO TUNAZILILIA. HATA NYIE MLIPITIA HUKO HUKO MPAKA MKAFIKA KUWA MAWAZIRI
Vijana wamekata tamaa ya maisha kabisa na wimbo wa kuajiri umekuwa mgumu kwao kwa sababu mazingira ya kujiajiri ni magumu, mikopo inatolewa kwa mashariti magumu na riba kubwa sasa huyu mtoto wa maskini hataweza saa ngapi?
Mnaposimama majukwaani vijana wajiajiri lakini nyie meshindwa kuwa mifano bora ya hawa vijana kujiajiri mnakosea sana. Mfano Kingwangala alipomaliza elimu yake ya juu, akakimbilia kuajiriwa mpaka wa leo yupo serikali na sidhani kama hata akifukuzwa kazi leo hatajiajiri ameshindwa uwezo na Dr. Ndondi amebaki kuwa msemaji. Kitu kinachowasumbua vijana wengi ni mitaji kwa hiyo mnapopiga debe wajiajiri wakati mazingira ni magumu ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.
Hii nchi ni ya kwetu sote na hakuna mtu mwenye hati miliki ya hii nchi na pia hakuna mtu aliyejuu ya sheria. Mama unaongoza kwa ajiri ya manufaa ya watanzania na si mawe sasa kama umeshindwa kushughulikia matatizo ya watanzania inabidi ujiuzuru. Haiwezekani watu wataabike mitaani wakati wewe kila mwezi unapokea mshahara na posho na umeshindwa kuwajali watoto wa masikini ni kosa kubwa sana na inabidi ushughulikiwe kwa kuchezea maisha ya watu.
KAMA MNAONA KAZI SANA KUAJIRI WATOTO WA MASIKINI, IANZISHWE SERA YA WATU KUPATA MITAJI, KAMA WEWE UMEFANYA KAZI MIAKA 7 SERIKALI UTOKE KWA SABABU UMESHAPATA MTAJI UKAJIAJIRI UACHIE WENGINE NAO WAKIFIKISHA MIAKA 7 WATATOKA WATAACHIA WENGINE. HAPO TUTASONGA MBELE
(mambo yote kwa sasa meingiza siasa na mnafanya kisiasa hata watu waliokuwa hawana mpango na siasa nao wameingia kwenye siasa. ILA MKUMBUKE WALE WATU MLIOKUWA MNAWAONGOZA MIAKA 1947 SIYO WA LEO 2017)