Angekuwa wewe ungefanyaje?

Angekuwa wewe ungefanyaje?

Nina rafiki yangu ambaye tumeshibana saana kwa kauli nyingine sio rafiki tena ni ndugu kabisa.

Huyo rafiki yangu baba yake ni mgonjwa saana anaumwa sana. Tulikwenda naye hospitali wakasema anahitaji kufanyiwa upasuaji tumboni mwake na hili afanyewe hivo kuna pesa fulani ambazo wanaomba hili apate kutibiwa.

Sasa kuna pesa ambazo nilipewa na familia yangu baada ya dada zangu kuolewa wazazi wakaona zile pesa tufanye nazo biashara wakanipa mimi kama mtoto wao wa kiume. Na kwenye plan yangu ya biashara nilikuwa nipo na huyu ndugu yangu (rafiki) tulikuwa tuna panga wote.

Sasa baada ya baba yake kuumwa hizo pesa anaomba eti ni msaidie hili amtibishe baba yake najaribu kumwambia nitampa nusu kwa bahati mbaya nusu nyingine hana kwa hiyo anaomba pesa zangu eti Mungu atanilipa utu wa mtu ni muhimu kuliko pesa. Na kweli mzee wake ni mgonjwa saana na asipo tibiwa mapema ni Mungu tu

Mimi na shindwa na la kufanya kabisa
Yaani sijui nikimpa wazazi nitawapa taarifa gani au nitapata wapi tena pesa zingine. Nahisi na changanikiwa kabisa

Naona sina bahati kabisa.

Sijui naombeni ushauri

Kwanza pesa si yako. Naye anafahamu hilo. Mweleze muende kwa wazazi na ndugu waliokupa huo mtaji watoe uamuzi. Hii itakuepusha na lawama kwake na waliokukabidhi huo mtaji. PESA SI ZAKO.
 
Ukimpa hela rafiki yako urafiki umeisha, na usipo mpa hela urafiki umeisha. Uchaguzi ni wako ufanyie biashara au umpe rafiki yako awe adui yako. Rafiki yako ana familia yake wakae kitako watatuwe shida zao sio wewe ubebe shida zao. Kwani wao wamewahi kukusaidia nini??
Dah mzee umezungumza kitu cha maana ila watu hawatakuelewa ,maisha haya kila kitu fanya kwa kiasi ,usifanye jambo ukapitiliza mpaka ukajinyima kila kitu kwa ajili ya mtu mwingine ambaye hatokuja jinyima kwa ajili yako ,utaumia sana mbeleni huko ,binaadamu sio wa kuwaaamini kabisaaaa
 
Kama hyo pesa ni kubwa huwezi kuipata wewe kama wewe kwa haraka kweny hustling zako usimpe..Tambua ana ndugu kibao mgaiye kidogo ,urafiki unakufa pia ..

Mfano kama pesa ni million 10 mpe hata million 1 au mbili usitoe pesa ndefu...huyo mzee ana mtoto mmoja pekee? baadhi ya marafiki haswa wabinafsi ni wajanja sana .

Marafiki huwa wabinafs mno tena wakikuona una roho nzuri Ndio wanatake advantage
 
Marafiki huwa wabinafs mno tena wakikuona una roho nzuri Ndio wanatake advantage
Watu wabinafsi haswa marafiki utawagundua kupeleka shida zake mbele kweny upande wake haswa kweny ishu za pamoja ..Kama hapo alitakiwa kujua kwamba ishu ya mzee wake ni yake private sio kuileta kwa rafiki yake
 
Mkuu kwanza futa neno rafiki kabisa, ili neno rafiki limeniponza mpaka leo sio chini ya ml 30 zimepotea kwenye mikono ya marafiki alafu hakuna nilichovuna zaidi ya unafiki, nilichoamua mpk sasa mm sina neno rafiki maishani mwangu alafu hao niliokuwa nawaita marafiki nilishawaambia hata nisikie yeye au ndugu yake yoyote anakufa sitatoa msaada hata kwangu mm nimewaambia sitaki msaada wao, huyo unayemwita rafiki sasa mpe hiyo hela utakuja kusimulia hapa tena atachokulipa baada ya kumpa hiyo hela, kama wadau wanavyosema hapo juu kupanga ni kuchagua mpe urafiki ufe au usimpe urafiki ufe, ila mm ningechagua kutokumpa wacha urafiki ufe nina experience mbaya sana na hawa watu tunaowaita marafiki.
 
Eti rafiki..urafiki unakufa.
Kama hizo pesa zisingekuwepo angefanyeje?
Pesa si zako kwanini umpe?
Kwani ni lazima ulipie urafiki wenu?
 
Mwambie rafiki yako kwamba huna sauti ya mwisho juu ya hzo pesa mpka ushirikishe Wazazi wako

Then rudi nyumban kwa wazee wako ongea nao swal litakuja why umemwambia una pesa utajua jinsi ya kujitetea then baada ya hapo sikilza maamuz yao

Wakikupa ruhusa ya kias gan umpe toa wasipokupa usitoe kamwambie ukwel Rafiki yako ili ajue kwamba ni nje ya.uwezo wako.
 
Kama huyo rafiki ni kama ndugu kama ulivyosema itakuwa hadi kwenu wanamfaham, itakuwa vyema kuongea na familia yako uone wanasemaje ila usijichukulie maamuzi wewe kama wewe maana baadae utakuja kujutia mambo yakibadilika sababu hela zinavunja sana urafiki hata undugu
 
Tutegemee nyuzi za majuto toka kwa mleta uzi.
Jamaa hakutakiwa kuigusia pesa yako, angekushirikisha hali ya mzee then wewe ndo ujichekeche.

Hiyo ya kusema mwanangu si una ile hela basi naiomba( aisee hiko ni kosa).

Washirikishe ndgu zako hilo tatizo, ukimpa bila kuwashirikisha. Yakitokea ya kutokea huenda ukakosa utetezi mkuu.
 
Back
Top Bottom