Ang'atwa na COBRA ndani ya ndege

Bujibuji Simba Nyanaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
61,745
2,000
NI ajabu na kweli kwamba abiria mmoja katika ndege ya Shirika la Ndege la Misri aling'atwa na nyoka aina ya Cobra akiwa ndani ya ndege.

Hali hiyo ikailazimu ndege hiyo kutua kwa dharua baada ya mwendesha ndege huyo kusikia kelele na hofu ya kuumwa na nyoka kama lilivyoripoti gazeti moja huko Jordan.
Ilikuwaje hadi abiria kwenye ndege kung'atwa na nyoka ?

Sikiliza ni kwamba abiria huyo Akram Latif alikuwa akimdhibiti nyoka wake baada ya kuporochoka ndani ya mfuko alikokuwa amemhifadhi.
Nyoka mfukoni akaona hapati hewa akatoka ndani ya mfuko na kuanza kuzuru ndani ya ndege kama mhudumu vile huku akipanda kwenye viti vya abiria.
Mmiliki wake kuona hivyo ndipo akahaha namna ya kumdhibiti ili asiendelee kuleta kizaazaa kwa abiria. Unadhani ndani ya ndege kulitokea nini? Umekaa mara unaambiwa nyoka huyo ukweli ni kwamba ilikuwa ni kizaazaa na hakuna abiria hata mmoja aliyekalia kiti chake.
Kuona hivyo mshika chombo akalazimika kutua kwenye mji mmoja huko huko Misri ili kunusuru abiria na kumpeleka mmiliki wa nyoka huyo hospitalini. Jamaa anatoa nyoka Misri kumpeleka Kuwait.

Nadhani huko Uarabuni kuna upungufu wa nyoka ndio maana mtu anasafiri na nyoka kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine. Mtu anafuga nyoka, wa nini jamani?
Kumbe sie huku bongo tunahangaika namna ya kuwaangamiza nyoka wenzetu wanafuga sijui na wao wanacheza ngoma za asili. Maana tumezoea kuona wachezaji wa Kibisa ndio wanabeba nyoka lakini nyoka mwenyewe wanayebebwa ni chatu sio Cobra.

Si mnaujua ukali wa Cobra, lakini wapi bwana mwarabu kabeba. Mwarabu kabeba lakini nyoka hana urafiki, lini shetani akawa na urafiki wakati kazi yake ni kudhuru watu.
Ndio maana nyoka akaamua kumng'ata bwana wake baada ya kuona anamghasi. Ilikuwaje mtu anapita na nyoka hadi kweye ndege? Hili nalo swali la kujiuliza. Kumbe pamoja na wenzetu kuwa mbele kimaendeleo lakini bado hawana vifaa vya kung'amua wanyama hatari kama nyoka wanaosafirishwa.
Abiria 90 wakawa na hofu, wakatua uwanjani na aliyeumwa na nyoka akapelekwa hospitalini kwa matibabu huku nyoka aliyemng'ata bwana wake akichukuliwa na maofisa wa uwanja wa ndege.
Sasa sikiliza, baada ya kizaazaa hicho waliokuwemo ndani ya ndege hiyo ililazimika wapekuliwe tena ili waendelee na safari eti ili kuona kama kulikuwa na nyoka wengine kwenye mifuko ya abiria.

Ehe kumbe Latif bwana sio mganga wa kienyeji ni mmiliki wa duka kubwa la nyoka huko Kuwait hivyo alienda Misri kusaka nyoka na akawa ameambulia mmoja tu ambaye naye alimng'ata mkononi.
Alivyopewa huduma ya kwanza na kushauriwa na madaktari akae walau saa 24 kwenye hospitali jamaa akagoma, akadai kwanza apewe nyoka wake ili aendelee na safari ya kwenda nchini mwake Kuwait.

Pamoja na madaktari kumshauri abaki hospitali aligoma, akarudishiwa nyoka wake na akaendelea na safari yake kwenda Kuwait.
Wadau kama una nyoka, soko hilo huko Kuwait. Kama unaweza kwenye misitu yetu huko Pugu, Tabora, Katavi na kwingineko kulikojaa nyoka, kuna soko la uhakika huko Kuwait jamani.
Wabongo changamkieni fursa hiyo ya biashara, tusikalie kulalamika tu ohoo hakuna fursa wakati tumeshafunguliwa soko la nyoka Kuwait. Kazi kwenu wadau.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom