Angalizo: Waziri Mwakyembe atadumaza michezo nchini

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,687
239,245
Uteuzi wa Dr Mwakyembe kwenye wizara ya michezo , hii wizara inayohitaji sana ushirikiano wa wadau mbali mbali ili kuchangia na kusukuma gurudumu la michezo mbele haukuwa sahihi.

Uchunguzi wangu umebaini kwamba wizara ya michezo inahitaji uteuzi wa kimkakati , anahitajika waziri mwenye uwezo wa kuvutia wadau na matajiri kuchangia michezo nchini , huyu wa sasa hana uwezo huo .

Mwakyembe ni kati ya mawaziri wa awamu ya tano wanaochukiwa na karibu wananchi wote wakiwemo wanamichezo kutokana na " mambo yake ya kisiasa ", hivyo kumweka mtu wa namna hii kwenye wizara ya michezo , wizara ambayo ili ifanikiwe ni lazima wadau wajitolee , ni sawa na kuzika michezo nchini.

Kwa mfano , zipo taarifa kwamba hata kudorora kwa harambee ya kuchangia Serengeti Boys iliyorushwa na TBC kulisababishwa na Mahusiano mabovu ya Mh Waziri na jamii inayomzunguka .

Naomba wadau tusihusishe andiko hili na siasa za upinzani , bali tujikite kuangalia kilichoandikwa kwa ajili ya maendeleo ya michezo nchini .
 
Ndio shida ya kuwapa watu wasio na weledi wizara husika..Hii wizara sijui kama anaimudu
 
Mapema sana kufaham kama hawezi kumudu au la. Harambe ndogo iliyopatikana yawezekana ikawa ni uchumi mbaya wa mtu na mtu, makampuni na sio mahusiano mabaya na wananchi pamoja na wafadhili au wadhamini
 
Mapema sana kufaham kama hawezi kumudu au la. Harambe ndogo iliyopatikana yawezekana ikawa ni uchumi mbaya wa mtu na mtu, makampuni na sio mahusiano mabaya na wananchi pamoja na wafadhili au wadhamini
Kumtetea Mwakyembe si rahisi kama unavyodhani .
 
Back
Top Bottom