ANGALIZO:Matapeli watoa vyeo ‘feki’ kwa walimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ANGALIZO:Matapeli watoa vyeo ‘feki’ kwa walimu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 20, 2012.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WIMBI la matapeli wanaotumia nyaraka za serikali kwa lengo la kuwapandisha vyeo bandia maofisa elimu kwa ngazi za maofisa vifaa na takwimu na maofisa taaluma limeikumba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi huku kukiwa na siri nzito katika kuwashughulikia walimu waliopandishwa vyeo.Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima tangu mwanzoni mwa mwaka huu umebaini kuwepo kuna wimbi kubwa la utoaji wa vyeo kwa walimu na kuwa maofisa elimu katika halmashauri mbalimbali nchini ambao wamepewa barua zilizosainiwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Hamisi Dihenga.Habari za ndani kutoka kwa maofisa elimu wa mikoa takriban sita ambayo ndiyo iliyofahamika kukumbwa na matukio hayo hawakuwa tayari kuzungumzia undani wa kuwepo kwa barua za kughushi huku kukiwa na habari za walimu waliopandishwa vyeo kukamatwa na kufikishwa polisi wakituhumiwa kwa kosa la kughushi nyaraka za serikali.Mikoa ambayo Tanzania Daima imebaini kuwepo kwa walimu wengi waliopandishwa vyeo na kunaswa ni Morogoro, Lindi, Rukwa, Mbeya, Mwanza na Iringa; na kwamba kundi la matapeli hao wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya watumishi wa wizara, ili kujua halmashauri zenye mapengo kwa nafasi za maofisa elimu vifaa na takwimu na maafisa vifaa taaluma.Baada ya kupewa majina na halmashauri zenye upungufu wa vyeo katika kada hiyo, ndipo kundi hilo huanza kufanya mawasiliano na walimu sehemu mbalimbali nchini na kuwaeleza nia ya kutaka kuwapa vyeo hivyo na kuhitaji kiasi cha fedha kati ya sh milioni 2 hadi 3 na wale waliofanikisha kuingia kwenye mtego huo ndiyo waliopatiwa barua zikionyesha zimetoka Wizara ya Elimu.Ofisa Elimu wa Mkoa mmoja alipohojiwa kuhusu hali hiyo, alikiri kuwa wamefanikiwa kuwanasa walimu waliopandishwa vyeo bandia na kwamba taarifa zao zimekwishatumwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara na majibu waliyapata kuwa wizara haijatoa ajira za namna hiyo na kuagiza kuwa wale wote walionaswa na barua hizo wachukuliwe hatua za kisheria.Ofisa Elimu Mkoa wa Mbeya, Juma Kaponda, alipohojiwa alikiri kuwepo kwa barua hizo ambazo zinaonyesha uteuzi wa maofisa hao na vyeo walivyopatiwa na kwamba ili kuthibitisha uhalali wa barua hizo baada ya kutiliwa mashaka wamerudisha kwa Katibu Mkuu na wanasubiri majibu ya wizara, ili kuona kweli kama wahusika wamepandishwa vyeo hivyo.Mkurugenzi wa jiji la Mbeya, Juma Iddi, ambaye halmashauri hiyo nayo imekumbwa na sakata hilo, alikiri kupokea barua ya uteuzi wa Ofisa Elimu Taaluma kutoka wilaya ya Mbeya Vijijini (jina lake tunalo) aliyepangiwa jijini hapo baada ya mtumishi aliyekuwa na cheo hicho kupandishwa cheo na kuwa Ofisa Elimu Wilaya ya Ileje.Angalizo...wilaya nyingi sana za pembeni mwa tanzania zimepata barua za namna hiyo tena wanawafuata wale waalimu ambao wanajua wamemaliza kusoma Degree,masters na diploma Hii wizara ya Elimu nayo imeshaoza kabisa inabidi uhakiki wa maafisa hawa ufanyike na mambo haya yanatokea hapohapo wizarani.

  source

  Matapeli watoa vyeo ‘feki’ kwa walimu
   
 2. N

  Njangula Senior Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii nayo kali hata elimu jamani? Sasa hata barua yangu ya kuthibitishwa kazini naifuatilia isije ikawa feki.
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mawizara hayana pesa kila mtu anawaza mchongo
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  wizara inaongozwa na waziri ambaye sio effective katika utendaji wake, huyu Kawambwa anafaa kuwekwa benchi hata kama anatoka BWAGAMOYO!!
   
Loading...