Niliwahi kuandika humu jinsi Mzee wa Pembe za Ndovu alivyojipanga kuimaliza CHADEMA nadhani wengi hawakunielewa na ule uzi uliondolewa chapuchapu humu. Mtego mzima umetegwa kwenye uchaguzi. Combination ya Mbowe na Dr Slaa inawatesa sana MAGAMBA wameapa kuwa CHADEMA isifike ikiwa kama ilivyo mwishoni mwa mwaka 2014 kwa kuwa wanasema kuwa ikifika hivi ilivyo hali yao itakuwa mbaya sana. Mchezo unaochezwa sasa hivi ni uchaguzi wa CHADEMA ulazimishwe ufanyike wanavyotaka wao. Mtu wao ndani ya CHADEMA pamoja na kusema hata gombea wanamshinikiza kweli kweli agombee wapate pa kupenyeza mgogozo. Baadhi ya waandishi na magazeti maarufu yameshapokea tenda kutoka kwa mzee wa pembe za faru. Hivyo muhimu CHADEMA ikafanya maamuzi ya ikajiandaa vilivyo na njama hiyo kabla ya kwenda kwenye uchaguzi. Nilisema mwanzoni kabisa kuhusu hili mara nilipolipata kutoka chanzo changu muhimu cha Lumumba nadhani sikueleweka, sasa mmemsikia Nape wenyewe. Inauma sana upinzani uliopo kuuwawa hivi hivi kwa maslahi ya kikundi kidogo kinachojiona chenyewe ndio kinastahili kuongoza tuseme hapana. Taifa letu ili lipige hatua lazima kuwe na tabia ya kubadilishana uongozi kutoka kwa walishindwa kuongoza kwenda kwa wengine.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI TANZANIA