Jana nikawa naipitia Bible, nikakutana na kipengele kinachozungumzia siku ya mwisho, kwamba siku hiyo kila kitu kitafunuliwa, mambo yote tunayofanya kwa siri siku hiyo yatakuwa wazi.
Mawazo yakakimbilia JF katika jukwaa hili, kuna watu wanafanya mambo kwa kudhani hawatajulikana, watu wengine mtu ungewaona ungeshangaa, huenda hata watu wakubwa wenye heshima zao wanayafanya haya, wanaweka uongo, mtu anaanzisha topic eti nina mzigo wa unatingishika.
Siku anajulikana unakuta hata siyo mwanamke na ni kimbao mbao tu. Je mnajua ipo siku isiyo na jina?