Mbelwa Germano
JF-Expert Member
- May 7, 2011
- 789
- 289
Hilo darasa la tuition wafundishe familia yako, imeshindikana deal na mkeo na wanako. Mabadiriko gani unayoyataka yafanyike ndani ya chadema wewe? Wanafiki kujificha ni vigumu sana, gamba kuu wewe. Tuache tuendelee na mapambano ya kuchukua nchi 2015. Peoples power, M4C.
Kwasasa mm sijui cha mabadiliko ya kimuundo, sujui uchafu gani, sijui nn....nachoelewa sasa hivi ni M4C only...
"swala langu hapa ni udhaifu wa baraza la wanawake chadema (bawacha) sijui wanafaida gani ndani ya chadema au ni kwa ajili ya ubunge wa viti maalumu hili ni lazima uongozi wa c.d.m ulifanyie kazi au kuuondoa uongozi wote kwa maslah mapana ya chadema bila kuangaliana usoni kwani wapigakura wengi wa tanzania ni wanawake.
tunahitaji bawacha isimame kama baraza ndani ya c.d.m lifanye kazi ya kuwaunganisha wanawake wawe na mwamko wa kuiunga mkono cdm.mwanamke akiwezeshwa anaweza viongozi chadema liangalieni hili kwa maslah ya chama". Na Mayage
Ndugu zangu wale wasioona haja ya mabadiliko hili ni moja ya mabadiliko ninayozungumzia. Kamwe tusibweteke...
Sasa ulishindwa nn kuwa straight kuanzia mwanzo wa thread yako....Mara oh Zitto, Mbowe sijui Dr. Slaa...
Mkuu wangu nakusoma vizuri sana na hakika umenigusa sana. Kuna kirusi kimeingia ndani ya chama ambacho kinaitwa UMAARUFU wa MUDA na kwa bahati mbaya umekuwa mtaji mkubwa kwa baadhi viongozi na wanachama wa Chadema. Hili huhitaji kulitazama upande mmoja ukiwa ndani isipokuwa kujitoa pembeni ukalitazama kwa makini ili upate kuona athari zake..Kama kuna jambo kubwa ambalo Watanzania wengi limewaathiri kifikra ni utawala wa CCM. Monopolization chini ya CCM imewafanya watu wengi ndani ya Taifa hili kuwa na fikra tegemezi, kukosa muda wa kutafakari mara mbili, kuwa wepesi wa kuhukumu na kukubali kuishi kwa mazoea.
Jambo hili bado limewaathiri hata wana-mageuzi nchini, wana-CHADEMA, baadhi ya wana-CDM wamekuwa wepesi kutekwa fikra zao, wepesi kuhukumu na kukubali kurudi kule ambako NCCR ya Mrema ilipotea.
Wanafikiri kuwa na fikra na mitazamo tofauti ndani ya chama ni chanzo cha vurugu na misuguano. Wameshindwa kutafsiri maana halisi ya migogoro na kuhisi kwamba wako mstari wa mbele kuepusha migogoro na kusahau kwamba wanajenga migogoro, wamelewa na mafanikio ya ghafla.
Wengi wanahisi kwamba wanaweza kuishi na kudumu nje ya demokrasia bila kuweka utaratibu wa kidemokrasia. Wamekataa kuishi kwa kudadisi bali wamekubali kuishi kwa kuhisi. Wamekataa kupima afya ya fikra zao na kutumia propaganda na maneno rahisi kuhalalisha agenda zao.Hatuwezi kamwe kufika kwa mtindo huu.
Lazima kwanza wajifunze kuwekeza kwenye siasa za akili na maarifa na hivi ndivyo chama chenye demokrasia pevu hufanya. Ukikataa njia ya majadiliano chini ya hoja kinzani ni kuhalalisha udhaifu na uwezo mdogo wa kifikra.
Zipo tofauti kubwa za kimtazamo na kifikra kati ya Mbowe, Dr.Slaa na Zitto lakini tofauti hizi haziwezi kuwa na athari iwapo zinafuata misingi na kanuni za chama. Leo ukiongelea kuhusu Zitto watasema umetumwa, ukitoa mapendekezo Dr. Slaa agombee uenyekiti wa chama watasema umetumwa, je nani ambaye atazungumza kuhusu Zitto na watasema hajatumwa.
Zitto ni Naibu Katibu Mkuu wa chama, nilitegemea wakati wa matukio makubwa ya chama Mwenyekiti wa chama angewaeleza wana-mageuzi kwa nini Zitto hayupo lakini hili halifanyiki. Ni wangapi waliwahi kuhoji ni kwa nini? Au tumeridhika na jibu rahisi ni MSALITI. Rejea NCCR ya Mrema na tafakari tafsiri halisi ya mgogoro. Hili ni tatizo. Na tatizo lipo ndani ya chama. Kama tumekataa hoja na na fikra kinzani kama moja ya kanuni za kidemokrasia basi tusitarajie kuishi kwa muda mrefu ndani ya ulingo wa siasa za kiushindani.
Kamwe wana-CDM tusibweteke na mafanikio ya sasa, bado tuna kazi kubwa ya kujenga chama. Mabadiliko ndani ya chama ni Muhimu.
Na wala sioni sababu kabisa ya Mwenyekiti kusimama na kuwaelezea wana mageuzi kwa nini Zitto hakufika ikiwa Zitto hakuwa mgeni rasmi ama alotarajiwa kuendesha matukio hayo.
Lakini kwa nini watu wajiulize hivyo ikiwa hawajajenga fikra mbovu vichwani. Hivi kweli leo JK yupo canada kuna mtu anataka kujua Mukama, Pinda au Msekwa wako wapi?..Kwa nini tunapenda kujiuliza maswali ambayo yanazidi kujenga utenganishi?..Mkuu, ipo mitazamo hasi ambayo inajengeka ndani ya chama ambayo inahitaji ufafanuzi, mara nyingi watu wanahoji ni kwa nini kombinesheni ya Zitto na viongozi wengine wa juu wa chama haionekani? Kila chama kina itifaki ambayo hutoa itiririko wa nafasi katika chama,hivyo tuna changamoto ya kujenga kombinesheni imara without individualism ambayo itaonyesha tunasimamia itikadi na sera moja na tunasimamia kwa pamoja mabadiliko na kubeba jukumu la kuyatafsiri mabadiliko yenyewe.
Wakati wa M4C ya mara ya mwisho Jangwani wengi waliuliza Zitto yuko wapi. Lakini kulikuwa na tetesi yupo Marekani akifungua matawi ya chama, kulikuwa na kosa gani kutambua jukumu ambalo ni kwa manufaa ya chama. Tukumbuke huyu ni NAIBU KATIBU MKUU WA CHAMA.
"swala langu hapa ni udhaifu wa baraza la wanawake chadema (bawacha) sijui wanafaida gani ndani ya chadema au ni kwa ajili ya ubunge wa viti maalumu hili ni lazima uongozi wa c.d.m ulifanyie kazi au kuuondoa uongozi wote kwa maslah mapana ya chadema bila kuangaliana usoni kwani wapigakura wengi wa tanzania ni wanawake.
tunahitaji bawacha isimame kama baraza ndani ya c.d.m lifanye kazi ya kuwaunganisha wanawake wawe na mwamko wa kuiunga mkono cdm.mwanamke akiwezeshwa anaweza viongozi chadema liangalieni hili kwa maslah ya chama". Na Mayage
Ndugu zangu wale wasioona haja ya mabadiliko hili ni moja ya mabadiliko ninayozungumzia. Kamwe tusibweteke...