Angalizo kwa Dr. Slaa na Edward Lowassa!

Angalizo kwa Dr. Slaa na Edward Lowassa!

KING COBRA

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2011
Posts
2,782
Reaction score
876
ANGALIZO KWA DR SLAA NA LOWASA
Kabla sijaanza kuelezea lolote napenda kumukumbusha Slaa ambaye ana taaluma ya upadri.
Katika kitabu cha matendo ya Mitume kuna ushahidi kwa Sauli alikuwa muuaji na tena alikuwa anauwa mitume lakini alipata badiliko la kweli na kujiunga na mitume wengine.

Wakati Sauli anafanya hivyo Mitume wengine walianza kumunyanyapaa na kumuogopa lakini katika bibilia , imethibitishwa kwamba hadi leo Paulo (aliyekuwa Sauli) ndiye aliyefanya kazi kuliko Mitume wote.

Bila shaka kuna watu ndani ya CHADEMA na hata nje ya
CHADEMA wanataka kujenga hoja ya kumunyanyapa LOWASSA ati ni Fisadi , hata mimi niliingia mtego huu lakini napenda kuhojhi yafuatayo:

(1)Lowassa amehama CCM na kwa hatua hiyo ameingamiza nafsi yake kwa kiwango Kikubwa.

(2)Lowassa yupo tayari kutumia Pesa yake na mali yake kubomoa CCM

(3)LOWASSA ana hasira kali na CCM na miungu watu ndani ya CCM

(4)LOWASSA kama waziri Mkuu mstaafu ametake risk ya Kifo kiasi kwamba anataka kupiga CCM kwa Nyaraka zito za Siri ambazo Slaa hawezi kuzielezea

(5) Lowassa anajua mikakati ya Wizi wa Kura ndani ya CCM kwa miaka zaidi ya 40

(6) Ndani ya CCM hawakutarajia wala hawakuwahi kupanga kuwa mtu kama Lowassa ambaye ameshika nafasi nyeti kama waziri mkuu anaweza kuasi serikali kiasi hiki.Huu uasi unatisha na haujawahi kutokea, na hata pale ulipojaribu kutokea wahusika hawakubaki hai

(7)Kwa sasa CCM wanahaha sana juu ya Lowassa kuchukua form. Mikakati ya CCM iliielekeza Nguvu kumshambulia Slaa lakini Mungu amebadili Plan ghafla na kumuleta Lowassa ambaye hawajajipanga na ni Pigo kubwa

(8)Kwa sasa Uasi uliojitokeza CCM ni vigumu kujua nani yupo kwa nani.Angalia mtandao wa Lowasa ndani ya CCM unatisha na umetulia Kimia.Mtandao huu jumlisha nguvu ya Umma ni lazima CCM ibaki kama KANU

MAONI KWA SLAA.
(1)Wakati unagombea urais ulikuwa na Rozi Kamili ukamwacha na kumuoa Josephine,
Rozi Kamili alikubali ujio wa Josephine lakini leo Josephine huyo amekuwa kikwazo kwa maamuzi yako.

(2)Mambo ya Chama huwezi kumuhusisha Mwanamke, huo ni udhaifu mkubwa na kama kweli unamsikiliza mwanamke basi ujue hutapata nafsi ya kurudi kwenye jamii na wakakuamini na kukupa heshima kama walivyokupa.
Mke ni mshauri wake kwa mambo yote lakini kikao kama kamati kuu kinapopitisha maamuzi harafu mkeo anapinga maana yake mke huyo hafai kuwa First Lady na hata wewe hufai kuwa Kiongozi

(3)Slaa aliwahi kusema kuwa anapata Nyaraka kwa watu wa Tiss , sasa angalia Mkurungezi wa zamani Tiss Apson ameonekana kwa Lowassa, Kingunge ambaye hajawahi kukaa na Slaa amejitokeza kwa Lowassa , akina Emmanuel Nchimbi na Sophia Simba ambao ni watu wa ndani serikalini na wameshiriki kukuibia wewe Slaa kura wamejitokeza Nyuma ya Lowassa na wala hawawezi kujitokeza kwako. Je, wewe huna akili ya kuona haya?

(4) Lowassa hadi leo ana ulinzi wa Ikulu ambao hauwezi kuhujumiwa , wewe Slaa juzi tu mlinzi wako amenunuliwa.
Lowassa hawezi kupewa nyaraka feki toka ikulu kwa kuwa kuna akina Apson , je wewe una nani zaidi ya Mkeo ambaye umempora kutoka kwa watu wa CCM?

Nina hasira na wewe Slaa pamoja na mkeo toka haraka huko uje huku Mungu anakuita kwa mara ya mwisho umuunge Lowassa katika urais vinginevyo utapotea Kisiasa bado wiki moja tu utapoteza mwelekeo

MAONI KWA LOWASSA
(1)Umeitwa Mwizi kwa siku nyingi sana na hata mimi nimekuita hivyo , sasa huu ni wakati wa wewe kutuambia mwizi halisi ni nani na utoe Ushahidi

(2) Zipo taarifa kwamba CCM wanapanga kukata jina lako kwenye tume ya uchaguzi hivyo nakusihii usikate tama.Muombe Mungu .Hii ni safari ya ushindi na si matumaini tena

(3)Usiogope kushambulia Ikulu kwa kuwa Mussa alikaa Ikulu ya Farao na kulelewa hapo lakini Mungu alimpa kazi ya kumuangamiza Farao.
Hivyo Lowassa umepewa kazi ya Kuingamiza CCM hivyo fanya kweli ujue kwamba Slaa hajui haya.

(4)Kama Lowassa ni mwizi na dhaifu kisiasa kwanini CCM wanahangaika baada ya Lowassa kuchukua form??

(5)Kama Lowassa ni mgonjwa , Kwanini CCM wananahaha baada ya Lowassa kuchukua form? Je, wanamuogopa mgonjwa??

HOJA DHAIFU KWA CCM

(1)CCM walisema Lowassa ni Mwizi na anatakiwa kujivua Gamba sasa Lowassa ameondoka kwanini munahofu???

(2)Kama Lowassa ni mwizi Kama wanavyoamini CCM basi nawashauri CCM wasihangaike na jina la Lowassa kwenye tume ya Uchaguzi , waliache harafu wapime nguvu ya Lowassa na Mangufili!!
Kikwete alisema Chama si mtu sasa uje umnadi Magufuli wakati anapambana na Lowassa!!

(3)Nawaomba CCM waje na ushahidi kwenye majukwaa ya Siasa kuonesha kuwa Lowassa ni fisadi, wasikimbilie kwenye kamati ya maadili na NEC.Wakifanya hivyo basi wananchi watachambua pumba na mchele.

 
Ni wakati muafaka wa Lowasa kutoa Maelezo yaliyojitosheleza kuhusu muhusika mkuu wa Richmond

Mungu ibariki Tanzania
 
moja ya hoja nzuri nilizowahi kuzisoma JF,na yeyote mwenye kusoma na kuelewa atakuelewa, hongera sana ndg kwa kutulia na kuandika ujumbe ulijaa ukweli. mimi nasema kama wapinzani watashindwa kuelewana na wakakubali kuvuruga movement yao ya pamoja, na ikawapelekea kutofikia yale waliyoyatarajia kwa pamoja, basi nitaamini viongozi wetu wengi ni mamluki na hawapo kwa ajili ya mageuzi, na hawako kwa ajili ya waliokandamizwa na mfumo, na itawachukuwa zaidi ya miaka 100 kuuondoa utawala wa mkoloni wa kijani.
 
Mkuu king cobra hili ni jiwe la maana sana sasa nimetoka njia panda maana hawa watu wawili walinieka njia panda nisielewe nikae upande gani..asante kwa uzi mtamu..viva ukawa!!
 
I like this explanation to the our leaders and their fellows.
 
BIG UP KING COBRA!!!! Hats off to you! Kama Slaa ana masikio asikie maneno haya! Kupanda mnazi ni kazi kubwa na huchukua muda mrefu, lakini kushuka ni dakika moja. Vivyo hivyo, kujenga heshima katika jamii ni kazi ngumu inayochukua muda mrefu, lakini heshima hiyo inaweza kuporomoka kwa dakika moja tu! Yeyote atakayeshindana na wimbi hili la mabadiliko, kwa kujiona yeye ndiye mtakatifu sana kuliko Lowassa, heshima yake itaporomoka kwa dakika moja tu!!!! Huu siyo Uchaguzi wa kumtafuta "Baba Mtakatifu", ni Uchaguzi wa mtu mwenye uwezo wa kuitoa CCM madarakani, hata kama mtu huyo ni mwenye dhambi kiasi gani! After all, Slaa ana utakatifu gani, mtu aliyemwacha mkewe na kumwoa mke wa Mahimbo, aliyejikoboa ngozi mpaka mishipa ya damu inaonekana??????
 
Well said. Hongera uzi umetulia,, Dr. Slaa upitie huu uzi uone faida ya ujio wa Lowasa kwa chadema
 
Nimejikuta nimesoma yote nikaanza kumind eti uzi umeisha,hongera kwa angalizo mahususi
 
Wanaopiga porojo wameshapewa fedha za rushwa na Mwizi mithili ya Escoba. Hata akili zao zimenunuliwa na jamabazi sugu. Wanatamani kaniki iwe nyeupe dhubutu!


Zile pesa zilizokamatwa St.Gasper ni za nani??
Unaposema Lowasa ni Mwizi ni kweli hata mimi nasema hivyo ila nataka Lowasa aseme walikuwa wanaiba na nani???
Haiwezekani Lowasa akaiba pekee !!!
Sasa wewe unataka Lowasa asitaje wezi??
Kuna wizi wa EPA, ESCROW, Meremeta nk
JAMBAZI huwa wanakuwa wengi
 
BIG UP KING COBRA!!!! Hats off to you! Kama Slaa ana masikio asikie maneno haya! Kupanda mnazi ni kazi kubwa na huchukua muda mrefu, lakini kushuka ni dakika moja. Vivyo hivyo, kujenga heshima katika jamii ni kazi ngumu inayochukua muda mrefu, lakini heshima hiyo inaweza kuporomoka kwa dakika moja tu! Yeyote atakayeshindana na wimbi hili la mabadiliko, kwa kujiona yeye ndiye mtakatifu sana kuliko Lowassa, heshima yake itaporomoka kwa dakika moja tu!!!! Huu siyo Uchaguzi wa kumtafuta "Baba Mtakatifu", ni Uchaguzi wa mtu mwenye uwezo wa kuitoa CCM madarakani, hata kama mtu huyo ni mwenye dhambi kiasi gani! After all, Slaa ana utakatifu gani, mtu aliyemwacha mkewe na kumwoa mke wa Mahimbo, aliyejikoboa ngozi mpaka mishipa ya damu inaonekana??????

Punguza mihemko hisiyokua na tija katika ujengaji hoja. Umeanza vizuri ila umemalizia na "shudu". Heshima huwa ni tunu ya kipekee Sana inapotolewa na MTU anayeitambua na kupokelewa na MTU anaye itambua pia. Swali la kipuuzi ulilouliza mwishoni. Ni sawa na umeuliza Lowasa anautakatifu gani kama alishindwa kuweka wazi ufisadi wa "Richmond"?
 
hii chance upinzan hawaji kuipata tena abadani.............kwa kipind hiki hakuna mtu awaye yeyote anaetaman CCM itoke madarakan km LOWASSA..........ndani ya nafsi yake anataman ccm iwe vipande vipande.......huyu ndo mpinzan halisi wa ccm
 
Back
Top Bottom