Danken Mbombo
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 651
- 339
Serikali iwe makini sana na wasomi wetu hawa ambao ina imani nao sana. Pamoja na kiwango chao cha elimu lakini BAADHI hawana rekodi ya utendaji mzuri. Wameathiliwa na mifumo kuliko uthabiti wa taaluma zao. Ni waoga na hawajiamini kama tunavyoona baadhi wana-copy na ku-paste ziara za kushtukiza bila mantiki yoyote kama ile ziara kwenye kituo cha tiba mbadala. Hapa ni mifano ya matokeo ya utendaji usioridhisha wa ma-doctors na ma-professors wa bongo:
ELIMU: Kiwango cha elimu kinashuka kila mwaka. Matumizi ya mfumo wa GPA hayana tija. Sera ya elimu na mafunzo haikidhi matakwa ya lugha ya kufundishia. Mipango ya maendeleo ya elimu haiendelezi elimu. Kufanya maamuzi ya kukurupuka. Chuo kikuu kutoa degree kwa wasio na uwezo kitaaluma.
AFYA: Huduma mbovu za afya, kukosekana madawa, kutotengeneza vifaa vinapoharibika.
MAJI: Kushindwa kubuni vyanzo vipya vya maji. Kutumia mabilioni katika sherehe za wiki ya maji, semina na makongamano badala ya kuchimba visima au kuvuna maji ya mvua.
KILIMO: Kutumia mabilioni kwenye tafiti zisizo na tija badala ya kuwekeza katika uzalishaji wa chakula.
UVUVI: Kuruhusu makampuni ya kigeni kufanya uvuvi bila udhibiti wowote.
JPM angalia UWEZO wa mtu kuongoza na kusimamia kazi kuliko kuangalia tu kiwango chake cha elimu. Kampuni iliyotengeneza barabara ya TAN-ZAM kutoka IYOVI hadi IRINGA hadi MAFINGA ni ya Denmark na Uholanzi. Kuanzia fundi mdogo hadi project manager hakuna aliye na PhD, masters wala degree, lakini kaangalie kazi yao.