Angalia hii kuhusu biashara ya mkokoteni

October man

JF-Expert Member
Nov 23, 2017
3,635
4,995
Salaam wadau

Katika moja ya idea(project) zangu zilizo kichwani ni biashara ya kukodisha makokoteni, dhumuni kubwa la kutaka kuanzisha hii biashara ni kukuza au kutengeneza mtaji wangu mwenyewe wa kuanzisha biashara zingine kubwa kubwa.
Nilimuuliza mtu mmoja ambaye kazi yake kusukuma mkokoteni akaniambia kuwa pesa ya kumpa mwenye mkokoteni ni makubaliano kwa yeye anampa 1000/= kwa siku, pia aliniaambia kama unaitaji kutengeneza kokoteni jipya pesa yake ni around 100,000/= mpaka 120,000/=

Kwa investigation zangu za haraka nikaona kama ndio hivyo hili faida iweze kupatikana angalau nitaitajika kuanza na makokoteni matatu kwa hesabu zifuatazo

Kokoteni 3 = 300,000/= yakutengenezea

Nikiingiza kwenye biashara

Kila Kokoteni moja =1200/day kukodisha

1200×3 kokoteni= 3600/day

Hivyo 3600/= kwa mwezi ninauwezo wa kuongeza lengine la nne hivyo hivyo la tano mwisho la sita ambapo nina target nikiwa nayo sita ndipo kikomo, nitakuwa naingiza 6000/= per day ambayo kwa mwezi ni 200,000/=

Nikifikia 200,000/= kwa mwezi hapa ndipo nitaanza kuhifadhi pesa zangu mpaka muda husika ambapo kwa mimi ni mwezi wa saba 2019 jumla kwa mahesabu yangu nitakuwa na minimum 2000,000/= si baba

Vipi kuusu hii investigation wakuu unajua nimeeleza katika linear form kuna fall and down na changamoto lakini siwezi kuzipima izo, kwa mwenye ushauri apa aweke

The List
 
Upo mkoa gani?
Je upo uhitaji wa mkokoteni?

Nasema hivi pengine umekokotoa tu pasipo kuangalia mazingira ya kibiashara ya eneo ulilopo
 
Upo mkoa gani?
Je upo uhitaji wa mkokoteni?

Nasema hivi pengine umekokotoa tu pasipo kuangalia mazingira ya kibiashara ya eneo ulilopo
Mbagala kwahiyo nina warenga waendesha kokoteni wa mbagala rangitatu, zakhiem mpaka kizuiani kwasabu kuna watu ni kazi yao ya kila siku kurndesha mkokoteni
 
Pambana mkuu. Napenda kukutia MOYO fanya wala usikate tamaa. Weka taratibu nzuri na malengo yanayofikika kisha ingia kazini. Usiidharau hata mia moja mkuu.
 
Back
Top Bottom