COARTEM
JF-Expert Member
- Nov 26, 2013
- 3,622
- 3,696
Anaandika Andrew Nyerere (mtoto wa kwanza wa Mwalimu J.K Nyerere. Kaka yao kina Makongoro na Madaraka)
___
NALAANI MBOWE KUWEKWA MAHABUSU.
Nalaani Hakimu kuiondoa dhamana ya Mbowe, na pia nalaani kesi yenyewe inayofanyika Kisutu ya kumsingizia Mbowe kuhusu kifo cha Acqulina.
Mbowe amekashifiwa sana na ameshindwa kujitetea. Hata Musiba alipoibua ushahidi kwamba Zitto ni kibaraka wa CCM, bado kashfa zimeendelea kuhusu Mbowe kwamba anafanya udikteta Chadema.
Sasa viongozi wengi wa Chadema wamehamia CCM ambao watakuwa mzigo kwa CCM Uchaguzi wa mwaka kesho. Tatizo la CCM ni kuwa na watu wengi ambao wanaweza kuongoza. Kwa hiyo unapotokea Uchaguzi wanajitokeza kugombea zile nafasi.
Sasa mtu anapowekwa ndani "ili ajifunze kuziheshimu sheria za nchi hii" lazima uhesabu siku unazomweka ndani. Mbowe amekula Christmas na Mwaka Mpya Segerea. Unataka akae Segerea mpaka lini?
Kwa hiyo nasema nalaani Mbowe kuwekwa Segerea. Nalaani. Siyo kwamba nataka aliyemweka Mbowe Segerea apate ajali, ila tu kwamba naona lile jambo siyo zuri, na haliwafurahishi watu wengi, sio tu Chadema.
Mimi ni CCM, lakini kama mtoto wa Baba wa Taifa inabidi nitazame broader picture, nitazame kuhusu umoja wa kitaifa, nifikirie kwamba sasa ni miaka ishirini tokea Baba wa Taifa afariki.
Sipendezewi na jinsi Mahakama inavyofanya kazi, jinsi ambavyo inavyowakamata watuhumiwa kwa mbwembwe na vifijo halafu kimya. Watu wanawekwa mahabusu, mahakimu wanaenda likizo kumpumzika. Na hakuna mrejesho. Hii si haki.
Tanzania inapaswa kuwa mfano kwa nchi za jirani ambazo zinatuangalia kwa makini sana, how keenly? It is a matter of life and death. Wanatuangalia kuona Tanzania tunafanya nini. Nchi kama DRC, Burundi, South Sudan, Somalia, nchi ambazo zina matatizo makubwa ya kiusalama, zinatutizama sisi.
Mtu kama Tundu Lissu ana genuine complaints. Analalamika, lakini anatishiwa as if you are the Kremlin. Kwa nini yanatokea haya matatizo ambayo yanaonekana kwamba ni viongozi tu wanagombana, hayawahusu wananchi?
Naona kuna mtu kule Venezuela amejitangaza kuwa Rais. Yule mtu nadhani ni mentally challenged kakini kama mimi, nadhani ni Baba wa Taifa.!
Sent using Jamii Forums mobile app