Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Meneja wa Huduma za Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka amesema Tuzo za Samia Kalamu Awards zimeanzishwa baada ya TCRA kubaini mapungufu katika maudhui ya ndani, hivyo wakaona kuna haja ya kutoa hamasa kwa waandishi wa habari kuandika habari zilizojikita zaidi katika maudhui ya ndani kwa ubunifu.
Akizungumza kwenye mahojiano katika Kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1 leo Mei 04, 2025 Mhandisi Kisaka amesema baada ya kuainisha mapungufu hayo kwa ajili ya kuyafanyia kazi, TCRA kwa kushirikiana na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) walitoa mafunzo kwa wanafunzi wa uandishi wa habari, wahadhiri, wamiliki wa vyombo vya habari, wanahabari na maafisa habari huku mafunzo hayo yakijikita katika maeneo muhimu ikiwemo ubunifu pamoja na matumizi ya teknolojia mpya katika uandishi wa habari.
Mhandisi Kisaka amesema baada ya kutoa mafunzo hayo likazaliwa wazo la kuanzisha tuzo zilizopewa jina la Samia Kalamu Awards ili kutazama kazi za waandishi wa habari hao baada ya kupewa mafunzo katika uandishi bunifu kwa maudhui ya ndani.
Tuzo hizo za Samia Kalamu Awards zinatarajiwa kutolewa kesho Mei 5,2025 katika Ukumbi wa Super Dome, Dar es Salaam, na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.