Andrew Chenge amekwepa mishale Mingi, hii ya mchanga haimuumizi kichwa

Joka la makengeza halikamatiki! Hata mkuu alipata kigugumizi kulitaja kwa jina lake! Ukilipamia ujue unampamia mkuu wa awamu ya tatu! Mkuu Hana ubavu huo! Ndo mana joka la makengeza halikamatiki!
 
Kuna muda nacheka japo naumia ninapo mtafakari Chenge aliwaambia kina Nape gamba limefika kiunoni njooni na shoka..
Akamaliza hivyo swala la kuvua gamba.

Akatushangaa tuliposema ana hela visiwa vya Jersey akaishia kusema ni vijisenti na likamalizika hivyo..
Ishu ya Escrow pamoja na kuwa ni mtuhumiwa ila Zitto Kabwe alikubali kufuata pendekezo alilolitoa Chenge na mwishowe akasema yeye ni nyoka mwenye makengeza na anaangalia fursa anapeleka kwa wananchi yake ile tume ya maadili ikaishia kuwahoji kina Ngeleja lakini Chenge hakutia maguu.

Katiba ya Warioba ikatupiliwa mbali ikakubalika ya Chenge.
Majuzi kaibuka kusema tume ya madini ya kwanza ilimdanganya rais lakini wakati tume ya pili inawasilisha taarifa zake Chenge alikuwa amekalia kiti cha uenyekiti bungeni akiendelea na mambo yake.

Kwa hakika Chenge sijui ni mnyama wa aina gani.
Jamaa ni noma halafu anajiamini ile mbaya,wataendelea kuzunguka mbuyu na kumuacha joka la makengeza
 
Kwa kinachoendelea katika hizi ripoti za madini, pasipo na shaka yoyote bila kumung'unya maneno wala kutikisa masikio Andrew Chenge ni mmoja ya wanadamu wenye akili zaidi ambao wamewahi kuzaliwa nchini Tanzania. Anajua nini anafanya na anajua mwisho utakuwaje, na ndio maana haishangazi kuona kila kwenye dili kubwa nchi hii ni nasibu sana kutopata jina lake.
Ifike kipindi tutambue matumizi yake makubwa ya akili kutokana na udhaifu wa nchi yetu. Kama kungekuwa na vitabu vya rekodi vya Guinness kwa nchi yetu hakika angeingia biloa kupingwa.
Naomba kuwasilisha!
 
Anaingia kwenye vitabu vya kumbukumbu na atakumbukwa kwa muda mrefu kwa miaka mingi ijayo
 
Wengi wa Vijana wa Tz mko very brainwashed,
Nothing important comes from your heads,
Nchi yenu imetafunwa na inaendelea kutafunwa lakini nyie mnakaa majukwaani kupongeza kwa ushabiki.
 
Wengi wa Vijana wa Tz mko very brainwashed,
Nothing important comes from your heads,
Nchi yenu imetafunwa na inaendelea kutafunwa lakini nyie mnakaa majukwaani kupongeza kwa ushabiki.
Kakojoe ulale...shubamiiit!!
 
Kwa kinachoendelea katika hizi ripoti za madini, pasipo na shaka yoyote bila kumung'unya maneno wala kutikisa masikio Andrew Chenge ni mmoja ya wanadamu wenye akili zaidi ambao wamewahi kuzaliwa nchini Tanzania. Anajua nini anafanya na anajua mwisho utakuwaje, na ndio maana haishangazi kuona kila kwenye dili kubwa nchi hii ni nasibu sana kutopata jina lake.
Ifike kipindi tutambue matumizi yake makubwa ya akili kutokana na udhaifu wa nchi yetu. Kama kungekuwa na vitabu vya rekodi vya Guinness kwa nchi yetu hakika angeingia biloa kupingwa.
Naomba kuwasilisha!
Remember alisema ni Nyoka wa Makengeza ha ha ha!
 
Back
Top Bottom