Andrew Chenge, akiri kupokea TSh 1.6 bilioni

Andrew Chenge, akiri kupokea TSh 1.6 bilioni

jme

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2013
Posts
4,768
Reaction score
5,102
Dar es Salaam. Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge amekiri mbele ya Baraza la Maadili kupokea Sh1.6 bilioni kutoka Kampuni ya VIP Enginering and Marketing Limited, zikiwa ni malipo ya kutoa ushauri.

Pia, alihoji kama kuna tatizo kutumia taaluma yake ya sheria kuzishauri kampuni binafsi na kujipatia fedha.

Chenge ambaye alitoa utetezi wake jana saa 7:30 mchana, alisema hakulipwa fedha hizo kwa sababu ni kiongozi wa umma, bali kwa kutoa ushauri.

Alisema aliingia mkataba na kampuni hiyo wa kutoa ushauri wa kisheria dhidi ya Kampuni ya Mechmer ambazo ni kampuni binafsi zilizokuwa na mgogoro.

"Nawashangaa mnalalamika Chenge kulipwa na Kampuni ya VIP au wamewafuata na kulalamika kwamba hayakuwa malipo halali," alihoji.

Alisema hakuna kufungu cha sheria kinachomzuia kutoa ushauri wa kisheria kwa kampuni binafsi.

Kuhusu malalamiko kwamba akiwa Mwanasheria wa Serikali aliishauri kuingia mkataba wa kuuziana umeme kati ya Kampuni ya IPTL na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Chenge alisema anawashangaa wanasheria wa sekretarieti kwa malalamiko hayo.

"Sikuishauri Serikali kuingia mkataba na IPTL bali ofisi yangu ndiyo iliyotoa ushauri kisheria. Nakubaliana na walalamikaji kwamba mwaka 1995 nilikuwa mwanasheria wa Serikali, lakini sikubaliani na madai yao."

Alisema Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali ilitoa ushauri huo kwa sababu ndiyo jukumu lake.

"Wanasheria ni lazima wafahamu kwamba ile ni taasisi na siyo mtu kama Chenge," alisema.

Alisema ofisi yake ilitoa ushauri wa mikataba mitatu ya IPTL na Serikali kwa lengo la kuongeza umeme hasa kutokana na ukame uliolikumba Taifa.

"Naomba baraza lako liyapuuze kwa dharua zote na kuyatupilia mbali malalamiko ya sekretarieti kwa sababu hayawezi kukusaidia kutoa uamuzi ulio sahihi," alisema.

Kuhusu kutumia taarifa alizozipata akiwa mwanasheria wa Serikali na kuzitumia kwa masilahi binafsi, Chenge alisema: "Naomba wachanganue taarifa hizo ni zipi kwa sababu huwezi kumlalamikia mtu kwa jumla lakini kwenye malalamiko husemi.

Shahidi wa mlalamikaji, Waziri Kipacha alisema Chenge akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) mwaka 1995, aliishauri Serikali kuingia mkataba wa miaka 20 na IPTL.

Alisema baada ya kustaafu mwaka 2005 aliingia mkataba wa kuwa mshauri mwelekezi wa kampuni hiyo iliyokuwa inamiliki asilimia 30 ya hisa za IPTL.

Alisema kitendo cha kuingia mkataba na VIP ni ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Chanzo:
Mwananchi
 
Chenge ni Rafiki Mkubwa sana wa Mgombea Urais wa Chadema na Mgombea Ubunge wa Ccm. Ufisadi umetamalaki sasa kweny Vyama vikuu vya Siasa hapa nchini
 
hakuna mwanasheria wa kumshinda chenge kwa hoja.

cheki anavyopangua hoja zao.

huyu baba mwizi sana. anatumia taaluma yake na upeo wake kutuibia
 
atakaribishwa..kwa shangwe kweli huyu cdm na tutaambiwa tatizo mfumo..ameshakuwa msafi.. alikuwa mchafu alipokuwa ccm..looh tumerogwa sie..
 
Hii post sasa hivi haiwezi kupata wachangiaji wengi kwa sababu group kubwa la wachangiaji ambao Ni chadema na ukawa kwa sasa hawawezi kuongelea ufisadi.

Hahahahaha.....
 
Kama anaona hali mbaya aje huku mwangani...
 
Hii post sasa hivi haiwezi kupata wachangiaji wengi kwa sababu group kubwa la wachangiaji ambao Ni chadema na ukawa kwa sasa hawawezi kuongelea ufisadi.

Mtasema sana, alipokuwa kwenu hamkufungua vinywa vyenu, muwe makini msilipuliwe!
 
Soon tutaambiwa ndio mshauri wa sheria Chadema.!
 
Mna mahakama, Polisi, Takukuru nk,mnashindwaje kuwatia hatiani? Mramba na wengine ndio wabadhirifu, wameshtakiwa, Lowassa lini alishtakiwa? Mwaka huu Mtabadili sana Mikao, Msumari unaingia tu slowly Kila mkijigeuza
 

Alisema hakuna kufungu cha sheria kinachomzuia kutoa ushauri wa kisheria kwa kampuni binafsi.

“Sikuishauri Serikali kuingia mkataba na IPTL bali ofisi yangu ndiyo iliyotoa ushauri kisheria.
Nakubaliana na walalamikaji kwamba mwaka 1995 nilikuwa mwanasheria wa Serikali, lakini sikubaliani na madai yao.”

“Wanasheria ni lazima wafahamu kwamba ile ni taasisi na siyo mtu kama Chenge,” alisema.

Alisema ofisi yake ilitoa ushauri wa mikataba mitatu ya IPTL na Serikali kwa lengo la kuongeza umeme hasa kutokana na ukame uliolikumba Taifa.


Chanzo:
Mwananchi

Wasomi wa Havard hao.
Mbona haikushitakiwa Gari lake alipo wagoinga wale akina Dada.Dereva ndiye aliyeshitakiwa hivyo hivyo yeye kama AG ndiye mhusika mkuu.


 
Mna mahakama, Polisi, Takukuru nk,mnashindwaje kuwatia hatiani? Mramba na wengine ndio wabadhirifu, wameshtakiwa, Lowassa lini alishtakiwa? Mwaka huu Mtabadili sana Mikao, Msumari unaingia tu slowly Kila mkijigeuza

Sheria ya maadili ya umma inasemaje? mtu akistaafu anaruhusiwa kutumia taaluma yake kujipatia kipato? IGP akistaafu akaanzisha kampuni ya ulinzi itakuwa makosa? RPC akistaafu akaajiriwa KK security itakuwa nongwa?

Au tulitaka akistaafu afuge ng'ombe wa maziwa wakati yeye ni mwanasheria kwa taaluma.
 
Chenge mbele ya ccm, Kinana, Kikwete na Nepi siyo fisadi wala makapi! Siku akitoka tu ccm na kujiunga na Chadema ataitwa fisadi na makapi.

Chezea ccm we we.....chama kubwa.
 
Naomba mwenye matokeo yake ya O level,A level na GPA yake ya UDSM. Harvard hadi SUMAY kasoma pale.
 
Ccm acheni kutuchezesha mchezo wa kitoto...tunataka kujua zile billioni zilizobebwa toka stanbic kwa viloba na magunia ni za nani...??
 
Back
Top Bottom