Andaeni wasimamizi wawili na fomu ya kusaini matokeo kwa kila mgombea wa Udiwani

Stabilaiza

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
1,843
1,143
Kutafuta ushindi kwa kubaka demokrasia ni mbinu ya kawaida inayotumiwa na chama cha CCM. Hawataki demokrasia ifanye kazi, wanataka chama kishike hatamu jua liwake lisiwake au mvua inyeshe isinyesha wao wanataka ushindi wa mezani. Nawatahadharisha UKAWA kuwa wajiandae kuzuia hujuma katika kutangaza matoeo. Njia sahihi ni kupitisha utaratibu katika kikao cha uchaguzi wa meya wa Ilala na Kinondoni kila mgombea awe na wasimamizi wawili wa uchaguzi, karatasi za kupigia kura zithibitishwe na wagombea na kuwepo na fomu za kusaini matokeo kabla ya kutangazwa na msimamizi wa uchaguzi. Kila mgombea apewe nakala ya matokeo kabla ya matokeo kutangazwa. Hii itazuia msimamizi wa uchaguzi kutagaza mshindi aliyeshidwa katika kura.

Ingawa UKAWA wamefanikiwa kuzuia madiwani wa Zanzibar kupiga kura kwa kuleta madiwani wa Zanzibar kama walivyofanya CCM, UKAWA wanataliwa wabane kwenye usimamizi wa kura na utangazaji wa matokeo kwa njia hizo nilizosema hapo juu. Nichukue fursa hii kuwapa hongera kwa kuleta wamumluki kutoka Zanzibar kama walivyofanya CCM vinginevyo hawa watu wa CCM ni specialist wa ushindi wa mezani, aka magoli ya mkono. Siku ya uchaguzi wawepo kujiandaa na hujuma yoyote ile ili kama wa CCM wataletwa dakka za mwisho madiwani wa Zanzibar kabla ya kuanza kikao na wa UKAWA nao wawe karibu kuingia.
 
Unapongeza utumbo kisa ccm wamefanya utumbo,akili za ukawa hizi.
Kura ni siri,yawezekana kabisa mtu wa cuf akampigia ccm,ndio demokrasia hiyo
 
Unapongeza utumbo kisa ccm wamefanya utumbo,akili za ukawa hizi.
Kura ni siri,yawezekana kabisa mtu wa cuf akampigia ccm,ndio demokrasia hiyo
Mtu wa UKAWA atapiga kura kwa CCM kama amehongwa na si vinginevyo!
 
Unapongeza utumbo kisa ccm wamefanya utumbo,akili za ukawa hizi.
Kura ni siri,yawezekana kabisa mtu wa cuf akampigia ccm,ndio demokrasia hiyo

Nani kasema kura siyo siri?? Soma thread uelewe. Vyovyote iwavyo, muhimu ni kuwa na utaratibu utakao hakikisha kinachotangazwa ni matokeo halali ya upigaji kura. Umesahau pia si mwiko kwa diwani wa CCM kupigia Ukawa kama sehemu ya demokrasia.
 
Unapongeza utumbo kisa ccm wamefanya utumbo,akili za ukawa hizi.
Kura ni siri,yawezekana kabisa mtu wa cuf akampigia ccm,ndio demokrasia hiyo
Kuandaa wasimamizi na fomu ya kujaza matokeo ndiyo utumbo? Nadhani utumbo ni huu unaoleta wewe. Kama CCM wanaleta mamluki wewe unaona kunauchaguzi hapo?
 
Back
Top Bottom