ANC yamtuhumu Malema kwa uhaini

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
160404130203_julius_malema_624x351_bbc_nocredit.jpg


Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimemtuhumu kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF),Julius Malema kwa uhaini.

Kiongozi huyo wa EFF anadaiwa kusema ''kuwa serikali ya rais Jacob Zuma inapaswa kukoma kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia wanaoandamana kwa amani la sivyo itang'olewa madarakani kwa mtutu wa bunduki.

Image copyright BBC World Service
Image caption Msemaji wa ANC Zizi Kodwa anasema matamshi ya Malema ni tishio kwa usalama wa taifa
''Matamshi hayo ni ya kutishia amani na utangamano nchini Afrika Kusini kwa hakika hayo ni matamshi ya uhaini na hatua kali zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya Malema'' msemaji wa ANC Zizi Kodwa alisema.

''Tunaiomba serikali ichukue hatua kali zaidi dhidi ya matamshi hayo ilikuzuia visa vya utovu wa usalama''

Katika mahojiano ya moja kwa moja na shirika la habari la Al Jazeera, bw Malema, alisema kuwa matokeo ya uchaguzi wa 2014 katika jimbo la Gauteng hayakuwa ya haki na akaonya dhidi ya wizi wa kura katika uchaguzi ujao wa kimkoa.

Image copyright AP
Image caption Uchaguzi huo wa mashinani unatarajiwa kufanyika mwezi Agosti.
Uchaguzi huo wa mashinani unatarajiwa kufanyika mwezi Agosti.

''Sehemu moja ya wajibu wetu wa mapinduzi ni kupigana na iwapo itatubidi ,hatutakuwa na ila bali kuchukua silaha na kutetea haki zetu.Tutapigana. alisema bw Malema.

Chama tawala cha ANC kinamtuhumu Malema kwa kukiuka kanuni za kitaifa za uchaguzi kwa kuwachochea watu wapigane.

Kodwa alisema kuwa hiyo ni kinyume cha sheria ya nchi.

140505162859_julius_malema_464x261_ap_nocredit.jpg
 
huyo alimwambia spika sitoki nje na sibadili kauli Zuma ni Mwizi tunaongozwa na Rais jambazi...aliwahi enda Jeshini na kuwaambia wagome wanajeshi kwa kulipwa mshahara mdogo na ilitokea vugu vugu la mgomo akiwa youth leader president wa Anc ndio kisa kilichomuondoa huko alianza kukubalika na majeshi pia..
 
huyo alimwambia spika sitoki nje na sibadili kauli Zuma ni Mwizi tunaongozwa na Rais jambazi...aliwahi enda Jeshini na kuwaambia wagome wanajeshi kwa kulipwa mshahara mdogo na ilitokea vugu vugu la mgomo akiwa youth leader president wa Anc ndio kisa kilichomuondoa huko alianza kukubalika na majeshi pia..
sipendagi viongozi radical kama hawa, hata kama wana hoja, kwa nchi zetu na wanachi wanavyoweza kuhadaiwa na wanasiasa hawa wanaleta vita
 
malema ni mchochezi na mbaguzi mimi binafsi simkubali ndie aliefanya mchakato wa kumtoa Mbeki ili Zuma apate leo wametofutiana maslahi akataka kumtoa tena Zuma ikabidi chama kimtimue na kuunda chama chake huyo sio kabisa..
 
Alishawahi toa kauli kuwa South Africa sio ya wa khosa tuu iweje Mandela mkhosa..Mbeki mkhosa nyinyi Wa zulu ndio mliopigania hii Nchi hao wakina Mbeki walikimbilia kusoma Urusi ndio maana wao wamesoma sisi hatujasoma huyo jamaa ni kavu kweli...
 
Back
Top Bottom