MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,801
Tokea dunia iumbwe na hata katika kufanya tafiti zangu kadhaa maeneo mbalimbali hasa zinazohusu viongozi wa kiafrika na tawala zao leo naomba tu niseme ukweli kuwa sijawahi kuona na kuvutiwa na aina ya uongozi mzuri kabisa wa hawa wawili Rais Dkt. Magufuli na Mkuu wake wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul C. Makonda.
Nadhani ifike muda sasa watanzania tuache kusikiliza maneno ya kimajungu, unafiki na uwongo tunayoaminishwa juu yao na ifike muda sasa kila mmoja wetu aonyeshe mapenzi yake ya dhati kabisa kwa Rais JPM na Mkuu wa Mkoa Makonda.
Kamwe chuki zetu ambazo zinaratibiwa kwa kiasi kikubwa sana na maadui wa nchi hii waliopo ndani na nje zisitufanye tukawachukia kiasi hiki hadi kufikia hatua ya kuwasema, kuwadhihaki na kuwahisi vibaya wakati pengine hata huo ushahidi labda hatuna.
Hivi kwa nchi kama yetu ya Tanzania iliyobarikiwa kabisa na Mwenyezi Mungu hadi akatupa hawa Viongozi wawili Rais Magufuli na Mkuu wa Mkoa Makonda na jinsi wanavyofanya kazi zao vizuri kabisa na kiueledi tukisema wewe au nyie ambao mnawadhihaki na kuwachukia kuwa pengine mna matatizo ya akili na mnahitaji kwenda kupimwa akili tutakuwa tunakosea?
Katika maisha yangu yote hadi sasa sijawahi kumpenda na kumkubali mtu hasa kiongozi halafu asiwe ni mzuri au anayefaa hivyo basi kupitia huu uzi wangu naomba kuanzia leo nyote mnaowaona akina Rais Magufuli na Mkuu wa Mkoa Makonda ni wabaya au hawafai basi badilisheni upesi hayo mawazo yenu kabla hamjamuudhi Mwenyezi Mungu kisha akawaondoa na nchi yenu ikawa kwa watu wengine wasiokuwa na hata chembe ya uchungu na Tanzania yetu.
Ewe Rais Magufuli na Mkuu wa Mkoa Makonda msiogope, fanyeni kazi na Mungu atawalinda na kuwabariki.