Anayesema Arusha si salama ni mnfiki

Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
11,733
14,627
Ndugu wanajamvi,kumekuwa na hoja isiyo na uzito inayosambazwa kwa kiasi kikubwa na kundi fulani la watu labda kwa maslahi yao ambayo hata hivyo hayako wazi sana,mfano ni jana nilipokuwa kwenye basi maarufu hapa arusha kama hiace,inayoelekea njiro kulikuwa na askari kadhaa(hawa wadogo wadogo waliotoka ccp juzijuzi) mmoja alikuwa akiongea na simu na nilichokinukuu ni kama hivi»"ndiyo mzee, mi nipo arusha huku,tumekuja kusimamia uchaguzi ukimalizika ndio tutarudi huko,aaah tupo poa tu, ila si unajua tena arusha mwanangu vurugu tupu? Eeh tunakomaa tu hivyo hivyo mwanangu,dah! Yaani arusha ni pagumu balaa mtu wangu". Hapo ndipo nilipoanza kuuhisi unafiki dhahiri unaosambazwa na watu fulani tusiowajua,na kwa sababu tusizozijua,Nasema ni unafiki kwa sababu,kwa yeyote aliyeishi arusha tokea miaka ya 80 atakiri kuwa arusha ni salama kwa sasa kuliko wakati mwingine,na hii inadhihirika kwa kuuliza ama kulinganisha matukio ya uvunjifu wa amani ya hapo zamani kidogo na sasa hivi ambapo matukio ya uhalifu yamepungua kwa kiasi kikubwa sana,mfano wa matukio hayo ni yale ya ujambazi wa kutumia silaha nzito yaliyowahi kushamiri hapa siku zilizopita,ambayo kwa siku za karibuni tunayasikia yakipamba moto jijini Dar es alaam,vile vile ukabaji na uporaji wa kutumia nguvu pomoja na silaha ndogondogo kama visu,bisi bisi,mapanga,marungu nk ambayo yaliondoa maisha ya raia wengi wasio na hatia huku wengine wakiachwa na ulemavu yamepungua kwa asilimia kubwa sana,na hata baadhi ya sehemu zilizokuwa zikiogopeka kwa matukio hayo kama vile unga ltd,kijenge,majengo nk,matukio y uhalifu na hata ulevi wa mihadarati haupo kwa kiwango kikubwa,hivyo kusema eti arusha si salama kwa sababu ya mabomu ya machozi ni upofu,tuki judge usalama kwa kuangalia idadi ya watu waliopigwa risasi na polisi hapo dhana ya usalama inabidi ibadilishwe,labda polisi na serikali iseme sasa inaamua kuondoa usalama uliokuwepo,na isinge kuwa haki kwa polisi kudai eti arusha hakuna usalama huku wakijua wazi uhusika wao kwenye kuhatarisha usalama waseme tu kama wanaamua/wameamua kuiondoa amani/usalama tuwaelewe!! Kipindi cha nyuma ilikuwa ni hatari kukatiza unga ltd hata saa kumi na mbili jioni,leo ni salama zaidi kukatiza ungaltd saa sita usiku iwapo tu hutakutana na polisi,enzi za mrema lyatonga watu walipigwa mabomu na huku wakikabwa na vibaka mitaani,watalii walikuwa wakiporwa mali zao kila kukicha,na wakati wote huo wananchi walikuwa wakilalamikia hali mbaya ya usalama ila polisi na viongozi wengine wa serikali walipinga vikali na kudai hali ya arusha ni shwari kabisa,leo wananchi wanaamini arusha ni shwari.polisi na chama tawala wanavuruga usalama na kutulazimisha tukiri kuwa arusha si salama!!! Kwa faida ya nani??ni nani anayetakiwa kulaumiwa ikiwa usalama wa arusha utayumba?huu ni unafiki mkubwa kwa serikali kutoa kauli za uongo huku ikijua wazi wao ndiyo watuhumiwa #1 kuvuruga usalama.
 
Back
Top Bottom