Anayekumbuka namna Dr Shein alivyo teuliwa kuwa Makamu wa Rais tafadhali atueleze

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,111
115,906
Mara baada ya kifo cha ghafla cha aliekuwa Makamu wa Rais wakati huo Dr Omary Ally Juma.

Aliteuliwa Dr Mohamed Shein kushika wadhfa huo...mnakumbuka ilikuwaje?

Alipigiwa kura bungeni?

Au aliteuliwa na kuapishwa?

Anaekumbuka naomba atukumbushe
 
Kwani katiba inasemaje Mkuu? Au toka enzi hizo katiba ilishaanza kusiginwa?
 
Labda kama katiba imebadilishwa.
Hata swala la makamu kurith urais, mara ya kwanza ilikua kama akirith kiti cha urais ikiwa imebaki miezi 18 au miaka miwili basi atamalizia muhula, ila kabla ya hapo angetakiwa kuitisha uchaguzi baada ya miezi mitatu.
 
Nakumbuka Mkapa alitangaza Tu na kumuapisha..
Shein hata mimi sikumbuki kama aliapishwa kwa Msekwa

Na nnakumbuka vizur sana nilikua nafuatilia lile Bunge nikimfuatilia Mrema na vipande vyake vya magazeti kila siku anapigwa "suspension".....
Toka awamu ya kwanza y BWM
 
Mara baada ya kifo cha ghafla cha aliekuwa Makamu wa Rais wakati huo Dr Omary Ally Juma.

Aliteuliwa Dr Mohamed Shein kushika wadhfa huo...mnakumbuka ilikuwaje?

Alipigiwa kura bungeni?

Au aliteuliwa na kuapishwa?

Anaekumbuka naomba atukumbushe

..Ninavyokumbuka aliapishwa moja kwa moja.

..Na sababu yake ni kwamba Raisi alikuwa hajabadilika.

..Swali ninalojiuliza mimi ni ikiwa Mama Samia anatakiwa ateue Waziri Mkuu na baraza la mawaziri upya.
 
Mara baada ya kifo cha ghafla cha aliekuwa Makamu wa Rais wakati huo Dr Omary Ally Juma.

Aliteuliwa Dr Mohamed Shein kushika wadhfa huo...mnakumbuka ilikuwaje?

Alipigiwa kura bungeni?

Au aliteuliwa na kuapishwa?

Anaekumbuka naomba atukumbushe
Alithibitishwa na Bunge baada ya Rais kupeleka jina lake

Nafasi za Makamu wa Rais na Waziri mkuu majina hupelekwa Bungeni kuthibitishwa na wabunge
 
Kwani Mama samia alipoteuliwa kuwa Makamu wa Rais alithibitishwa lini na Bunge?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…