Anayejua dawa ya gaga tafadhali

Lububi

JF-Expert Member
May 3, 2013
2,121
3,732
Zinamsumbua mama. Naskia kuna dawa yakuzifuta kabsa. Sijawai kukosa jibu sitahiki jf
 
Nafikiri akitoka kuoga aweke maji ya uvuguvugu kiasi kwenye lita moja kisha achanganye na maji ya betri vijiko vinne, wiki tu gaga hakuna.
 
Mwambie ajitahidi kusafisha vizuri miguu yake kisha akaushe kwa tauro na apake mafuta ya mgando ili kulainisha ngozi mara nyingi ngozi ya miguu ikiwa kavu ndo huwa inasababisha hilo tatizo.
 
Mafuta ya argan ndo yakoje. Ya nyonyo ngum kupata
ya nyonyo nenda uuka lolote la dawa za kizungu au asili ulizia "CASTOR OIL" Utayapata ndo ya nyonyo na kuhusu mafuta ya "ARGAN" Nenda maduka ya wapemba ya viungo na dawa asili utayapata yanatoka nje kichupa ni sh.2500/=
 
Pole, ila mwambie miguu asiisugue na mawe inazd kuwa migumu, tafuta brush laini tu weka maji ya vuguvugu kwenye beseni ingiza miguu iache kwa muda kdg hata dk 5 then anza kusugua na brush taratiibu baada ya hapo futa maji yote pakaa vasline then mwambie avae soksi hata akiwa nyumbn na asipende kutembea peku(barely).

Namshaur pia apende kuvaa viatu vya kuvika pamoja na soksi akiwa ana Safari, hii inasaidia kuipa miguu joto la kutosha na kufanya iwe lainiiii na hatimae hilo gaga hataliona tena kwenye miguu yake
 
Nafikiri akitoka kuoga aweke maji ya uvuguvugu kiasi kwenye lita moja kisha achanganye na maji ya betri vijiko vinne, wiki tu gaga hakuna.
Weee unataka kumkata mama wa watu miguu;
Kijana mmoja alishauriwa hivyo akiwa na fungus, ugonjwa ukabadilika ukawa kansa;
 
1. - chemsha maji yawe ya uvuguvugu
- mimina kwenye beseni
-weka sabuni katika maji yako
-tumbukizi miguu kasha uanze kusugua kama na jiwe au brush
- kausha miguu na kitambaa kikavu na upake mafuta kasha vaa socks tena lala nazo

2. MAJI YA LIMAO
-kata limao vipande viwili
- chukua kimoja na uanze ku sugua katika magaga yako hakikisha maji ya limao yana ingia au kupita katika magaga yako
- fanya hivi kwa muda usiopungua dakika tano
- sugua magaga kwa brush au jiwe
- uoshe miguu yako.

3. OLIVE OIL
- paka mafuta ya olive katika pamba
- anza kusuuga katika magaga kwa mfumo wa duara kwa muda wa nusu saa
- vaa soks na iache kwa dakika 45

JARIBU HIZO HAPO ONE OF THAT.
 
Back
Top Bottom