Anayejua anajua tu.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anayejua anajua tu....

Discussion in 'Sports' started by Anselm, Jul 29, 2012.

 1. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Siku zote matokeo ya uwanjani katika mchezo wa mpira wa miguu ndo hutoa picha kamili ya nani anajua.
  Yanga walipiga mechi 2 za kirafiki, ya kwanza dhidi ya Xpress ya Uganda ambapo walishinda 2-1,siku iliyofuata Xpress walicheza na Simba na kutoka droo 0-0,gazeti 1 lilimnukuu anayedaiwa kuwa kocha wa Xpress akiisifu Simba kuwa inajua zaidi,akisahau kabisa kuwa hao anaowasifia walishindwa kutoka na ushindi dhidi ya team yake ambaye mwenyewe alikiri ilikuwa haina baadhi ya wachezaji wake tegemeo.
  Yanga wakapiga mechi ya 2 ya kirafiki dhidi ya 1 wapo ya team inayosifika kwa kusakata kabumbu safi hapa Tanzania wakashinda 2-0,watu wakasema hiyo team ni dhaifu kwakuwa Yanga na Simba zilichangia kuidhoofisha kwa kuwachukulia wachezaji wake mahili Frank Domayo na Abdalah Juma wakasahau kuwa JKT Ruvu ambayo ni team ya jeshi hukaa kambini muda wote wakifanya mazoezi hivyo katika hali ya kawaida hasa inapokutana na team hizi kubwa huleta upinzani mkali sana.
  Haya pazia la Kagame likafunguliwa,mechi ya kwanza Yanga akachukua kichapo kutoka kwa Attletico 2-0,waumini wa kuiona Yanga mbovu wakapata maneno ya kusema bila kujali kuwa hadi Yanga ikicheza mechi ile ya kwanza Kocha wao Mkuu "Mt Tom" alikuwa hajapata kikosi cha kwanza na hilo lilidhihirika hata kwenye upangaji wa ile team,uwepo wa wachezaji kama Jerry Tegete,Shamte Ally na Rashid Gumbo aliyecheza namba 8 akimsogeza Febregus namba 9 kwenye kikosi kilichoanza kulitupatia picha tunaoijua Yanga kuwa bado kocha ana'struggle kutengeneza team,ikumbukwe alikuwa na wiki 1 tu ya kuiandaa team hiyo kwa mashindano hayo,game ikapigwa na Yanga ikavuna ilichovuna kipigo cha 2-0.
  Game ya 2 ikawadia "Mt Tom" akabadili kikosi na mfumo wa uchezaji,wenye namba zao akawarudisha kwenye namba zao,Yanga wakapiga soka 1 la uhakika sana siku hiyo na kuichapa Wau Salam ya Sudan Kusini 7-1....kama kawaida Wasemaji(hasa wa upande wa 2) wakabeza Wau Salaam vibonde kwahiyo huo ushindi si wa kutambia sana,siku inayofuata Simba wakateremka dimbani kucheza na Vibonde wa kundi lao,wakitaka kudhihirisha kuwa wao ni bora kuliko Yanga washinde magoli mengi zaidi,ubovu wao ukadhihirika wazi wakapata ushindi wa kupigania kwa nguvu zao zote wa goli 3-0 shukrani kwa goli la kuotea la Abdalah Juma na lile la penalt,wenye kujaliwa vipaji vya kutathmini soka tukajiridhisha kuwa kati ya team hizi mbili zilizoingiza vikosi kwenye michuano ya Kagame Yanga anaujua kuliko Simba.
  Zikafuata mechi za 3 za kutafuta nafasi za team zitakazocheza robo fainali ambapo kimsingi team zote 3,3 kutoka katika makundi zilishajulikana, Yanga ambayo ilikuwa inaendelea kuimarika siku hadi siku ikamchapa team ngumu kabisa APR 2-0,wakati Simba katika mechi yao dhidi ya AS Vita ilibidi ifanye kazi ya ziada kusawazisha goli na kufanya matokeo yawe 1-1 ,bado WajingaX2 wakaponda ooh APR haikucheza seriously ksbb walikuwa wameshakata ticket wakasahau kuwa pamoja na AS Vita nao kutocheza seriously ksbb kama za APR lkn team yao ilishindwa kutoka na ushindi.
  Haya walioingia robo fainali wakaingia,Yanga dhidi ya Mafunzo game ikapigwa dk 90 1-1,wakiongozwa na kanuni wakaingia kwenye matuta Yanga wakapenya nusu fainali kwa penalt 5-3, wachongaji kama kawaida yao wakachonga tena ooh mmeshindwa kuwafunga Wazanzibar ndani ya dk 90 team yenu mbovu, wakasahau Mafunzo ambayo mimi naichukulia 1 kati ya team zilizosakata soka safi katika michuano hii ilikuwa vizuri sana na ndo maana walitoka sare na Azam(wababe wa Simba) na Tusker ya Kenya.
  Robo fainali ya 2 ikawadia Simba na Azam sina haja ya kukumbushia matokeo hapa,kilichotokea kila mtu anakijua.....AIBU.
  Haya...walioingia nusu fainali wakaingia,Yanga akaangukia katika mdomo mwa APR tena,safari hii wakiwa wamepania hasa,game ikapigwa dk 90 0-0,kanuni zikaziingiza kwenye dk 120,Hamis Kiiza akaifungia Yanga goli la kuipeleka fainali,Wachongaji kama kawaida ooh mmebahatisha,mara goli tata...maneno kibao,mwisho wa siku wanaojua wakaingia fainali.
  Fainali ikawadia jana Yanga dhidi ya Wababe wa Simba,mashabiki wa Simba wakiamini ksbb team yao ilifedheheshwa na Azam, basi na Yanga nayo itafedheheshwa vilevile,wakajazana uwanjani kui'support Azam.
  Vijana wa "Mt Tom" wakawadhihirishia kuwa wanaujua, mpira ukaisha ndani ya dk 90 na Wababe wa Simba wakafedheheshwa kwa kipigo cha 2-0,shukrani kwa magoli ya ma'super strikers Kiiza na Bahanuzi.
  Cha kushangaza bado wajingaX2 wameendelea kuingiza maneno yao (najua hata hapa wata'comment) ooh mara wamebahatisha mara beki ya Azam ilifanya makosa ya kizembe..jamani ndo kutoujua kwenyewe huko.
  Tukubali tukatae,ANAYEJUA ANAJUA TU.....Yanga ya safari hii inaujua,fullstop(.)
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  najuta kwa nini hatukuchukua maana zingekuja post za wamenunua mechi....:eek2:
   
 3. collycool

  collycool Senior Member

  #3
  Jul 29, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 45
  Nakuunga mkono na miguu 100% yaani yanga wamefunga midomo wengi sana hasa hawa wanaojiita wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari waliokuwa wanaponda kuhusu yanga semeni tena
   
 4. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,223
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Naungamkono hoja 100%
   
 5. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
 6. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kiongozi ungejuta kwanza kwa kushindwa kufika angalau kwenye dk 120 au penalt,unajua fainali ya kuisha ndani ya dk 90 ni kwamba Mzani ulilemea upande mmoja haswa despite zile pass za visigino zisizokuwa na tija zilizokuwa zinapigwa na wachezaji wenu
   
 7. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 740
  Trophy Points: 280
  Hakika ni kweli uyasemayo wa 2 ni 2 tu.
   
Loading...