mstaafrika
Member
- Jan 3, 2017
- 10
- 2
Kutoka kwa Nguli wa sanaa Tanzania; Mswahili VITALI MAEMBE.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Dk Harrison Mwakyembe Unazidi kunitia Aibu!
Mtu Mzima: Guitar Man!
Vitali Maembe: Hi!
(Eti namimi nikajikuta nimeitikia tu kama
Mzungu)
Nilivyoongea tu akagundua sio wa kwao...
Akajinyooshea kidole kujigusa kifuani aniambia,
"Chace, from France"
Namimi sikubaki nyuma, nikajishika kifua
nikamwambia "Vitali from Tanzania"
Akacheka!
Chace: Tanzania, beautiful country! How is
Trump!
Vitali: I am NOT American, I said "VITALI FROM
TANZANIA"
Chace: I know Tanzania, I know Nyerere, Ali,
Ben, Kikwete and this one!
Chace akanitazama usoni na kuanza
kunizungumzisha kuhusu Gita na Muziki!
Moyoni mwangu nikaziwaza kama ni hivi hawa
jamaa inawezekana kabisa wanaona na
wanakumbuka!
Billioni 50 za JK, Bilioni 205 Kampuni ya
MEREMETA, 2014 Bilioni 306 TEGETA ESCRO na
STANBIC Bank, 2011 Bilioni 73 CHENJI YA
RADA, Bilioni 133 EPA - BOT, 2006 RICHMOND/
DOWANS.
Nilikuwa ndiyo nimeshuka kwenye Ndege ya
awali Amsterdam, Uholanzi, ndani ya jengo la
uwanja nangoja kuunganishia Ndege, Geti
namba D16 niende niendako!
Nimetulia nimejikunyata kwa baridi nikiwa
natafakari Mustakabali wa Taifa letu na kisa cha
Rais wangu kuitwa Trump, mara nasikia tena
huko nyumbani Tanzania, ndani ya Bunge
tukufu Daktari Mzima, Waziri mwenye dhamana
unakurupuka, unazungumza kama sio msomi
bwana! eti "wanamuziki wakae nje ya siasa na
kuzingatia sanaa zao"
Yaani kumbe Waziri hata hujui ujumbe katika
Sanaa unatokana na nini?
Dk Mwakyembe, unawadanganya watu
hakukuwa na mwanamuziki DUNIANI ambao
wamepata mafanikio na umaarufu kwa kuikosoa
serikali yao.
Sitaki kuamini kuwa mafanikio kwako wewe ni
kuwa na pesa na umaarufu!
"Alafu unatoa mfano wa WAFU wa nje wa
kitamaduni wa kutoka nje, unaacha kuwataja
akina Marijani, Mbaraka, Ongala, hao unaona
hawajafanikiwa watoto na wajane wao unawalea
wewe?
Wenye akili wanakushangaa unaposhauri
Wanamuziki tunyamaze, tuwaachie wanasiasa
wafanye Siasa.
Wanasiasa gani? Kwa uwelewa upi wa Siasa mlio
nao mpaka tuwaachie nchi?
Siasa hizihizi za Dharau, ubaguzi na vitisho?
Hakuna Mpinzani wala Chama tawala ambaye
anafikiri atamnyamazisha Msanii mwenye akili.
Muziki wetu hauna ugomvi wala chuki na nyinyi,
Muziki una chuki na matendo yenu ya Uwongo,
Wizi, Rushwa, Uharibifu wa Nchi na Utamaduni,
jirekebisheni tutawasifia lakini kwa haya
mtasifiwa na hao wasanii wenu mnaocheza nao
na kuwaita Ikulu Bungeni wizarani na
majumbani mwenu.
Muziki wetu siyo wa hivyo, hautaweza
kuubadilisha.
Nawewe John tuheshimiane bwana!
Hii sio Wizara ya majaribio, kila kukicha
tunakosa sisi tu.
'Wizara hii Muhimu, usiwe kama Makocha wetu,
una wachezaji wazuri 30 Unashindwa kupanga
listi ya wachezaji 11, kwenye nafasi
wanazoweza. Umetoa afadhali umeingiza
potelea mbali.
Mwakyembe!
Makelele yatanyamaza lakini Muziki
utaendelea.