Eversmilin Gal
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 778
- 270
Yeye huyo rafiki yako ndiye chanzo cha tatizo. Kwanza alitakiwa akae na mume wake wapange future zao mfano waamue kama ni shule kwanza zaidi au kazi kwanza. Kama angemkatalia sema kazi anaweza kutafuta watu wakawashauri. Kosa jingine ni la yeye kumtegemea mume amtafutie kazi, kwani yeye hajui kusoma magazeti? Atafute kazi kivyake vyake,
kwani akiamua kujiendeleza shule je?
kumshauri amuache mume now ana mtoto mdogo na hajawahi jitegemea
ni ngumu sana...
ushauri avumilie hukuanajiendeleza shule
na akitaka kumuacha mume ahakikishe amepata kazi kwanza
mpe pole
jamani nimepokea simu ya rafiki yangu akaniambia anatamani afanye maamuzi magumu lakini yuko kwenye dilemma anataka aachane na mume wake dilema iko kwenye mwanaye bado hajaweza kujitegemea anajisahau anajiko**lea mara nyingine anajin**e hajaweza kuongea vizuri huyo rafiki yangu ambaye tupe jina la Q ni binti mdogo tu miaka 25 ameolewa na an amtoto mmoja amebahatika kusoma mpaka form six na badaye akasoma certificate IFM ya insurance bada ya kumaliza hiyo cert hakuweza kuendelea tena na masomo wala hakufanya kazi akawa mama wa nyumbani huku mumewe akimuanbia atamtafutia kaz na atamuendeleza mume wake ni marketin manager ofisi moja hapa mjini hatakiQ afanye kazi anataka awe mama wanyumbani kiukweli ukimuangalia q amebadilika hana confidence ni miaka minne yupo tu ka mama wa nyumbani hata ndugu zake anashindwa kuwaface hana rafiki zaid ya mimi anajifungia ndani hatoki wala hatembelei mtu ameniomba ushauri amechoka kua golkipa anataka ondoke na mimi nkaona niwashikirishe maGreat thinker nilisahau kusoma kote kasomeshwa na mama na mume w ake hamheshimu mama yake hata kidogo please naombeni msaidie kama unaona ni hadithi usichangie
Nitahahakisha amepata pole yako The boss kweli anatia huruma hata kujiendeleza huko cdhani kama mume wake atamruhusu kwani mpaka leo hii hajaply chuo chochote ndo maana anasema afanye maamuzi magumu ya kuondoka
mume wake ndo alitaka amzalishe fasta na alimuahidi pindi atapojifungua ataendelea lakini badaye alibadilika mpaka mtoto wake afikishe miaka mitatu
Asiachane naye. Yeye atumie network yake kutafuta kazi, then aanze kufanya kazi, suala la kazi ni maisha yaomume wake ndo alitaka amzalishe fasta na alimuahidi pindi atapojifungua ataendelea lakini badaye alibadilika mpaka mtoto wake afikishe miaka mitatu
ataondoka kwenda wapi?
huko kuna uhakika wa maisha na mtoto?
Dah... Haya maisha ni ya kukaa na kumtegemea mwanaume kweli jamani? Maisha ya sasa ni kusaidiana.. Na asikwambie mtu kazi inaleta heshima ndani ya nyumba.. Aaache kujibweteka atafute kazi huyo rafiki yako.. Na kuhusu kumuacha mumewe asithubutu kabisaa.. Aongee nae tuu kwa heshima na ustaarabu wataelewana... Leo hii akimuacha mumewe kesho huyo mumewe atakuja JF kutafuta mke mwingine.. Hasara kwa nani?
Loh. Jamaa ni mtu wa mfumo dume! Na pia sioni kabisa kuwa anamjali
mwenzi wake. Nilitarajia kuwa angepashwa kumsikiliza kuwa nae anataka nini katika maisha yake.
Command ya nini kuwa mpaka mtoto afikishe miaka mitatu?. Mtoto ni wa kwao wote wangeweza
kujadiliana kwa pamoja wafanyaje kuhakikisha kuwa mtoto anapata huduma ili mkewe nae ajiendeleze
au atafute kazi kwani kufanya hivyo ni kwa faida ya familia. On my views jamaa ashauriwe, sioni kuwa afanyavyo ni sawa. Itasaidia kuepusha hizo hisia za mke za kutaka kuondoka. Mazingira yoyote yanayojitikeza katika familia wote mume na mke wanapaswa kuuvaa uhusika.
Mwambie akae na mumewe aongee nae kuwa amechoka kukaa nyumbani na kuwa golikipa.
Kama hatashindwa kumsikiliza, afanye maamuzi magumu hakuna njia nyingine.
Ameshakaa naye sana na hataki kuelewa anataka abaki mama wa nyumbani
Kwa ninavyomjua huyo mwanaume ni dikteta wa maamuzi wala hashauriki