Anataka kusema "nisamehe" ila anashindwa

Nilijuana na Lilian (Jina si halisi) mwaka 2017 kupitia shirika moja la mazingira wakati najitolea, yas, ni mtu mzima kidogo ukifananisha na sisi tulio mwanzoni mwa 20s.

Mazoea nae yalikuwa ya kawaida, na mimi nimemmpa heshima ya UDADA, lakini pia kwangu ni boss wangu, nyakati fulani mwaka 2019, kupitia WhatsApp status yake alipost chombo, naaam, chombo haswa, sumaku ya mwanamume macho, alipost mdada aliyenichukua akili kwa mara ya kwanza. "Love at first sight"

Mtoto mithili ya Kipemba, mzurii, ikabidi nimuulize anaitwa nani, akasema "Zuriath" (Jina si halisi), nikamwambia tuu Msalimie".

Hilo neno likampeleka mbali sana Madam Lily, wakati huo mimi nipo chuoni, mwaka wa mwisho, yani sina hili wala lile, mwenzangu akanitumia namba zake za simu....
Jamani weee' kutongoza mtu uliyevutiwa nae kaziiii, (domo chenga linachangia pia )

Ikanibidi nim text, hata hivo Zuri sio mkali, wala hakuwa na reaction mbaya, akanikaribisha kabisa kwenye uwanja wake wa CHAT

Wanaume, wanaume, wanaume wenzangu, nimewaita mara tatu, yaani usiku kucha nikawa nahangaika kutongoza mtu ambae kimsingi simjui zaidi ya sura tu , na Mungu alivo wa ajabu dada wa watu kanikubalia (wanawake wana huruma) nikarudi Dar, nikakutana nae, let me tell you, demu ni mtoto wa Kigogo mmoja Bandarini, nyie nyie nyiee!! Sikuwa na amini kama ndio mimi namiliki moyo wa yule dada.
Siku zikaenda, mwenzangu akasafiri kwenda Unguja, kiukweli sikuwa na siko vizuri kiuchumi, niliona kabisa nikipoteza nafasi yangu kama Mwanamume, sio poa, ingawa hilo yeye wala hakulijali wala nini, mjomba nikajikuta Marioo.

Siku zikaenda, mara akaanza kuwa hapokei simu zangu, mara hataki kuongea sana na mimi akidai kuwa busy. Roho iliniuma sana, kama ilivo ada kwa wanawake kuwa desperate sana na ndoa, sijui nani alimvutia Zuriath akatafuta kisingizio cha kuniacha, akaniambia tuwe marafiki tuu, kwa sababu hawezi kuwa nami mkristo, hakuna kauli kwenye mahusiano iliwahi kuchana moyo kama hio, alidai wazazi wake wangekataa as if nilimwambia nataka nimuoe that time.

Nimekaa nimtafakari sanaa, nikahitimisha kuwa Dini sio kigezo bali Uchumi, sina hela, indeed, sina pesa, mtoto akanitema kiivyo. Nami nikaona isiwe shida, meseji yangu ya mwisho niliandika "In God's Will" yaani kwa mapenzi ya Mungu, alilotaka liwe.

Sasaa nimekaaa Mpaka mwezi wa 11, mwaka huu tangu mwezi wa 10 mwaka jana, nashangaa madam Lily ananiambia

"Zuri amenitumia ujumbe anataka kukuomba msamaha lakini anashindwa, roho inamsuta alikufanya kitu kibaya"

Kiukweli nikifikiria hiko kitu kibaya kaa upande wangu sikioni, kwa sababu naona bora alivyoniambia kuliko angeondoka Kimya Kimya, nimekuwa muoga, sitaki kumtafuta, nahisi mambo yaweza kuwa mabaya ten, nisije kuwekwa punch nyingine, ni hatari.
Nipe namba ya Madam Lily nimkumbushe kitu
 
Sijawahi na sitowahi kuvunga kwenye "chiu" vinginevyo kuwe kuna tatizo kubwa
 
chini ya maji kwanza mkuu kwasababu ukiflow na matakwa yake ndo udhaifu utatumika vyema
lakini kwa taadhima Madam Lily husali kanisa gani
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom