Anataka kumwua kisa kamkataa!!!

OIL CHAFU

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2012
Posts
996
Reaction score
776
KUNA RAFIKI YANGU AMENIPIGIA SIMU JANA, Ameogopa sana ANAOMBA USHAURI,
Ni mwanachuo, ametongozwa na wanaume wawili humo darasani kwao, amewakataa wote wawili,
Sasa, kuna mmoja wa hao wanaume anatoka Mbeya ni Mnyakyusa amemtishia huyo binti laivu kuwa kama hataki kuwa naye asimuone na mwanaume yeyote hapo chuoni au popote pale, la sivyo atamwua.

Na sasa binti hata akisimama na mtu barabarani kuongea au kusalimiana naye, jamaa huyo ashakuja na kuhoji huyo nani wako. Jamani huu ni ushamba? au ana matatizo ya akili? Mapenzi gani haya? Binti kashaonyesha hampendi jamaa analazimisha. Sasa ikitokea kweli kaua ndo atafaidi? Ni matumaini yangu kama huyo mtu anakuja humu jamvini acha kabisa hiyo tabia, na upate ushauri nasaha kama una matatizo ya akili, pia wadau hebu mpeni somo huyu mtu, aache ushamba mbona wadada wengi siku hizi warembo wanazaliwa kila siku?
 
Ni suala la kureport Police haraka......huyo aweza kuwa yuko obssessed na mdada, ishawahi nitokea anatakiwa pia huyo dada mpe karipio kali huyo mtu likiendana na kureport Polisi
 
ampe karipio mbele ya darasa zima kuwa hampendi na asimfuate futa
pili aripoti polisi fasta kama walivoshauri hapo juu, nadhani kila chuo kina police post karibu
ili polisi nao wamwite wamwonye yasije kutokea kama yaliotokea mabibo hostel mwaka juzi akachinjwa kwa kisu
 
kama vipi ampe tu atakuwa kamfia kiukweli huyo
 
Kama kamchuna jamaa lazima amlipe,inauma demu anakula pesa zako halafu kupanua mapaja hataki
 
Awahi police, ila awe makini kwani police nao wagwadu, wasije mtishia na mabinduki akaachia mzigo kwa afande.
 
Ni PM jina lake, tumshikishe ukuta huyo wakuja.
 
Ukimuona tu, bonyeza kitufe cha "report abuse" Mods watamshuhulikia immediately!!
 
Shosti wako atoe taarifa kwa maprinciples wa hapo chuoni waangalie watamsaidiaje,na asithubutu akamkubali kwani inonyesha kijana ni mtata na ni mgomvi,hivyo kumkubali sio suluhisho ila ni kuongeza matatizo na stress,ametoswa anakuwa hivyo je akikubaliwa?itakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…