Anataka kumpa mwanangu mfilipine aoondoke nae | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anataka kumpa mwanangu mfilipine aoondoke nae

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by raja wa raha, Feb 14, 2012.

 1. r

  raja wa raha New Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilipo maliza kidato cha sita nilienda kuishi katika kijiji cha usangi,ambacho kipo wilayani mwanga mkoa wa kilimanjaro,nilikutan na mwanadada mmoja aliyeitwa neema.Ambaye nilifanikiwa kuanzisha nae uhusiano.kwa bahati mbay au nzuri hatukuweza kudumu kwa muda mrefu,sabbu aliondoka kwa ghafla bila kuniaga na kubadilisha namba ya simu.bila kujua hili wala lile nikaamua kuachana na habari za kumtafute tena.zaidi niliambiwa kua yuko anaishi jijini dar es salam.Baada ya miezi kumi na mbili kupita nikiwa nimefanikiwa kujiunga na chuo kikuu cha sokoine,nilipokea simu ikwa na namba mpya,Alinifahamisha kua yy ni Neema,nilikua na furahi coz it was a long tym htujaonana wala kuwasiliana mm na yy,katika kupiga story mbili tatu akanieleza kua amejifungua mtoto wa kike na niwa kwangu kwa hiyo nimpe jina la kumuita mtoto.nikamuuliza inakuaje siku zote hizo awe na mimba yangu na asinieleze chochote,Akanijibu mi cha huhimu nimpe jina na nisubiri mtoto akiwa mkubwa ataniletea mtoto wangu so nisiwe na shida.
  Akanieleza viungo vyote nilivo fanana na mtoto ,kwamba aliamua kuondoka usangi kwa sababu alilazimishwa na wazazi wake.na yy mwenyewe hakutaka kuniambia kwa kua alijua nitamkataa mtoto.maisha yaliendelea kwenda huku 2kiwa tunawasiliana mara moja moja ,likizo ilipofika nilikua field arusha ananijulisha kua yuko Usangi ,nikapanda gari na kwenda ili nimuone mwanangu,kufika namtafuta akaniambia amesha ondoka.katika kuuliza ndugu zake wakaniambia kua Neema hana mtoto.Nikabaki nikiwa nimechanganyikiwa na sielewi wa kumuamini.ilipo fika likizo nyingine ambayo ilikua december kufuatia januari 2012,nilifunga safari mpa Dar na kufika mpaka uwanja wa ndege alipokua anakaa,alinikaribisha kwake na akaniambiie kabla hajanionyesha mtoto anataka anieleze jinsi alivo mlea mtoto.''akanimbia wakati akiwa na ujauzito wa miezi nane alikutana na Mphilipine ambaye alimtongoza akiwa katika kipindi hicho,akamsaidia kulea mimba na mtoto alipo zaliwa pia akawa anamlea.kwa sababu alikosa msaada wowote kutoka nyumbani kwa kua alikua ametoroka nyumbani ikabidi akubali yote yale atakayo ambiwa na Mphilipine.huyu kaka wa kigeni akataka akamchumbie huyu binti na kwenda kumtolea mahari,wazazi wake wakakubali ijapokua hawajui mtoto ni wa nani,lakini walimkataza mtoto asije akamjua baba yake.yule kaka aliweza kutoa mahari ya shilingi milioni moja(1,000,000,000)''mwisho wa siku aligoma kunionyesha mtoto na akanipa picha ya mtoto na ni kweli 2mefanana naye.akasema anahofu kua huenda nikamnyang'anya mtoto kama nitamwona.ikanibidi niondoke bila kuwa na mafnikio.baada ya wiki 3 kupita alinipigia simu na kuniambia kua yule mfilipine amepata likizo ya mwezi mmoja na anataka aondoke na mtoto aende nae huko kwao,ikiwa yeey ndo kamlea mtoto je nilkweli atamrudisha? ,na asipo mrudisha inamana ndo nitapoteza damu yangu hivo ikakulie ughaibuni.?naombeni mnisaidie mawazo akili yangu sasa imesimama

  ahsanteni
  raja wa raha
   
 2. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Pa kuanzia ni kwa huyo dada mama wa mtoto, mwambie akupe kadi ya clinic ya mtoto ya wakati ule alokuwa na mimba, kwa kutumia card hiyo utapata hospitali alipojifungilia, hapo utapata hati ya mtoto kuzaliwa, itakuwa na jina la baba wa mtoto endapo aliwaambia ukweli. Baada ya hapo toa taarifa uhamiaji haraka uhamiaji haraka na Ili kucheki uhalali wa huyo mfilipino kumliki huyo mtoto wakati wewe ukiendelea na vipimo vya DNA. Asiondoke nchini pasipo kuhakiki uhalali wake kuwa baba wa mtoto, anaweza kuwa step-father wa mwanao sabab amelea mimba hadi sasa matunzo, ila ijulikane kuwa wewe ndio biological father. Baada ya mkubaliane kiume!
   
 3. Eghorohe

  Eghorohe JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tutafute sisi Makachero tuoneshe anapokaa tu inatosha,tutamnasa kisheria hadi kwenye DNA na wewe utaujua ukweli.
   
 4. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Huyo dada ulipomuona anaonekana km ni mtu aliyejifungua yaani ana dalili ya kuwa na mtoto???
  Km ni kweli wewe ni baba halali wa mtoto huyo kwanini amfiche asikuoneshe???
  Umefika hadi nyumbani kwa huyo dada anapoishi, mara zote kilio cha mtoto akiwa ndani au chumbani hakijifichi je ulisikia hata sauti ya mtoto kulia au alimpeleka kwa jirani???
  Naomba unijibu haya maswali kabla sijaendelea zaidi.
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ndo tabu ya kuzaazaa kiholela kama ngedere. cha msingi tafuta kama afu 50 hamsini uende polisi waje na difenda wamzoe huyo mwanamke kisha wamsweke sero, atasema mwenyewe ukweli wote na ataacha upuzi na danadana za kijinga.
   
 6. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mbona huyo dada anacheza na akili yako? mtoto hujamuona na kila siku anakupa vigezo vipya,kwamtazamo wangu au niseme ningekua wewe ningemwambia afanye anavyo jisikia na huyo mtoto sababu ukiwa kama baba mtoto vp akufiche au aliogopa kukwambia ungeweza kumkata sasa vp ungekata wakati wa mimba umkubali sasa keshazaliwa?
   
 7. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huyu brother ni mwoga tu, kama anapafaham wanapoishi hapo uwanja wa ndege iweje ashindwe hata kutoa taarifa kwa balozi wa nyumba kumi kuwa anadhulumiwa mtoto? kisha balozi atawaita watuhumiwa waje na mtoto, au kwa mtendaji! shituka!
   
 8. m

  mkazamjomba Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  changa la macho sio lazima umwagiwe na chizi
   
Loading...