Anataka kukopeshwa Mahari

Sasa kama ataki Ku assist analalamika nn coz situation ameiona ilivyo ukizingatia wataenda Mbele huko kupeana company kwenye shida na raha
mmmmh ku assist iyo vepeee, kila mtu anawajibu wake kwakweli
 
Ana mshahara mdogo wa wizarani ila nadhani hana nia tu, kwani wangapi wanafanya kazi kwenye mawizara na wanalea familia zao vizuri
basi ahesabu maumivu maana hakuna muoaji hapo!
 
Tatizo vjana siku hizi mme-mix culture!
Uzungu na uaAfrika ni sawa na mashariki na magharibi, yaani zote ni dira za dunia lakini zina uelekeo tofauti.
Mleta mada nadhani umeathiriwa na niliyoyasema.
Kifupi hapo hapakuwa na swali wala kuomba ushauri. Jambo hilo halikubaliki na ni haramu.
Labda nikueleze mtoa mada kuwa uzunguzungu wenu ndiyo unaotutukanisha na kutufedhehesha sana wazazi wenu.
Tunawalea na kuwafundisha maadali mena na kuwasomesha kwa karo za kidhalilishaji kwa kuwa tunajikamua na kujinyima sana.
Lakini linapokuja suala la kujitegemea, mnatuangusha.
Mila za kiafrika ni mwiko wachumba kukaribiana hadi kupikiana chakula na kulala pamoja kabla ya kufunga ndoa.
Kingine ni kwamba, ndoa haiwezi kufungwa kabla ya mahari iliyoafikiwa kutolewa.
Utaratibu huo ukizingatiwa, huongeza ari na kasi ya muoaji kufikia malengo yake na masharti hayo ni kipimo halisi cha upendo wa dhati.
Mwanamume mwenye nia na mapenzi ya kweli, hata awe ni masikini kiasi gani, yupo radhi ajinyime hata kula aweze kutimiza kiwango cha mahari alichopangiwa aweze kupata mke.
Hii ya kujirahisirahisi kumvulia nguo na kumpikia mwanaume kama vile mke,imeshusha sana hadhi ya wasichana wa siku hizi kuweza kuolewa.
Unalala naye na unampikia, kitu gani zaidi ya mambo hayo ambayo tayari anayapata bure kitakachomsukuma mwanaume apaparikie ndoa?
 
dah anatakiwa kujipanga, mahari sikukopeshwa.
ndoa sio lelemama, lazima ajipange
 
Kama yuko tayari kuweka dhamana vitu vyake, Dada amkopeshe ila Kwa kutumia watu wengine na asipolipa vitu vyake vipigwe mnada.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…